Salaam wakuu,
Japo tayari nimeshafanya kosa la lugha kwa kushindwa kutohoa neno chat lakini mathalani dhumuni kuu la uzi huu ni tuweze kufanya mazungumzo hapa kwa kutumia kiswahili fasaha aghalabu bila kutumia lugha yoyote ya kigeni wala kuchanganya maneno na kuandika kwa vifupisho. Nawasabahi wana JF wote. Kiswahili ni lugha tamu sana, juzi nilikua naperuzi kwenye wavuti mbali mbali nikiangalia jinsi raia wa kigeni wanavyojifunza lugha hii kwa kasi. Ama kwa hakika kiswahili kinakua na tukiamua wenyewe kwa juhudi zetu za dhati basi nafikiri lugha yetu itafika mbali zaidi.