We umeandika kitu gani sasa? Utakua muhaya tuMkuu
Inategemea na yule anae ongea kazaliwa wapi, kwa mfano mwanangu hivi sasa ana miaka mitatu, nimemzaa njee ya Tanzania, lugha ya kiswahili ndio tunayo ongea nyumbani, anafahamu everything na ana ongoea japo sio sana, kwa vile ameanza nursery akiwa na Miaka 2, ana peak English kuliko kiswahili, yaani tunashindwa kuelewana lugha kwa kiswanglish, yaani English na swahili.
Sasa mtoto huyu unataka kusema mshamba ? Nina watoto wa brother wangu wamezaliwa nje ya Tanzania, wanaongea kiswahili kama kazaliwa Tanzania, lakini hawawezi kuongea moja kwa moja bila ya kiengereza, hii ni kutokana ni lugha zao mama.
Hata ndani ya Tanzania hasa wale wenye uwezo na walio educated wanawafundisha watoto English kama mother tongue. Hakulia mazingira ya kuongea lugha mbili kwa pamoja.
Ila pia kuna kata bia ya visichana siku hizi wanaongea English kwa kuweka poz tu, ila mi naona kama wana jifunza, lugha bila ya kuongea huwezi ku learning
So what? Nyie ndo waburundiWe umeandika kitu gani sasa? Utakua muhaya tu
Lugha ndiyo nyenzo muhimu popote pale duniani kujipatia maendeleo.Hakuna nchi duniani imeendelea kwa lugha ya mwenzake
Niajabu kumkuta mswahili akichanganya kiswahili na kingereza au mswali ndani ya jamii ya kiswahili akizungumza kingereza.Kwanza niuite ushamba na ulimbukeni wa lugha
Unafikiri usipo ithamini lugha yako unazani nani ataithamini usipopenda cha kwako unafikiri nani atakipenda.Hatuwezi kutumia lugha ya wenzetu tukaelewa mambo
Ajabu sasa mtu yupo chuo kikuu unamwambia zungumza hicho kingereza basi past,future,present zote kazichanganya kueleza tukio la sasa unajiuliza sasa huyu atajua kiswahili hawez kingereza ndiyo kabisa bora liende halafu unategemea tunawataalamu tanzania
Kasumba hili limeingia kwenye elimu ambapo baya zaidi.Leo hii wasomi wengi wanakariri na siyo kuelewa madhara yake swali hilo hilo alilokariri akapata mgeuzie kidogo utasikia sijafundishwa..Matokeo yake tunatoa injinia kwanza ukimpa ajenge baada ya mwez nyufa pili injinia hawezi kushindana na mchina mwenye cheti
Sasa tuendelee kutumia kingereza watoto wa shule za kata wa feli na watoto wa intenational wazidi kufaulu..lugha hii ifundishwe kama lugha nyingine ila mtoto afundishwe kwa lugha yake aelewe na siyo akariri
Mwafaka au muafaka? Maana kiswahili kigumuHoja yako ni ya msingi sana. Kujua lugha ni kuipenda na hasa inapokidhi matakwa ya mtumiaji. Maadalizi yetu sio sahihi kwa watoto wetu. Kosa halipo kwa walimu peke yao hata sisi wazazi tumekuwa na kasumba ya kuchanganya lugha. Hata tunapotumia lugha yetu ya kiswahili kuna maneno hatuyatumii kwa usahihi. Mfano wa neno linalotumiwa vibaya, ni neno "mwafaka". Utasikia mtu anasema ; afadhali ,umekuja muda mwafaka kwa sababu tu alikuwa anamhitaji. Muda mwafaka unatokana na maridhiano. Imepengwa tukutane saa 12.00 jioni. Akifika muda huo, ni sahihi kusema amekuja muda mwafaka na si vinginevyo.
Kukosoa kosa hili tunahitaji tuandae walimu wazuri wa kufundisha lugha kwa kufuata sayansi ya lugha na sayansi ya kufundisha.
Mwafaka au muafaka? Maana kiswahili kigumu