Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
RIWAYA: JASUSI KOMANDO
NA; BAHATI MWAMBA.
SIMU: 0758573660
1.
BERBERA, SOMALIA (Somaliland).
Alivuta pumzi zake kwa kasi kisha,alizishusha taratibu huku akiwa amefumba macho yake na kichwa chake akiwa amekiinamishia mbele kiasi, kidevu chake kiliegama kifuani mwake.
Zoezi lile alikuwa amesharirudia zaidi ya mara nne. Mara ya tano lilianza kuvuna matunda alioyatarajia. Alilegeza mwili wake, kisha alifumba macho na kubana pumzi. Masikio yake, yalibaki kusikia namna mapigo ya moyo, yalivyopishana kila baada ya sekunde moja.
Mikono yake iliofungwa nyuma ya kiti alichokalia, haikumpa hali ya maumivu tena, makovu yaliojiwekea makazi kwenye mwili wake,hayakuwa kitisho tena, hata joto kali liloletwa na taa iliofungwa sentimita chache kutoka kichwani kwake na kuwaka muda wote na, kumletea joto utosini kwake, hakusikia tena adha ile.
Mawazo yake yalisafiri hatua nyingi kutoka alipo. Mwili wake haukufanya kazi yoyote zaidi ya kuacha akili ipokee hatua nyingine ya mwanadamu; hatua ambayo, binadamu wengi hawaifikii na hawajui kama wanaouwezo wa kufika hatua hiyo.
Bwana huyu alikuwa anafanya tahajudi; tahajudi ya tiba. Aliona ni wakati muafaka kufanya tahajudi ya tiba, baadaa ya kupitia misukosuko kwa siku kadhaa, ambazo hakujua idadi yake. Hakuwa anajua usahihi wa siku alizopitia mateso na shuruba kubwa, shuruba za kupigwa na kugombaniwa na makundi ya wapiganaji ndani ya nchi ya Somalia yenye vinchi vingi ndani ya ardhi moja.
Alifanya tahajudi kwa kuwa alihisi kifuani mwake kumejaa rundo la vumbi, damu nayo haikutembea vyema mwilini mwake na, akili yake, ilikuwa nzito isioweza kufikiri vyema. Tahajudi ilikuwa ni tiba tosha katikati ya wanadamu wenye roho mbaya, wanadamu ambao hawajali machozi ya wenzao.
Licha ya kumtesa sana, lakini hakuna alieshauri apelekwe kwenye matibabu ili kumweka sawa kiafya, hivyo aliona ni vyema kufanya tahajudi ya tiba kisha atajua cha kufanya baada ya matokeo ya zoezi lake.
Akiwa bado ameyafumba macho yake, akili yake ilishirikiana na mlango mmoja wa fahamu, kisha aligundua kulikuwa na mtu karibu na chumba alichofungiwa.
Haraka aliamua kulisitisha zoezi lake. Alishusha pumzi nyingi kisha alifumbua macho yake na kufanya moyo wake udunde kwa shangwe ya kupunguziwa uzito kwa tahajudi.
Aliendelea kutulia na kumngojea mtu aliemsikia akitembea nje ya chumba alichokuwamo. Ngojeo lake lilimkutanisha na mtu aliemtegemea kuingia katika chumba kile kwa wakati kama huo.
Mtu yule alikuwa amebeba sinia la chakula, kiunoni mwake alikuwa na bastola asiopenda kuiacha mara zote aingiapo chumbani mle.
Mtu yule alimtizama kwa tuo kana kwamba ilikuwa ni siku ya kwanza kukutana.
“Leo umeletewa nyama ya kuku, hii si ishara nzuri kwako!” Alizungumza mtu yule, huku akiweka chini sinia lililosheheni nyama ya kuku na ugali mkubwa.
“Tunajua wewe ni mtanzania, na huitwi Rebu, bali unaitwa Obimbo Mtei” Alisema tena mtu yule, huku akishika kiuononi mwake kwa mikono yote miwili.
Obimbo Mtei aliekuwa amefungwa kitini, alimtizama bwana yule. Maneno yake yalimwingia vyema, lakini hakushituka. Alijua ni lazima watu wale wangelijua utambulisho wake sahihi licha ya kuukana mara kadhaa mbele yao.
“Sasa kwa nini unanambia haya?” Obi alimuuliza mtu yule.
