Kitabu: Mfanyabiashara wa Venice.

Kitabu: Mfanyabiashara wa Venice.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,884
Reaction score
18,824
Tafsiri ya kitabu The Merchant of Venice.
1939.

SHYLOCK (SHAILOKI) NA ANTONIO

SHYLOCK, Myahudi, alikaa Venice (mji mmoja wa Uitalia). Alikuwa mkopeshaji fedha wa namna mbaya kabisa. Yaani yeye hungoja hadi mchuuzi awe katika hali ya dhiki kubwa ya kuhitaji fedha; ndipo Shylock humkopesha fedha kwa kumtoza kadiri iliyo kubwa ya faida. Kwa kufanya hivi alijipatia utajiri mkubwa. Alikuwa na moyo mgumu sana tena katili, kwa sababu hii alichukiwa sana na watu wote walio wema, na hasa alichukiwa sana na Antonio, kijana mchuuzi wa Venice.

Antonio pia alikuwa na mazoea ya kuwakopesha fedha wachuuzi walipokuwa na dhiki, lakini yeye abadan hakutwaa faida yo yote kwa fedha aliyokopesha. Kwa hiyo ulikuwapo uadui mkubwa baina ya Shylock mshupavu na Antonio mchuuzi karimu. Kila wakati Antonio alipomwona Shylock penye Rialto, yaani mahali katika mji wa Venice palipofanyika shughuli ya kukopesha fedha, alizoea kumsuta huyu Myahudi kwa sababu ya vitendo vyake vya ushupavu.

Antonio alipozungumza katika Rialto habari za ukatili wa Shylock, Shylock mwenyewe alijifanya kama hazimhusu hizo, lakini katika dhamiri yake sikuzote alikuwa akitazamia sana apate wasaa kumdhuru yule kijana mchuuzi.
 
BASSANIO, RAFIKI YAKE ANTONIO​

ANTONIO alikuwa mtu karimu sana katika Venice; alikuwa mtu mwungwana ambaye hakuchoka kamwe kuwasaidia wengine. Baadhi ya watu walimnena ya kuwa alionyesha busara pevu mno ya heshima katika shughuli zake kuliko mchuuzi ye yote katika Uitalia yote. Kwa sababu hii alipendwa vikubwa mno na wenzake.

Baina ya marafiki waliompenda Antonio, mmoja aliyekuwa mfaragha na mpenzi kabisa katika moyo wa Antonio alikuwa Bassanio. Ingawa Bassanio alizaliwa katika jamaa ya namna iliyo maarufu kabisa katika Venice, lakini hakuwa tajiri. Kadhalika huyu Bassanio kwa kidogo alipendelea kuishi katika hali ya fahari, kama vile watu vijana wa jamaa iliyo maarufu wenye utajiri kidogo waelekeavyo kufanya. Ilimtukia kuwa alitumia karibu utajiri wake kidogo wote aliorithi kwa watu wa ukoo wake. Hata pana wakati Bassanio hakuwa na fedha iliyomsalia, lakini, alipokuwa na haja ya msaada, Antonio alikuwa tayari kumsaidia. Ilionekana kama kwamba walikuwa na moyo mmoja na shirika ya utajiri baina yao.

Siku moja Bassanio alikuja kwa Antonio akamwaridhia ya kwamba alitamani kumwoa bibi mmoja aliyempenda kwa mapenzi makubwa. Baba wa yule bibi alikufa siku zile zile za karibuni, akawa amemwachia binti yake utajiri mkubwa. Bassanio alisema ya kuwa wakati wa uhai wa baba wa yule bibi, alizoea kwenda nyumbani kwa yule bibi. Bibi huyu pana wakati alionekana kusema kwa macho yake ya kwamba kama Bassanio akihitaji kumshika mkono waoane ata- mkubali. Walakini, Bassanio kwa utovu wa fedha ya kumtimizia matumizi kwa kiasi cha kujionyesha ya kwamba yu mchumba wa bibi aliye tajiri hivi, alikuja kwa Antonio, akitumai kwamba Antonio atazidi kumfanyia hisani kama alivyozoea kumfanyia, kwa kumkopesha shilingi ishirini na saba elfu.

Antonio hakuwa na fedha iliyo tayari ili kumkopesha rafiki yake, lakini alikuwa akitazamia merikebu zitakazorejea punde, zikileta bidhaa nyingi kutoka nchi nyinginezo. Akatoa shauri ya kuwa yeye na Bassanio waende kwa Shylock, tajiri mkopeshaji fedha, ili wapate fedha kwa tumaini la zile merikebu.
 
