Kitaa ni kigumu. Shekeli imetoweka

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Kwa kawaida hii ndio miezi ya pesa.. Ni miezi ya pesa kwakuwa bajeti inakuwa imeshatoka na pesa ishatembea mitaani.. Wakandarasi wameshalipwa hivyo maokoto ni ya kutosha sana kitaa.

Kipindi kama hiki watu huwa hawana shida ndogo ndogo.. Ile kuombana pesa ya kuzungusha fasta na kurejesha wala sio ishu kivile.

This time around mambo ni tofauti sana si kwa waajiriwa, si kwa waajiri si kwa wajisiriamali wala si kwa wazee wa fursa! Huko vilingeni waganga sasa wanapokea hata broiler huwezi kuamini.. Na sometimes wanaagiza hata perege mbichi! Just imagine mganga wa kienyeji anaagiza perege.

Wafanyakazi wanaodhaniwa wana nafuu nao ni vilio
Wakopeshaji hata wale wa mikopo ya kausha damu kote ni vilio tupu... Hata wale wa nani kama mama sauti zao hazina stereo tena.. Hata mitandaoni wanaingia kwa kuibia na bando za mkopo

Inasemwa/inasemekana kibubu cha kaya kiko empty zero kabisa.. Halafu madeni ya wahisani ndio usiseme wanafyonza mpaka ndururu.

Kulazimika kusaini lile zimwi kimagumashi sana ni kwa ajili ya kugewa maokoto

Just imagine miaka 60 ya uhuru bado tunahemea Pengine ni uhuru wa manyani..
Hivi kweli mimi ni wa kunywa ngumu kumeza kwa mama bonge? Yaani hata kisungura kimenishinda?

kuna jirani yangu hapa na kitambi chake kikubwa na tai kaagiza kisungura ila kasema kimiminwe chote kwenye birauli ya kioo

Sijui wenzangu nyie huko mliko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii post imenipa Kili mbili kumbe kuna mdau yuko hapa na wakati napost aliniona
20231025_194825.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kawaida hii ndio miezi ya pesa.. Ni miezi ya pesa kwakuwa bajeti inakuwa imeshatoka na pesa ishatembea mitaani.. Wakandarasi wameshalipwa hivyo maokoto ni ya kutosha sana kitaa....
😁😁🙌 Kunywa dabo kiki kweli hizi tarehe ndo tarehe za maokoto ila nashangaa ebu tusubiri Pesa za lidubwana labda zitatutoa huku kwnye wanzuki

Uhuru wa manyani na mganga kupokea kabejiQmmk noma Sana😁😁😁
 
Back
Top Bottom