Kama kina tija mbona hakijamsidia yeye.
wewe unailinganisha Libya na Tanzania, katika nyanja ya kiuchumi na kielimu?- Libya ina asset Katika nchi kibao Africa sisi tuna nini?, West walifreeze zaidi ya dola billion 130 za libya, hizo pesa zilipatikana na kutunzwa vizuri chini ya uongozi wa nani?
Sattelite ya kwanza ya Africa ya mawasiliano ni nani alitoa dola million 300?
Unaijua the great manmade river, mto ambao maji yake yametolewa chini ya jangwa la sahara na kuwa supplied katika miji ya Libya, dola billion 33 zilitumika katika hiyo project, ni kiongozi gani alipreside katika hiyo project?
kila mwezi kila mlibya anawekewa katika account yake dollar 500, ni lini bongo tutafikia hali hiyo?
Elimu bure mpaka University, sisi bongo hata hiyo form four ni ndoto!
Mlibya akitaka kwenda abroad kusoma serikali inafinance, bongo unaielezeaje?.
Unaujua mchango wa Ghadafi katika kupambana na Apartheid kule south Africa, jiulize ni kitu kilimfnaya Mandela kufunga safari kwenda Libya kumshukuru Ghadafi licha ya vikwazo vya anga west walivyokuwa wameiwekea libya.
Unaulezeaje mchango wa Libya kussurport vikundi vilivyokuwa vinapambana na France installed puppet regimes throughout Africa?
Kuhusu kumsurport Iddi-Amin, anyway ile vita kwanza ni contraversial kuna vitu vingi sisi bado hatuvielewi, Sisi bongo tumewahi kumsurport Savimbi at one time, naamini nayo ilikuwa ni mistake pia. Lakini Mwalimu Nyerere alikuwa rafiki wa Ghadafi na aliendelea kuwasiliana naye hata baada ya kug'atuka (hata msikiti wa Mwalimu uliojengwa butiama, fedha ilitoka kwa Ghadafi).
Gadafi alikuwa ametenga dola billion 30 ili zitumike kuunda Africa Monetary Fund , lakini hizo pesa zikawa freezed na serikali ya Obama, mwezi March, unaweza kuona ni kwa namna gani huyu bwana alikuwa na vision ya Africa.
Ghadafi ni mwanamapinduzi wa Ukweli, hawa waasi wa Bengazi si wanamapinduzi chochote, ni vibaraka tu wa West, na soon watajuta kwa kuwakalibisha wakoloni katika nchi yao!