Kitabu kipya: Maisha ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu 1957 - 2014

Mzee Mohamed Said nakihitaji hiki kitabu lakini niko mikoani

Naomba mawasiliano yako
 
Mohamed Said
Sheikh Mohamed Said unaweza kutupa historia fupi ya Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Ahad Salum. Ni mwenyeji wa wapi ana sifa zipi hasa zilizompa nafasi kubwa aliyonayo akiwaacha wakongwe na masheikh wengine wa Dsm
 
Faru...
Hakika niliahidi lakini clip kwa kuwa imewekwa na kuna mwenzangu kasherehesha nimeona hakuna haja ya mie kuweka sherehe juu ya sherehe.

Au hukupendezwa na uamuzi huu?
 
Huyu marehemu alikuwa hatari kwa usalama wa taifa kwa uchochezi aliokuwa akiufanya tunasema anaamini uislamu wa siasa kali kama wa kipindi kile mtume anaueneza uislamu. Kufa ilikuwa halali yake kwani mbegu alizokuwa anapanda zinaumiza wengi mpaka leo. Apumzike kila roho itaonja umauti.
 
Kwanini hizo kopi usigawe bure?

Kwanini unabidhaaisha maarifa?

Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kaingia katika historia ya Dar es Salaam katika kifo chake.

Bahari ya watu waliojazana Msikiti wa Kichangani kuja kuswalia jeneza lake na kisha kulifata nyuma jeneza hilo hadi Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa haijapatapo kuonekana.

Sheikh Ilunga ni ''mgeni'' katika mji wa Dar es Salaam kwa maana ya kuwa hakuzaliwa Dar es Salaam wala hakuwahi kuishi Dar es Salaam wala hakuweza kujinasibu kwa lolote au chochote katika mji wa Dar es Salaam.

Alikuwa akija na kuondoka zamani akirejea kwao Tabora na baadae baada ya kuhamia Mwanza, akija Dar es Salaam na kurejea Mwanza.

Iweje leo mji mzima wa Dar es Salaam usimame na utoke kuja kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu?

Hakika hili ni swali linalotaka majibu ya kuridhisha.
Jibu ni dogo na rahisi sana.

Hivi ndivyo Waislam wanavyofanya dunia nzima kila wanapofiwa na kipenzi chao.
Labda linaweza kuja swali jingine, ''kipenzi?''

Sheikh Ilunga kawaje kuwa kipenzi cha Waislam?

Naam Sheikh Ilunga Hassan Kapungu juu ya udogo wake wa umri alikuwa kipenzi cha Waislam na si Waislam wa Dar es Salaam peke yao.

Sheikh Ilunga alikuwa kipenzi cha Waislam wa Tanzania nzima.

Kibla cha kila msikiti wa Waislam katika Tanzania kilikuwa kinamkaribisha kama si kuwaidhi basi angalau asimame awasalimie nduguze Waislam.

Sheikh Ilunga alipendwa na umma hakuwa katika lile kundi la mesheikh wanaoogopa kuswali katika baadhi ya misikiti au hata kupita nje yake.

Sheikh Ilunga hakuwa katika lile kundi la masheikh wenyeji katika futari za serikali na''misikiti ya wakubwa'' lakini wageni katika misikiti ya ndugu zao Waislam maskini, Manzese au Tandale.

Kubwa Sheikh Ilunga hakukosa usingizi wala kujiona duni kwa kukosa kualikwa futari Ikulu au kualikwa katika dhifa za kitaifa akapigwa picha kavaa kanzu za kupendeza na katupia kashda za marembo kakaa na waheshimiwa na kutokea katika runinga na magazeti siku ya pili ukurasa wa mbele.

Sheikh Ilunga Hassan Kapungu hakushughulishwa na hayo.
Yeye alishughulishwa na kuliweka juu jina la Allah Subhana Wataala.

Hili ndilo lililokuwa likimshughulisha mpaka siku Allah alipomuhitimisha.
Kitabu hiki kinaeleza maisha yake mafupi hapa duniani.

Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani kwa bei ya Shs: 2,000.00 tu.
 
Kwanini hizo kopi usigawe bure?

Kwanini unabidhaaisha maarifa?
Lukubuzo,
Labda nikuulize.

Duka gani umeona vitabu vinagawiwa bure?

