Kiswahili si Lugha ya wasomi

Aloysius

Member
Mar 1, 2011
80
9
Jamani enendeni mahakani, mjichekeshe kwa vituko vya huko. Unakuta Hakimu anafurukuta kuandika kwa kutafsiri kwa haraka maneno anayoyatoa shuhuda au hivo kizimbani, haraka haraka kwa kiingereza...!!! Yaani maneno yanazungumzwa kwa kiswahili lakini analazimika kuandika kwa kiingereza. Mbali ya hiyo, pia katika hukumu yake atageuza yote ya kiswahili yawe kwa kiingereza na hivo. SIKU YA HUKUMU: Yale yaliyoandikwa kwa kiingereza tena yanasomwa kwa kiswahili, wali maharage wali maharage hivyo hivyo. MASKINI WAHUSIKA: Wanatafuta mtafsri. MTAFSIRI: akiwa sio mwanasheria istlahi za sheria zikimpiga mweleka atatafuta wakili. WAKILI: atataka pesa. PESA: haiwapendi maskini
HATIMA: haki haitendeki.
KISWAHILI SIO LUGHA YA WASOMI?!!!
 
Ukisoma kiswahili ndo utajua kama ni lugha ya wasomi au la!Lakini ninavyojua kuna wasomi wengi wanajua kiswahili.
Jamani enendeni mahakani, mjichekeshe kwa vituko vya huko. Unakuta Hakimu anafurukuta kuandika kwa kutafsiri kwa haraka maneno anayoyatoa shuhuda au hivo kizimbani, haraka haraka kwa kiingereza...!!! Yaani maneno yanazungumzwa kwa kiswahili lakini analazimika kuandika kwa kiingereza. Mbali ya hiyo, pia katika hukumu yake atageuza yote ya kiswahili yawe kwa kiingereza na hivo. SIKU YA HUKUMU: Yale yaliyoandikwa kwa kiingereza tena yanasomwa kwa kiswahili, wali maharage wali maharage hivyo hivyo. MASKINI WAHUSIKA: Wanatafuta mtafsri. MTAFSIRI: akiwa sio mwanasheria istlahi za sheria zikimpiga mweleka atatafuta wakili. WAKILI: atataka pesa. PESA: haiwapendi maskini
HATIMA: haki haitendeki.
KISWAHILI SIO LUGHA YA WASOMI?!!!
 
hapa nadhani ni suala la urasmi na sio usomi katika lugha. wanahofu kuandika phrase kubwa ya kiswahili wakati ni maneno mawili tu ya kisheria ya kiingereza.
 
Back
Top Bottom