“Kwa sababu nchi yako imekana kukujua hivyo kuendelea kukaa na wewe hapa, ni kujiletea hasara na hatari zisizo takiwa!”
“Lakini tangu mwanzo niliwambieni mimi si mtanzania, natokea Lilongwe Malawi na siko hapa kwa ujasusi, bali nafanya kazi na shirika lisilo la kiserikali.” Obi alimwambia mtu yule, huku macho yake yakikitizama chakula kilichokuwa kando ya miguu yake.
Njaa ilimuuma lakini alijizuia kuomba kufunguliwa ili ale chakula kile. Hisia zilimtuma vibaya juu ya chakula kile, hakujua ni kwanini lakini alisita kabisa kukifurahia. Akili yake ilikuwa inafanya kazi kubwa kuamua la kufanya juu ya chakula kile.
Alikitizama kwa tuo, aligundua kimepikwa kiswahili,kimepikwa na mpishi anaejua aina ya vyakula vya Tanzania. Alijua kuna kitu hakiko sawa juu ya matayarisho ya chakula kile na, alijua wanamtega ili kuujua utaifa wake ambao amekuwa akiukana tangu aingie mikononi mwa watu wale.
“Mimi bado ni lulu kwa hawa jamaa, hawawezi kuniua, wanataka hakika ya utaifa wangu….” Obi alijiwazia.
“Vipi rafiki, huhitaji kufunguliwa ili ule?” Aliuliza bwana yule alieleta chakula, ambae wakati wote alikuwa akimtizama Obi bila kusema kitu.
“Umekuwa ukifanya hivyo kila siku, fanya sasa ili nihudumie tumbo langu”
Baada ya kujibiwa, bwana yule alimfungua kamba za mikono, kisha aliondoka ndani ya chumba kile.
Obimbo Mtei alikiinamia chakula kile na alipotaka kumega alisita, alilegeza mwili wake kisha alitulia. Alihisi kuna mtu anamtizama, haraka aligeuka na kukutanisha macho na mtu aliekileta chakula. Mtu yule alikuwa amesimama mlangoni na ameelekeza macho yake kwa Obi.
“huu ni mtego!!” Obi alijiwazia kisha alianza kuumega ugali na, aliumega tofauti na matarajio ya mtu aliekuwa akimtizama.
Obi aligundua mtego wake upo kwenye umegaji wa ugali; kawaida waswahili wengi hawamegi ugali kuanzia juu, humega ugali chini kabisa kiupande. Lakini mataifa mengi ya Afrika, watu humega ugali vile watakavyo. Obi alitegua mtego ule kirahisi sana na nyuma yake alisikia mlango ukifungwa.
Obi alikula harakaharaka, kuna kitu alitaka kukifanya kabla ya muda wa kufungwa haujawadia; muda ambao ni dakika saba tu baada ya kupewa chakula.
Kwa makadirio yake alikuwa ametumia dakika tatu kumaliza chakula, alisimama haraka na kukichukua kijiko kilichokuwa chini ya kiti alichokuwa akifungiwa. Alinyata kwa kutumia ncha za vidole vyake. Alifika mlangoni na kukitazama kitasa cha mlango, kitasa ambacho vishikio vyake(bolt), vilizingwa na kutu kiasi. Obi alilichukulia lile ni kosa la watu waliomteka, pengine walijua na kupuuzia au hawakujua kabisa.
Obi alitumia kijiko kulegeza vishikio vile na, ndani ya dakika tatu, alikuwa amelegeza nati tatu na kubakiza moja ambayo alikuwa ameshailegeza tangu alipogondua udhaifu wa mlango ule.
****
Mleta chakula alirejea akiwa ameongozana na mtu mwingine aliekuwa na bunduki ya kivita aina ya AK 47. Watu hawa ilikuwa ni kawaida yao kushirikiana kumfunga kwenye kiti na kumwacha pale kila siku. Lakini kitu kimoja hawakujua, ni mipango ya Obi juu yao. Obi hakutaka kulala tena ndani ya kambi ile ya wanamgambo wa Hizbul Islam.
Walipomaliza kumfunga na kutoka, Obi alirudia zoezi lake la tahajudi, lakini wakati huu hakufanya tahajudi ya afya, alifanya tahajudi ya hisia na nguvu za ziada. Alifumba macho na kutulia tuli.
Tahajudi ilimletea matokeo alioyatarajia, alisikia maji yakimwagika sehemu na aligundua ni mkondo wa maji umepita chini ya nyumba ile aliohifdhiwa.
