Kitabu Cha Dr.Slaa: Sura Ya 23: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitabu Cha Dr.Slaa: Sura Ya 23:

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Big Lady, Sep 11, 2010.

 1. Big Lady

  Big Lady JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dr. Slaa 23:

  1 Kisha Dr. Slaa akauambia umati wa Watanzania pamoja na wafuasi wake wa CHADEMA pale Jangwani,

  2 "CCM na Mafisadi wana mamlaka ya kufafanua Sheria za Watawala na Ilani zao za Uchaguzi na kutoa Ahadi kem kem.

  3 Kwa hiyo wasikilizeni na kupima chochote watakachowaambieni. Lakini msiwape kura zenu wala msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyawahutubia.

  4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika Watanzania mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.

  5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa nguo nzuri za gharama, kutembea na magari mazuri ya gharama na kuishi katika nyumba nzuri za gharama zenye hati za majina yao, au watoto wao au ndugu zao.
  6 Hupenda nafasi za heshima bungeni na katika karamu au hafla mbalimbali hupenda viti vya meza kuu ili waonekane.

  7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima bungeni, maofisini au hata barabarani, sokoni, kwenye sherehe au misibani na kupendelea kuitwa na watu: Mheshimiwa.

  8 Lakini ninyi msikubali kuitwa kamwe Mheshimiwa maana Nchi yenu ni mmoja tu na wala haijawagawa wa kuheshimiwa sana wala kidogo, nanyi nyote ni Watanzania mlio na haki sawa za Kibinadamu.

  9 Wala msimwite Fisadi yeyote hapa duniani Mheshimiwa au Mtukufu, maana Mtukufu ni mmoja tu Mungu aliye mbinguni.

  10 Wala msiitane Mheshimiwa bali Wapiganaji maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Dr. Slaa.

  11 Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.

  12 Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.

  13 "Ole wenu walimu wa Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Maendeleo ya Kweli mbele ya macho ya Watanzania. Ninyi wenyewe hamwendelei kwa amani, wala hamwaruhusu Watanzania wanaotaka kuendelea wafanye hivyo.

  14 Ole wenu CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnawanyonya Watanzania na kujisingizia kuwa watu wema kwa kuwapa misaada ya danganya toto. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali na kunyimwa Kura.

  15 "Ole wenu CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnasafiri Angani, baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate Ilani Yenu ya Uchaguzi na Kuwapa Kura. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika Mateso makali wakati ninyi wenyewe mkiponda raha kama mko peponi.

  16 "Ole wenu viongozi vipofu wa CCM! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kuwa Raia kama Bashe ama Ulimwengu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa kutoa fedha na dhahabu na kukubali kuwa Fisadi, kiapo hicho kinamshika.

  17 Enyi vipofu wapumbavu wa CCM! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu, pesa au Kuwatumikia Watanzania kitakachofanya hiyo fedha na dhahabu kuwa ya Maana?

  18 Tena mwasema ati hata akiwa na Dhahabu lakini Viongozi wake hamjampenda basi si kitu hata kama hana matatizo na hata kama Wananchi walimpitisha katika Kura za Maoni; lakini akiapa kuwa mnyenyekevu, kuwalamba miguu na kuwatumikia matakwa yenu, basi huyo mtu huonekana wa Maana hata kama si Raia kama ilivyokuwa kwa Mustafa Mkulo.

  19 Enyi vipofu wa CCM! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, fedha au Uongozi wenu kwa Umma ambao hufanya hizo, zawadi na fedha kuwa za maaana?

  20 Anayeapa kuwa Kiongozi wa Umma ameapa kuwa Mtumishi, na Kuwatumikia watu huku akipiga vita Ufisadi wote kwa Uadilifu wa juu.

  21 Na anayeapa kwa Chama cha Mafisadi ameapa kwa hilo Mafisadi na pia kwa kulinda maslahi ya Mafisadi Wakuu.

  22 Na anayeapa kwa Watanzania na kwa Mungu kuwa muadilifu huyo astahili kupewa Kura.

  23 Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnatoza watu kodi mbalimbali, hata juu kwa masikini lakini punde mkikusanya pesa mnaacha mambo muhimu ya yaliyo katika Ilani zenuya Kuleta maendeleo ya Kweli na kuwanyima watue haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.

  24 Viongozi vipofu wa CCM! Mnatoa inzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!

  25 "Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo wa Watanzania Masikini.

  26 Wana CCM na Mafisadi Vipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.

  27 "Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.

  28 Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

  29 "Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnajenga makaburi ya Viongizi Waadilifu na kuyapamba makaburi ya watu wema.

  30 Mwasema: Kidumu Chama Cha Mapinduzi! CCM Nambari Wani! JK Apewe Kura Za Ndiyo!

  31 Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua Viongozi Waadilifu kama: Nyerere, Karume, Sokoine, Kolimba, Malima, Kombe, Mwaikambo na wengineo

  32 Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu wanafiki waliyoianza!

