Kiswahili ni kitamu; Ona aibu kukiharibu.

Regnatus Cletus

JF-Expert Member
May 26, 2018
1,114
958
Nimekuwa nikipitia majukwaa mbalimbali mitandaoni, nimeona waafrika wengi wakivutiwa na Kiswahili, hasa wanaposikiliza nyimbo za wasanii kama Diamond Platnumz.

Kiswahili kina viimbo vitamu ambavyo vinaleta ladha ya kipekee na ladha tamu mno kinapozungumzwa na kuandikwa kwa ufasaha wake.

Wote mtakubaliana na mimi, kama mkijaribu kukisikiliza kiswahili cha wakazi walowezi wa dar es salaam, Tanga, na zanzibar. KISWAHILI NI KITAMU MNO.

Tumekuwa tukijinasibu kwamba tunapaswa kukitumia Kiswahili na tuachane na Kiingereza kwasababu ni ukoloni kuzungumza lugha zilizokuja na meli!! NI SAWA, LAKINI, NI KWELI TUNAKIPA KISWAHILI HADHI INAYOSTAHILI?

Watu wengi nchini ni waharibifu wa hii lugha mpaka unajiuliza hawa watu ni watanzania kweli??

Mfano : Nimehona badala ya NIMEONA.

Kura badala ya kula.

Ajala badala ya hajala.

Kumekuwepo na uharibifu wa kutisha wa kiswahili na matokeo yake tunapata lugha za ajabu.

Hivi leo tu tumepata taarifa kuwa Afrika Kusini inataka kufundisha Kiswahili mashuleni kote. Hii inaonesha Kiswahili ni lugha ambayo inaweza kulikamata bara la Afrika lote baada ya miaka kadhaa ijayo.

Kama wazungumzaji wakuu wa Kiswahili, tunakitunza kiswahili inavyopaswa?

MTANZANIA, KITUNZE NA KIPE KISWAHILI HADHI YAKE.
 
Nimekuwa nikipitia majukwaa mbalimbali mitandaoni, nimeona waafrika wengi wakivutiwa na Kiswahili, hasa wanaposikiliza nyimbo za wasanii kama Diamond Platnumz.

Kiswahili kina viimbo vitamu ambavyo vinaleta ladha ya kipekee na ladha tamu mno kinapozungumzwa na kuandikwa kwa ufasaha wake.
:D.
 
hapo sio kujinasibisha ??

Hakika Kiswahili kitamu. Na tunatakiwa tutambue umuhimu wa kujua na kuweza kuongea lugha zaidi ya moja
Kujua lugha zaidi ya moja hakika inaweza kuweka mtu katika nafasi nzuri ya kutangamana bila tatizo na watu wa kabila mbalimbali, mathalani, mtu ajuaye kiingireza na kiswahili atakosa kuona ugumu wa mawasiliano na mwingereza na mswahili panapomhitaji.
 
Ndio uzuri wa kujifunza lugha nyingi.

Unatokea kujiamini na inakupa fursa nyingi za kitaaluma, kiuchumi , kisiasa, na kijamii.

Hapa nilipo niko darasani najifunza kilatini.
 
Mkuu Tuwekee japo 2mistari 2wili 2tatu twa Diamond
Kinachoniumiza nafsi, Kunisikitisha kwa watu kujishongondoa,

Kumbe mapenzi hisabati, wakati nazidisha mwenzangu kwa watu unayatoa,

Wewe cement mimi mchanga, Nikasema penzi tujenge lisijeloa,

Najitia mkandarasi naezeka mabati, kumbe wewe kenchi unabomoa.
 
Back
Top Bottom