Kitabu cha Mwanzo katika Bible ndio msingi wa mambo matatu duniani! Intelijensia, Sayansi na Uchawi

Baada ya unabii kutimia... Kitabu cha ufunuo kila haya majibu labda hili linahitaji post kamili kuhusu kiama/kiyama na kile kilichomo kwenye kitabu cha ufunuo
Ina maana unabii haujatimia au umeshatimia ila kilicho baki ni muda tu ?
 
Replies zako 3 tofauti tayari zimekutambulisha kiwango chako cha ufahamu... Hupaswi kulaumiwa wala kukasirikiwa bali kuelekezwa kwa upole na kujulishwa kwamba huku ni intelligence na sio jukwaa la siasa kwenye matusi dhihaka na vijembe... Huku hoja inajibiwa kwa hoja
hakuna Hoja ulichpfanya ni kumpamba bibi harusi Kwasababu ya mahaba
 
njoo na nyuzi fikirishi
Inawezekana kabisa wewe ni mgeni hapa ama ni mkongwe lakini kwa ID mpya..... Lakini iko hivi si kila wakati lazima tuandike vitu complicated... Vingine huwa viko wazi japo kuna tafsiri kubwa sana nyuma yake kama ukisoma kwa kutulia... Lakini pia kumbuka si kila siku utavaa nguo zilezile au kula chakula kilekile

Nilichoandika hapa kuhusu kitabu cha mwanzo kinaweza kuwa ndio msingi wa mada nyingi za intelligence... Lakini nimeandika kwa lugha rahisi na ya moja kwa moja
 
Ina maana unabii haujatimia au umeshatimia ila kilicho baki ni muda tu ?
Kuna tofauti ya tafsiri ya muda uliomaanishwa kwenye bible na muda muda tunaoufahamu
Neno la Mungu linasema hivi... Siku moja kwake ni sawa na siku elfu moja kwako na siku elfu moja kwako inaweza kuwa sawa na siku elfu moja kwake...
 
Hii kaka sio kwa masiku ya duniani,nini namanisha hapa. Swali langu linazungumzia siku ya kiyama kwa maana kitakapo tikea.

Kuhusu siku moja kwake sawa na masiku elfu kwetu katika yale masiku ya uumbaji.

Na Allah ndie anaejua zaidi.

Swali langu linaulizia ile siku ya uduniani ambacho kiyama kitatokea,je Biblia inasema kitatokea lini ?
 
Kitatokea baada ya yale yaliyotabiriwa katika unabii kupitia kitabu cha ufunuo kutimia... Je ni unabii gani huo? Je kiama bado ni valid? Kwakuwa kuna mahali Mungu anasema haitateketeza tena dunia kwa moto wala kwa maji... Refer Gharika ya nyakati za Nuhu na moto enzi za Sodoma na Gomora...
 
.
 
Hadi pale atakaporudi Masihi Mwana wa Mariamu, kuja kuuhukumu ulimwengu kwa yale uliyotenda hapa duniani.

Zaidi Soma kijana usitake kutafuniwa kila kitu, hii ni Jamii Intelligence.

Ya Radhiiina Amanu, Iqraa Bismi Rabik.
Kaka ni makosa kuandika aya kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu sababu unakosea na unabadilisha maana. Kuwa makini mzee. Hapa utaona sasa kati yangu mimi na wewe nani anatakiwa asome sana ?
 
Jina huathiri muktadha, asili, chanzo na uhalisia wa kitu..... Kitabu cha MWANZO katika Biblia takatifu ndicho kitabu msingi kinachosomwa zaidi duniani... Tena na imani na dini zote...
Nukuu na rejea nyingi kwenye malumbano mijadala, tafiti za kisayansi, tafiti za kilozi na kishirikina, ulimwengu wa nguvu ya 'supernatunal powers (nguvu zisizomithilika) na hata maandiko mbalimbali yahusuyo asili na chanzo cha ulimwengu... Huwezi kuacha kutaja kitabu hiki....
Masomo ya sayansi, fizikia, baiolojia, historia, kemia historia, filosofia uchawi na ulozi.. Yote haya katika ujumla wake unayapata katika kitabu hiki cha MWANZO....
Unaposoma... MUNGU AKATAMKA NA IKAWA... hii ni aina ya ushirikina, imani katika nguvu za asili na uwezo wa kuumba na kuunda kwa matamshi tu... Sayansi iwayo yote haina uwezo huu... Mambo hayo kwasasa ni ya manabii mitume na wachawi(wanga na washirikina)
Mungu anapotamka kuwa kaumba viumbe vyote... VINAVYOONEKANA NA VISIVYOONEKANA... mpaka leo hii sayansi imeshindwa kutoa jibu sahihi juu ya hivyo VISIVYOONEKANA!
Hapa ndipo inabidi turudi kwenye rejea ya kitabu cha MWANZO na kuona nini kilisemwa na kikawa halafu kikawaje! Na ndipo tunapata ufunuo wa ajabu na ugunduzi kwamba hii tunayoita SAYANSI YA ITHIBATI si chochote bali ni njia tu ya mwanadamu kujaribu kutafsiri kwa njia yake kile ambacho kilishaandikwa na kufanyika kwenye kitabu cha MWANZO
Hakuna kipya chini ya anga na kwa hakika bado hatujaweza kuvumbua kila kilichomo na kilichoandikwa kwenye zile kurasa chache za kitabu cha MWANZO
World encyclopedia, volumes kwa volumes za sutras, misahafu kwa misahafu, maandiko na mavitabu makubwa ya wanafilosofia maarufu kuwahi kutokea duniani... SUMMARY yao iko kwenye kitabu cha MWANZO

Kuna wenzetu wenye mawazo mbadala kuhusu Bible na kitabu cha mwanzo.. Ukiwa mwepezi wa tafakuri wanaweza kwa HAKIKA kabisa kukuteka na hoja zao mahiri kabisa lakini zisizo na hakika.. Ni wajenzi wazuri wa hoja zinazoteteresha kama wewe ni legelege lakini ukitulia na kutafakari hawana mwendelezo na hawaendi zaidi ya kilipokomea kitabu cha mwanzo...
Wataandika na kuchagiza kwa maneno mengi na misamiati huku wakiweka nukuu za wengine ambazo nazo zinaishia kwenye kuakisi kile kilichomo kwenye kitabu hicho cha mwanzo....
Tukirudi hapa JF hata jukwaa hili la intelligence kwa sehemu kubwa linatawaliwa na maandiko toka kitabu cha mwanzo...
Ni kwa Muktadha huu kitabu hiki cha MWANZO kinabaki kuwa chanzo kikuu, msingi, chimbuko na asili ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku... Iwe sayansi uchawi imani ama intelijensia....!!!
Kazi ya ufagio kwa mtumiaji ni kufagia mengine anayejua ni designer, biblia ina mengi mkuu na information za uhakika zipo kwenye original Bible tofauti na hizi tunazotumia zilizotafsiriwa na watu.
 
Kaka ni makosa kuandika aya kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu sababu unakosea na unabadilisha maana. Kuwa makini mzee. Hapa utaona sasa kati yangu mimi na wewe nani anatakiwa asome sana ?
Umejuaje kama hiyo ni Aya ?

Kwani hiyo Aya yako inabidi iandikwe kwa Lugha gani ?

Na ni Aya ya nini ?

Umejuaje kuwa hicho ni Kiarabu wakati mimi sijakuambia chochote ?

Hebu nipe Darsa nijue
Natabasamu kwa fulaha
 
Natambua wazi huwezi kujibu zaidi ya hiki ulichojibu
nilikuwa nakuangalia uwezo wako wa kupambanua mambo sasa kwa vile umeonya ujuaji twende sawa
BAADA ya Yusufu kufika misri na kutupwa gerezani mpaka walipokuja wale maakida wawili waliowekwa lindo gerezani baada ya kumghadhibisha farao .Yusufu alitafsiri ndoto zao kisha kuna maneno aliongea kwamba amefika pale kwasababu ya kuibiwa SASA basi kuna hii kauli aliongea ndipo kwenye swali langu

MWANZO 40:15
;"kwa sababu hakika naliibiwa kutoka NCHI YA WAEBRANIA ,wala hapa sikutenda neno lolote hata wanitie gerezani;"
Swali langu ni kweli yusufu alitoka nchi ya waebrania ?
 
Umejuaje kama hiyo ni Aya ?

Kwani hiyo Aya yako inabidi iandikwe kwa Lugha gani ?

Na ni Aya ya nini ?

Umejuaje kuwa hicho ni Kiarabu wakati mimi sijakuambia chochote ?

Hebu nipe Darsa nijue
Natabasamu kwa fulaha
Kwenye kitabu cha mwanzo unaweza kuniambia kati wanyama na binadamu nani alianza kuumbwa?
 
Back
Top Bottom