AGANO LA AJABU
ANTONIO na Bassanio walikwenda pamoja kwa Shylock. Antonio akamwomba yule Myahudi amkopeshe shilingi ishirini na saba elfu. Naye aliahidi kulipa faida iwayo yote atakayotaka Shylock. Shylock aliposikia hivi, aliwaza nafsini mwake, “Mara nikimpata Antonio katika uwezo wangu nitamtesa kwa ajili ya madhara yote aliyonitenda. Anatuchukia sana sisi Wayahudi; anakopesha fedha nyingi wala hataki faida; na huko katika Rialto hunisibabi na biashara yangu.' Lakini Shylock hakujibu kwa haraka, hata Antonio alikosa subira kwa sababu ya kutaka fedha, akasema: Shylock, unasikia? Utanikopesha fedha ?"

Kwa hoja hii yule Myahudi alijibu hivi: "Bwana Antonio, wewe kule Rialto mara nyingi umenisuta kwa sababu ya namna ninavyokopesha fedha, nami nimestahimili maneno yako kwa subira. Tena, umeniita mimi kafiri, hata pengine umenipiga mateke kwa mguu wako kama kwamba mimi ni mbwa. Vema, imetukia sasa ya kwamba unahitaji msaada wangu. Umekuja kwangu na kusema, Shylock nikopeshe fedha.' Je, Mbwa ana fedha? Yawezekana mbwa akukopeshe wewe shilingi elfu ishirini na saba? Naweza kujinyenyekea na kusema, Bwana adili; Jumatano iliyopita ulinicheka; wakati mwingine uliniita mbwa; na malipo kwa ajili ya haya uliyonitenda, ndiyo mimi nikukopeshe fedha "!"

Kwa maneno haya Antonio alijibu hivi, “Napenda kukuita mbwa tena, na kukusibabi kati ya wafanyi biashara wa Rialto, hata napenda kugeuza uso wangu ninaposema na wewe. Ikiwa utanikopesha hiyo fedha, nikopeshe, wala si kama rafiki, lakini kama adui. Kwa hivi kama nikihalifu miadi, utaweza kuchagiza malipo kamili pasipo haya."

Shylock akasema, "Angalia jinsi ulivyohamaki. Mimi nataka tuwe marafiki, tusuhubiane. Mimi tayari kusahau maovu uliyonitenda. Nitakidhi matakwa yako, wala sitatoza faida kwa ajili ya fedha yangu."

Ahadi hii njema ya kinjenje ilimshangaza Antonio vikubwa mno. Ndipo Shylock, kama kwamba akitaka kuzidi kwa wema kulinasa pendo la Antonio, alisema tena ya kwamba atamkopesha shilingi elfu ishirini na saba, wala hatatoza faida kwa fedha yake. Ila alifanya sharti moja tu- ndiyo kwamba Antonio na yeye waende kwa mwana sheria, na huko wakaandike sahihi zao kwa kicheko na furaha agano ya kuwa Antonio asipolipa fedha kwa siku watakazowekeana miadi, itamlazimu kulipa ratli ya nyama, ikatwe katika sehemu yo yote ya mwili wake atakaporidhia Shylock.

Antonio akasema, Nakubali, nitaandika sahihi yangu kwa sharti hii, na kusema ya kuwa Myahudi ana uhisani mwingi."

Bassanio hakutaka Antonio aitilie sahihi sharti kama hii kwa ajili yake; lakini Antonio alizidi kusisitiza ya kwamba ataiandika sahihi, kwa sababu alikuwa na hakika kwamba merikebu zake zitarejea kabla ya siku ya malipo, zitamwasilishia mali nyingi zaidi kushinda thamani ya ile fedha.

Shylock aliposikia mabishano yao, alisema, "Ohoo, angalia jinsi hawa Wakristo wasivyokuwa na muamana! Mambo magumu yao wenyewe yafunza kutowaamini wengine. Tafadhali Bassanio, ebu niambie neno moja: Kama Antonio atahalifu agano lake kwa kukosa kunilipa katika au kabla ya siku tuliyowekeana miadi, nitapata faida gani kwa kuchagiza maneno ya agano letu ? Ratli ya nyama ya mwanadamu kutwaliwa katika mwili wa mtu, haina thamani wala faida kama nyama ya kondoo au ya ng'ombe.

Mimi nasema hivi ili nipate upendeleo wake, nami namtolea mapenzi yangu, akiyakubali, nitafurahi, la sivyo, basi kwa herini."

Hata mwisho, kinyume cha shauri la Bassanio, ambaye hakuyaamini maneno ya yule Myahudi, na kwa sababu hiyo hakuridhia rafiki yake ajitie hatarini kwa ajili yake, Antonio aliiandikia sahihi yake ile sharti. Kwa habari ya ratli ya nyama, yeye alidhani sharti imetiwa katika agano (kama alivyosema yule Myahudi) kwa mzaha tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom