Kitabu.New World Order
Mwandishi.Ralph Epperson
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Chapter 13 The Pyramid of Giza
Mwandishi anasema kuwa Masonia wanakubaliana kabisa na Wamisiri kuwa Osiris alikuwa mungu(Osiris ni miongoni mwa miungu ya wamisiri) ambaye ni mungu jua,ambaye kwa baadhi ya wamisiri wanaamini kuwa yale Piramid ni mahekalu yaliyojengwa kwa amri ya Osiris…zinaitwa Pyramid of Gizeh inatamkwa Giza.Itakumbukwa kuwa watawala wa Misri maarufu kama Farao walikuwa na miungu kadhaa,waliyoiamini na inaaminika kuwa Farao wa aliyejenga Piramid alijenga kwa maelekezo ya mungu Osiris
Kwa mujibu wa watafiti mbalimbali kuhusu Piramid za Misiri,wanakubaliana kuwa ujenzi wake ulikuwa wa akili ya hali ya juu,ni moja ya uhandisi maridadi kabisa kufanywa na binadamu,na ndani ya Pramid kuna matumizi kadhaa,ikiwepo ibada,korido pana ya inchi 6000,kaburi etc lina mita 30 chini.Kimsingi kuna jamii mbalimbali za Dunia ambazo huenda kufanya ibada kwenye hizi Pramid(Pramid ni moja ya eneo linalopokea watalii wengi sana Africa) wengi huenda kama kutalii lakini ni sehemu ya ibada na ibada hizi zimeanza miaka mingi…zaidi ya miaka elfu sita
Mwandishi anasema kwa msingi huu sio kweli kuwa Pramid zilijengwa kwa misngi ya kuzika (makaburi)kama ambavyo imekuwa ikielezewa na watu wengi.Kuna uhusiano mkuwa wa Ibada za miungu,hasa mungu jua na New Agers,eitha ndani kabisa under ground kuna chamber maarufu ambayo huitwa Kings chambers na Queen Chamber hizi chamber zimewekewa Ventilator kwa ajili ya kuruhusu hewa
Chapter 14 Obelisks
Mwandishi anasema kuwa OBELISKS ni jiwe/mwamba mkubwaa wenye pembe nne,mfano wa mnara mkubwa kwa sasa upo unaitwa Washington Monument,wa pili ni Central park New York)ulihamishiwa kutoka Misiri mwaka 1831)wa tatu upo Vatican ambao Papa huelekea hapo wakati akihutubia(Lazima akae kuelekea mnara uliko)na wanne upo Alexandria Misiri.Rejea kila alama/ishara ina maana kubwa kwa masonia tumeona kuwa jua na nyota ni mojawapo ya alama takatifu kwao.Hivo basi kwa masonia wanaamini kuwa OBELISKS ni kiwakilishi cha mungu jua ambaye huabudiwa na wamisri na wao masonia huabudu jua kwa kuwa jua ni chazo cha Nuru na Nuru ni chanzo cha hekima na maarifa
Mwandishi anasema mnara wa Washington Monument ulijengwa kumuenzi Rais wa kwanza wa USA George Washington ambaye alikuwa active member wa Masonia na aliyetoa mchango mkubwa sana kwa jamii za siri.Mnara huu una urefu wa miguu 555.Ujenzi wake ulianza mwaka 1833 na kukamilika 1848,jumla ya paundi za capstone 3300 zilitumika kukamilisha namba 33 ambayo ndio namba ya juu kabisa ya Masonia.Wakati wa Ujenzi watu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali walichangia ujenzi wake na walitoa mawe ya kumbukumbu(Mfano wa ile dhahabu ya malikia wa Sheba aliyompa Mfalme Suleiman)au ( Tausi ambao wastaafu wamepewa ni aina ya ndege wa ukumbusho/kumbukumbu) sasa basi Zaidi ya jamii 188 zilichangia mawe ya kumbukumbu na jamii 33 kati ya hizo zilikuwa jamii za siri za Masonia,ndio kusema wanatoa hela mfuko wa kulia wanahamishia kushoto….namba 33 inajitokeza tena hapo
Mwandishi anasema kuwa gharama ya ujenzi huu nayo iliakisi tena namba ya Masonia namba 13..ujenzi uligharimu usd 1,300,000(rejea ni mwaka 1848 ndio ujenzi ulikamilika,ni fedha nyingi hata kwa dunia ya leo) mnara huu una madirisha nane,mawili kila upande,madirisha sita yana ukubwa sawa ila dirisha namba saba na namba nane ambalo linatazama Mashariki ni makubwa Zaidi,kumbuka kuwa Masonia huamini kuwa mungu wao wanamwita Master huketi Mashariki hivo upande wa mashariki ni upande takatifu kwao.
Namba 13 ni moja ya alama muhimu sana kwa Masonia….namba ya Uasi (kwenye hotel nyingi za nyota tano huwa hakuna chumba chenye namba 13,maana inaaminika ni namba ya uasi,namba isiyokuwa na bahati,namba ya balaa na mikosi)
Kwa ujumla Mnara wa Washington una alama nyingi za namba na vielelezo ambavo vinadhibitiha kuwa ni mnara wa masonia.
Kimsingi hizi Obelsks zinaaminiwa kuwa watu wa kale hasa Misri ya kale ambayo ni moja ya kielelezo cha ustaarabu wa binadamu walikuwa wanamahusiano ya kiibada na miungo hii,hivo masonia wa leo wanaji attach nao.(kuna baadhi ya jamii Tanzania humwita mtoto jina la mtu aliyefanikiwa wakiamini na yeye atafanikiwa,wanafanya attachment)