Juu ya hayo vitabu hivyo si mali yangu mimi ni mwandishi tu lakini mwenyewe ni Ibn Hazm Media Centre.
 
Huyu marehemu alikuwa hatari kwa usalama wa taifa kwa uchochezi aliokuwa akiufanya tunasema anaamini uislamu wa siasa kali kama wa kipindi kile mtume anaueneza uislamu. Kufa ilikuwa halali yake kwani mbegu alizokuwa anapanda zinaumiza wengi mpaka leo. Apumzike kila roho itaonja umauti.
Hakuna ambaye alishangazwa na kifo chake kwani hata yeye mwenyewe alifahamu kuwa kadiri anavyosema kuhusu mfumo kristo ndio analikaribia kaburi.
Lakini cha kujiuliza hapa ni kuwa, nini hasa kilimsukuma kuanza kusema haya hadharani? bila shaka huku wengi wanapakimbia
 
Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kaingia katika historia ya Dar es Salaam katika kifo chake.

Bahari ya watu waliojazana Msikiti wa Kichangani kuja kuswalia jeneza lake na kisha kulifata nyuma jeneza hilo hadi Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa haijapatapo kuonekana.

Sheikh Ilunga ni ''mgeni'' katika mji wa Dar es Salaam kwa maana ya kuwa hakuzaliwa Dar es Salaam wala hakuwahi kuishi Dar es Salaam wala hakuweza kujinasibu kwa lolote au chochote katika mji wa Dar es Salaam.

Alikuwa akija na kuondoka zamani akirejea kwao Tabora na baadae baada ya kuhamia Mwanza, akija Dar es Salaam na kurejea Mwanza.

Iweje leo mji mzima wa Dar es Salaam usimame na utoke kuja kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu?

Hakika hili ni swali linalotaka majibu ya kuridhisha.
Jibu ni dogo na rahisi sana.

Hivi ndivyo Waislam wanavyofanya dunia nzima kila wanapofiwa na kipenzi chao.
Labda linaweza kuja swali jingine, ''kipenzi?''

Sheikh Ilunga kawaje kuwa kipenzi cha Waislam?

Naam Sheikh Ilunga Hassan Kapungu juu ya udogo wake wa umri alikuwa kipenzi cha Waislam na si Waislam wa Dar es Salaam peke yao.

Sheikh Ilunga alikuwa kipenzi cha Waislam wa Tanzania nzima.

Kibla cha kila msikiti wa Waislam katika Tanzania kilikuwa kinamkaribisha kama si kuwaidhi basi angalau asimame awasalimie nduguze Waislam.

Sheikh Ilunga alipendwa na umma hakuwa katika lile kundi la mesheikh wanaoogopa kuswali katika baadhi ya misikiti au hata kupita nje yake.

Sheikh Ilunga hakuwa katika lile kundi la masheikh wenyeji katika futari za serikali na''misikiti ya wakubwa'' lakini wageni katika misikiti ya ndugu zao Waislam maskini, Manzese au Tandale.

Kubwa Sheikh Ilunga hakukosa usingizi wala kujiona duni kwa kukosa kualikwa futari Ikulu au kualikwa katika dhifa za kitaifa akapigwa picha kavaa kanzu za kupendeza na katupia kashda za marembo kakaa na waheshimiwa na kutokea katika runinga na magazeti siku ya pili ukurasa wa mbele.

Sheikh Ilunga Hassan Kapungu hakushughulishwa na hayo.
Yeye alishughulishwa na kuliweka juu jina la Allah Subhana Wataala.

Hili ndilo lililokuwa likimshughulisha mpaka siku Allah alipomuhitimisha.
Kitabu hiki kinaeleza maisha yake mafupi hapa duniani.

Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani kwa bei ya Shs: 2,000.00 tu.
Inna lillahi wainna ilaih rajiuun.
 
Msanii,
Watu wengi wamekuja na taarifa hii na mimi nimeamua kuwa kimya kwa kutambua hisia kali ambazo zinaweza kusababishwa na mjadala huu.

Ikiwa utaweza kuweka clip yake na tukaisikiliza sote mimi nitasherehesha maneno yake.
Kuna clip yake niliiona naongea kwakweli hakuwa na maneno ya hekima. Alikuwa msambaza chuki wa wazi wazi.

Kama ndio role model kwako basi kuna upotofu ndani ya fikra zake eneo la uwepo wa imani zingine.
 
Back
Top Bottom