Alifumbua macho yake na kushusha pumzi nyingi. Aligundua eneo alilofungwa.
Kulingana na ramani ya nchi ya Somalia, ni mji mmoja tu ulio na miundombinu ya mikondo ya kumwaga maji machafu baharini na mji huo ni Berbera, kaskazini mwa Mogadishu na kusini mwa guba ya Aden.
Obi aliguna kisha alijiangusha chini na kiti chake na kutulia. Hakutgemea kuwaona walinzi wakiingia ndani ya chumba kile, kwa sababu alishafanya mazoezi ya sauti ya kishindo na kugundua ni sauti kiasi gani inaweza kuwakurupua na kuja ndani ya chumba kile.
Zoezi hilo alilifanya kwa kupiga komeo la mlango na kijiko kila alipoletewa chakula, hivyo alipojiangusha chini, alikadiria kishindo ambacho kisingeweza kuwagutua walinzi waliokuwa kando ya mlango.
Obi alipodondoka chini, alifanya jitahada na kukifikia kijiko kwa kujiburuza na kiti chake, kisha alianza kuzikata kamba kwa kutumia kijiko.
Ilimchukua dakika thelathini kufanikiwa kuzikata kamba. Hatimae mikono yake ikawa huru na alijifungua kamba za miguuni mwake na kusimama wima.
Aliifuata taa iliokuwa inawaka,aliinyofoa na kufanya giza libebe nafasi ndani ya chumba kile.
Hakuwa na viatu miguuni mwake, hiyo ilikuwa ni faida kwake kwa kuwa aliweza kutembea ndani ya chumba bila hatua zake kusikiwa na mtu aliekuwa karibu na chumba.
Heka heka alizozoea kuzisikia, taratibu zilianza kupungua na hiyo ilikuwa ni ishara nzuri kwake, maana alijua huo ni usiku na watu wengi kwenye nyumba ile hupumzika na kuwaacha walinzi watatu wakilinda chumba alichokuwemo na, walinzi wale hulala fofofo katikati ya usiku mkubwa na alijua ni sauti kiasi gani ingesikiwa na walinzi wale katikati ya usingizi wao, hivyo alijua atumie sauti gani ili asiwaamshe wakati wa kutoroka.
****
Hatimae muda ambao aliutarajia ulifika. Tayari alikuwa amefanikiwa kuhamisha mfumo wa kitasa na mlango ulikubali kufunguka.
Aliuvuta taratibu bila kelele, kisha alinyata na kutoka nje ya chumba na kujikuta kwenye korido pana na kando ya mlango kulikuwa na walinzi watatu wakiwa wamelala kwenye viti na silaha zao.
Aliwatizma kwa haraka haraka na kumuona mmoja akiwa amening’iza rundo la funguo kwenye suruali njiwa aliovaa.
Obi alinyata na kumfikia, kisha alianza kumpuliza shingoni na upepo wa mahaba. Hii ilikuwa ni mbinu ya kiueledi wanayofundishwa makomando wawapo mazoezini na huaminika upepo shingoni humzidishia mtu kilele cha usingizi na kumfanya mzito kuamka.
Obi alichomoa funguo na kuanza kuanza kutoka kwenye ile korido na kuafuata upande ambao aliamini hakukosekani jiko. Alihitaji kutoroka kwa kutumia upande wa jiko, ambako aliamini kuna chemba ya kumpitisha kwenye mkondo wa maji machafu.
Nyumba nyingi za Berbera zimejengwa kwa mfumo huo na ni kwa sababu ni mji uliokaliwa na waingereza na kuugeuza eneo la kijeshi.
Obi alitaka atoroke bila tafrani, maana hakuwa na nguvu za kutosha na mwili wake ulikuwa dhaifu, kashikashi yoyote asingeweza kukabiliana nayo
NB: RIWAYA HII NI KITABU NA KINATOKA RASMI, KATIKATI YA MWEZI WA 11 MWAKA HUU.
BEI YAKE NI TSH 10,000/=
KITABU HIKI SI CHA KUKIKOSA KWENYE MAKTABA YAKO....
WEKA ODA YAKO SASA KWA KUWASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA; 0758573660.
KUMBUKA: KITABU HIKI KINATOKA KWA ODA MAALUMU, HIVYO ODA YAKO ITAKUKUTANISHA NA KITABU HIKI MAPEMA KABISA.
KARIBU.