  33 Enyi CCM na mafisadi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?

  34 Ndiyo maana mimi mmeletewa Mshindani Dr. Slaa na Wapoiganaji wa CHADEMA, watu wenye hekima na Viongozi Makini; lakini mnawapaka matope na kuwachafua baadhi yao, na wengine mnawakatia Rufaa Tume ya Uchaguzi yenu na kuwasakama katika kila mji kwa kila aina ya uzandiki mkiacha kuelezea Sera zenu na kujibu Tuhuma zinazowakabili.

  35 Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi na matope mnayowapaka Wapiganaji wa CHADEMA. Naam, tangu kuuawa kwa Sokoine ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Horice, mwana wa Kolimba, ambaye mlimuua Katika Vikao Vyenu mbele ya wajumbe.
  36 Nawaambieni kweli CCM na Mafisadi, kizazi hiki chenu kitapata adhabu na kunyimwa Kura kwa sababu ya mambo haya.

  37 "CCM, Ee CCM! Unawaua Viongozi Waadilifu na Kuwachafua Viongozi Wazalendo wenye Uchungu na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako kama Seleli, Mpendazoe na wengine. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya Viongozi Wazuri na Watanzania kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.

  38 Haya basi, nyumba yako Dodoma na Lumumba itaachwa magofu!

  39 Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati Nitakapoingia Ikulu pale Magogoni
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Ama kweli kanisa limesimama mwaka huu
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  What a creativity? We miss this kind of positive creativity in the CCM! During Kambarage, we used to have it. Remember this:

  Tuambie ni nani? Yuko wapi? na anafanya nini katika kuhujumu uchumi nchi; nasi tutamrusha hewani" (MIKINGAMO).
   
 4. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Ni nzuri,ila tujaribu kujua tofauti kati ya heshima kwa injili na upupu wa siasa
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ======

  seconded with applause
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Big Lady umetumwa n shetani, kejeli zako zitakwisha tu!!!
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  4. Hufunga mizigo mizito na kuwatwika Watanzania mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.

  Mkuu wetu hapa anaona kugusisha sarawali yake kwenye udongo ni ufedhuli!...anatumia mkeka kupanda mti...Haya ni mambo ya kwenye sayari MPYA ya Kleptomaniacs!..huh!...utapanda ekari ngapi kwa utoto huo?
  [​IMG]
   
 8. P

  Paul S.S Verified User

  #8
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wakati mwingine tuangalie mambo ya kupost, hivi ulitakaje hapo ajipakae matopo mwili mzima ndio ujue anafaa,
   
 9. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ajipake matope ndiyo! Tafuta uone picha za Mwalimu Nyerere alivokuwa akifanya kazi. Alikuwa haangalii unadhifu wa mavazi. Alikuwa yuko radhi kuchafuka, lakini alionesha mfano kwa watu. Sasa hii ya huyu bwana ni nini? Si kutudhalilisha sisi tunaofanya kazi za mikono? Si angeacha tu badala ya kufanya haya maigizo yasiyo na maana? Ni mfano gani anautoa kwa watu: kwa kupanda mti akiwa juu ya mkeka, akiogopa kuchafuka kwa udongo?
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Inanikumbusha kuna kipindi cha Nyerere kuna kipindi alikaa chini anatolewa miiba baada ya kulima kwa kitambo kama raisi
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Sure!
  Why hypocricy bana!...ukitaka kuonyesha mfano wa kazi onyesha kikweli sio kufanya maigizo ya waMexico akina MaryMar!
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tatizo dunia inakwenda mbele ninyi mnamawazo ya kizamani bado, unampima mtu kwa upuuzi huu, eti nyerere alifanya kwahiyo kila alichofanya nyerere ndio nini, muongozo wetu
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu kama alijua atakwenda panda miti utakwendaje kavaa suti asitake kuchua suti yake.
  Hii picha ina maelezo mengi zaidi ya unavyofikiria..
   
 14. coby

  coby JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe kweli ni kenge, Nyerere alikua hachafuki?? Unadhani umaskini wako wa kutonunua sabuni JK anaujua??
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Sep 11, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Watu mbona mnapenda sana kulinganisha?

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  wengine humu jf walishalogwa na majini ya sheikh yahye na kikwete wake, ni kumtetea tu hata akiwa muozo
   
 17. D

  Dopas JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda hiyo. Ubunifu huo unafaa. Ni aina ya viongozi wanaotakiwa nchi hii: wanaokuwa wabunifu na kuwashirikisha wananchi wanachofikiria ili kuwe na maendeleo ya kweli kwa nchi yetu.

  Ombi langu ujitajihi wakati huu wa maandalizi ya uchaguzi kuwaelimisha watu 50 ili wakishaelewa ulichozungumzia wawachague viongozi watakaofaa kwa maendeleo ya nchi yetu.

  Mimi tayari nina 42. Nitajitajidi nifikie watu mara mbili ya hiyo na zaidi. Ni kuwaelimisha kwa faida ya nchi yetu. Asante ndugu Big Lady.
   
 18. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Hii imetulia sana. Ukweli mtupu!
   
Loading...