Kiswahili ni lugha ya ngapi duniani kwa ubora?

twalibr2

Member
Mar 17, 2017
82
125
Kiswahili ni miunganiko ya lugha tofautitofauti duniani na nimoja ya lugha tamu na yenye kuvutia pindi uongeapo.je ni lugha ya ngapi kwa ubora duniani?
 
Ubora wa lugha mara nyingi huangaliwa kulingana na idadi ya wazungumzaji kwa ujumla hivyo basi kujua kiswahili ni lugha ya ngapi kwa ubora duniani ni suala gumu kidogo ila ninavyofahamu mpaka sasa ndiyo lugha pekee ya kiafrika yenye wazungumzaji wengi sana ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Msumbiji, Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, Burundi, Rwanda, Comoro. Ina wazungumzaji zaidi ya milioni 100.
 
Sina uhakika sana ni ya ngapi ila ni moja ya lugha zinazosambaa kwa kasi sana Duniani....haikosi kumi bora duniani
 
Ubora wa lugha mara nyingi huangaliwa kulingana na idadi ya wazungumzaji kwa ujumla hivyo basi kujua kiswahili ni lugha ya ngapi kwa ubora duniani ni suala gumu kidogo ila ninavyofahamu mpaka sasa ndiyo lugha pekee ya kiafrika yenye wazungumzaji wengi sana ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Msumbiji, Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, Burundi, Rwanda, Comoro. Ina wazungumzaji zaidi ya milioni 100.

Hakuna lugha bora kuliko nyingine ila kuna lugha zinazotumika na idadi kubwa ya watu. Na kuzungumzwa na idadi kubwa ya watu siyo kigezo cha ubora. kuna vigezo vingi vinavyosababisha lugha kuzungumzwa na watu wengi ama wachache. kwa mfano wengine wanazungumza kiingereza, kifaransa ama Kireno kwa sababu ama ni lugha yao mama, ama walitawaliwa (koloni) na nchi ambazo hizo ni lugha zao mama ama wamezaliwa na kukulia katika nchi zinazozungumza lugha hizo ama wamesomea huko. unaweza kupangilia nafasi za lugha kama ya kwanza, ya pili ....n.k kwa kuzungumzwa na idadi kubwa ama ndogo ya watu.
 
Ubora wa lugha mara nyingi huangaliwa kulingana na idadi ya wazungumzaji kwa ujumla hivyo basi kujua kiswahili ni lugha ya ngapi kwa ubora duniani ni suala gumu kidogo ila ninavyofahamu mpaka sasa ndiyo lugha pekee ya kiafrika yenye wazungumzaji wengi sana ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Msumbiji, Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, Burundi, Rwanda, Comoro. Ina wazungumzaji zaidi ya milioni 100.
Tujivunie lugha yetu
 
Hawaangalii uwingi wa watu bali usambaaji wake kwa nchi mbalimbali katika shughuli za kimaisha.. NB KICHINA NDIO LUGHA YENYE WAZUNGUMZAJI WENGI IKIFUATIWA NA KIHINDI.. lkn lugha namba moja kwa mawasiliano ni ENGLISH
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom