Kitabu kipya sokoni!

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Shalom! Jana nilipata wasaa wa kuzindua kitabu changu cha mfumo wa pdf, kinachoitwa "NJIA PANDA YA USAWA WA KIJINSIA"; kuandika kitabu hiki kumetokana na mguso niliopokea kutoka kwa namna jamii ilivyo sasa, hasa matokeo ya harakati za usawa wa kijinsia kwenye mitazamo ya vijana wa leo.

Zipo changamoto nyingi ambazo zimejadiliwa kwenye kitabu, ila kwa ufupi, nitajadili kwa ufupi makosa matano ambayo yanatafuna jamii leo hii hasa kundi hili, ambayo kama yatabaki yalivyo, kuna hatari kubwa ya anguko la jamii kwa miaka 20 ijayo.

1. Vijana wengi wa Kike hutafsiri Usawa wa Kijinsia kama kuwa na haiba, tabia, mamlaka au kaliba ya Kiume. Wanawake wanaacha haiba yao ya kike (femininity) na kukumbatia kaliba ya kiume, wanajikuta wapo ulimwetu tofauti na kwao. Wanageuka watumwa.

2. Vijana wengi tunawaza kufanya kazi zenye fedha na vyeo vyenye nguvu, ila hatuwazi kuwa baba au mama bora kwa familia zetu. Jamii imara huanzia nyumbani, sio kwenye cheo.

3. Tunaamini kila ajenda itokayo Magharibi ina lengo la kutuimarisha; tunasahau ya kuwa hawa watu ndio waliuwa elimu yetu ya kijinsia, iliyotufanya kuwa imara kimajukumu, wakatupa elimu ya kutuandaa kuwa vibarua, leo unakutana na boss wa kampuni ambaye hajui namna ya kuwa mzazi/mwanandoa. Ni aibu.

4. Kutowaza kuwa, uhuru wa mtu binafsi unaweza kuwa utumwa wa mtu binafsi; jamii ya leo inaamini katika uhuru na chaguo la mtu juu ya namna ya kuishi, leo tumekuwa watumwa wa uhuru wetu, tunafanya mambo mengi ya kupotoka kwa jina la uhuru binafsi.

5. Kushindwa kutofautisha mapenzi, mahusiano n ngono. Haya ni mambo makuu matatu, kuwa na mahusiano sio kupendana, kupendana sio kufanya ngono, na unaweza kufanya ngono bila kuhusiana au kupendana. Leo vijana wanalia kwenye mahusiano, hawajui hayana uhusiano na ngono na mapenzi kama wanavyodai.

Licha ya mambo hayo, nimegusia kwa ufupi namna gani kuanguka kwa elimu ya jinsia iliyokuwa ikitolewa na Jando la Unyago ilivyotugeuza watumwa katika ardhi yetu wenyewe.

Unaweza kupata copy yako kupitia 0684436954

Lipa namba 5635955 Vodacom. Jina Dominick Diwani.

Tuungane kukomboa kizazi chetu na kijacho.
View attachment 2817351View attachment 2817354
Blue%20Aqua%20Minimalist%20Sea%20Soothes%20the%20Soul%20Quote%20Instagram%20Post_20231117_1233...jpg
 
Back
Top Bottom