Kitaalam, alichomaanisha Polepole ni hiki

torosi

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2020
Posts
1,114
Reaction score
2,088
TZ

Mifumo hii imeunganishwa vipi, kupitia kadi yako ya NIDA, walichokifanya ni kuongeza idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura kabla ya kutoa idadi ya waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura ( ndio sababu ilikua kubwa )

Kwa maana ya kwamba kama hukujiandikisha kupiga kura possibility ya wewe kuwa katika daftari la kupigia kura ni kubwa kwa sababu tu tayari taarifa zako za NIDA walikua nazo.

Wengi ambao hawana kadi ya kupiga kura ( wengi wakiwa vijana ) , hawakuhangaika hata kwenda kujihakiki katika daftari la mpiga kura sababu wanajua hawapo, hapo ndio uhaini ulipofanyika, baada ya mlango wa kuhakiki kufungwa na kabla ya kutangazwa, daftari likaongezwa taarifa kutoka NIDA ( Ambapo kuna taarifa zako zote, picha yako na fingerprint yako ). Kwa mifumo ya IT hii ni process isiyochukua hata dakika 3 kuongeza hata zaidi ya 10M voters.

Sasa siku ya kupiga kura, sababu unaamini huna vigezo, hautatokea kituoni, ila wakija kuhesabu baadae ( baada ya kuongeza box za kura feki ambazo zitakua na kura zenye taarifa halali kutoka NEC ) utajikuta upo katika orodha ya watu waliopiga kura

Ni nini tume ya uchaguzi ifanye kutuhakikishia kuwa kama sikujiandikisha basi taarifa zangu hazipo NEC, waweke portal ambayo mtanzania yoyote anaweza ingiza NIDA ( sio namba ya mpiga kura ) yake kuangalia kama yuko katika daftari la mpiga kura. Na hii portal iwe wazi mda wote ( kabla na baada ya uchaguzi )

Nyongeza
Tukumbuke pia CCM wana access sio tu na mfumo wa NIDA, bali hata RITA, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa wapiga kura wakawa ndugu zetu waliokwisha tangulia mbele ya haki, as long as alishawahi jiandikisha na daftari la mpiga kura.

Kitaalamu ni kuwa ukifanya uchunguzi sasa hivi hakuna kitu utaona sababu tayari kuna record zisizo halali zilishawekwa tayari. Suluhisho pekee, mchakato wa uhakiki na uandikishaji wa daftari la wapiga kura uanze upya na uwekwe wazi mda wote mtu akitaka kuhakiki taarifa zake kupitia NIDA zionekane, kuwe na portal ambayo mda wote inaonyesha idadi kamili ya wapiga kura, verification ifanyike direct kutokea katika DB ya NEC, na ikitokea mtu amefariki taarifa yake itoke NEC in real-time baada ya kufika RITA.

Haya ni mambo yanayowezekana ni kwamba wanajitoa ufaham tu.
 
Bila kusahau Sensa, hiyo milioni 37 ni copy na paste toka mfumo wa sensa.
 
TZ

Mifumo hii imeunganishwa vipi, kupitia kadi yako ya NIDA, walichokifanya ni kuongeza idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura kabla ya kutoa idadi ya waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura ( ndio sababu ilikua kubwa )

Kwa maana ya kwamba kama hukujiandikisha kupiga kura possibility ya wewe kuwa katika daftari la kupigia kura ni kubwa kwa sababu tu tayari taarifa zako za NIDA walikua nazo.

Wengi ambao hawana kadi ya kupiga kura ( wengi wakiwa vijana ) , hawakuhangaika hata kwenda kujihakiki katika daftari la mpiga kura sababu wanajua hawapo, hapo ndio uhaini ulipofanyika, baada ya mlango wa kuhakiki kufungwa na kabla ya kutangazwa, daftari likaongezwa taarifa kutoka NIDA ( Ambapo kuna taarifa zako zote, picha yako na fingerprint yako ). Kwa mifumo ya IT hii ni process isiyochukua hata dakika 3 kuongeza hata zaidi ya 10M voters.

Sasa siku ya kupiga kura, sababu unaamini huna vigezo, hautatokea kituoni, ila wakija kuhesabu baadae ( baada ya kuongeza box za kura feki ambazo zitakua na kura zenye taarifa halali kutoka NEC ) utajikuta upo katika orodha ya watu waliopiga kura

Ni nini tume ya uchaguzi ifanye kutuhakikishia kuwa kama sikujiandikisha basi taarifa zangu hazipo NEC, waweke portal ambayo mtanzania yoyote anaweza ingiza NIDA ( sio namba ya mpiga kura ) yake kuangalia kama yuko katika daftari la mpiga kura. Na hii portal iwe wazi mda wote ( kabla na baada ya uchaguzi )

Nyongeza
Tukumbuke pia CCM wana access sio tu na mfumo wa NIDA, bali hata RITA, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa wapiga kura wakawa ndugu zetu waliokwisha tangulia mbele ya haki, as long as alishawahi jiandikisha na daftari la mpiga kura.
Hilo la Rita ndo balaaa. Lawama zilishatokea marehemu wamepiga kura uchaguz serikali za mitaa
 
Back
Top Bottom