Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Nyanja: Utawala Bora/Haki za Binadamu.

Imekuwa ni tabia kuwa chaguzi zinapowadia huwa serikali nyingi mahala pengi duniani zinafanya mabadiliko ya baadhi ya sera, mikakati na mipango yake ili kuakisi mahitaji ya kisiasa ya ushindi katika chaguzi mbalimbali hasa uchaguzi mkuu ambao ndiyo unaweka madarakani serikali. Mabadiliko yanayojiri kwa mfumo huu mara nyingi yamepwaya katika kuzaa matunda kutokana na kuwa yanakuja kwa hofu na shinikizo za chaguzi na siyo kwa matakwa halisi ya wakati ya jamii husika, na mahala pengine yamezisababishia serikali sintojuwa kutoka kwa wananchi wake. Aidha mabadiliko ni muhimu sana katika kujitathmini kimafanikio ili uweze kuona mbeleni unakoelekea kwa uhakika, lakini pia yanaonyesha uhai wa mtu au kikundi au taasisi au taifa nk.

Hali hii huwa na gharama kubwa sana katika maendeleo ya taifa kwa ujumla wake na huacha pia madhara kama misuguano ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ni bahati mbaya sana kuwa wanasiasa hasa wa bara la Afrika wa kizazi cha pili [baada ya waasisi] kwa ujumla wao [wasomi na wasio wasomi] huwa wanasumbuliwa na tatizo la kudhamiria la upofu/uduni/umaskini/ufilisi wa kifikra kwa sababu historia inaonyesha kuwa huwa mara nyingi wanaangalia mwelekeo mmoja tu wa ushindi katika chaguzi hata kama utapatikana kwa gharama ya roho za watu haijalishi.

Serikali ya awamu ya tatu ilifanya marekebisho makubwa sana ya pili baada ya ile ya awamu ya kwanza iliyobadili mfumo wa elimu kuwa ya taifa toka elimu ya mkoloni [Cambridge System] mwaka 1967 ambayo yaliakisi matakwa na malengo ya Azimio la Arusha na mabadiliko hayo yakaja kuzaa Azimio lake na kupewa jina Azimio la Musoma ambalo lilisisitiza sana juu ya UPE [Universal Peoples Education] [Mwl wangu mmoja akaitafsiri kuwa ni Ualimu Pasipo Elimu] akirejea wanafunzi wengi wenye uwezo wanaokosa nafasi katika sekondari chache zilizokuwepo wakati huo na wengi wao kukimbilia kuajiriwa kama Walimu wa UPE wakipewa maarifa kidogo sana ya kufundisha tena kwenye semina tu na siyo kozi kamili vyuoni.

Lakini pia serikali ya awamu ya kwanza isingekwepa mabadiliko hayo kwa sababu kila kona ya Afrika yaani kila taifa lilikuwa linajinasua toka kwenye makucha ya masalia ya wakoloni ikiwemo kwenye sekta ya elimu hivyo ikabidi Tz tuje na mpango wa elimu ya taifa ambapo darasa la 7 ndiyo kilikuwa kiwango cha msingi cha elimu, ungeweza kuajiriwa kwa kiwango hicho kama ambavyo tumeona mfano wa UPE.

Lakini awamu hiyo ilivunja rekodi kwa kufuta ujinga na kuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kwa kufanikiwa katika mpango wa taifa wa elimu ya watu wazima [Adult Education Programme], mpango wa kufuta ujinga kimsingi ulibuniwa na UN kupitia shirika lake la UNESCO.

Hali hii pia ilijirudia kwenye awamu ya tatu ya serikali kwa kuwaajiri vijana wa kidato cha sita kwa kuwapa semina ya mwezi mmoja na kupangiwa kufundisha sekondari wakabatizwa jina Vodafasta, walioleta jina hili la Vodafasta nadhani walirejea Walimu wale wa UPE waliotokana na Azimio la Musoma.

Aidha katika awamu ya kwanza pia tulishuhudia program za michezo mashuleni na vyuoni zikianzishwa kama UMISETA, UMITASHUMTA kama sikosei n.k. ambazo serikali ya awamu ya nne ilipochukuwa dola ikaziondoa hata kabla utekelezaji wao haujapimwa kwenye mzani kuona kama zilifanikiwa au la.

Sambama na mabadiliko hayo, taifa likashuhudia serikali ikianzisha program za MEM, MES na MEMKWA ambapo tukaona shule pacha zikianzishwa yaani two in one, serikali ikafuta mchipuo wa masomo ya biashara na kubakisha sayansi, sanaa, kilimo, uchumi, maarifa ya nyumbani, ufundi stadi nk.

Huko nyuma pia serikali ya awamu ya pili ilifuta somo la siasa katika ngazi ya msingi na upili na kuibakisha ngazi ya vyuo, na ikaibadilisha na somo la uraia kwa ngazi ya msingi na Civics kwa ngazi ya upili, japo hili wadau wa elimu wanasema kuwa ilikuwa ni kuakisi mahitaji halisi ya mabadiliko ya dunia ya kisiasa, kijamii na kiuchumi [structural change].

Mabadiliko yaliyofunguliwa duniani na Perestroika ya Gor Bachev iliyoanza kwa kubadili iliyokuwa Jumuiya ya Wakulima wa Kisoshalisti wa Sovieti yaani USSR kwanza kwa kuigawa kuwa nchi mbalimbali; mabadiliko yaliyofuatiwa na Ujerumani mbili kuungana kwa sababu muasisi wa Ujamaa USSR alikuwa tayari amefungulia mlango mabadiliko hayo hivyo East Germany ikawa haina cha kujitenga, wakavunja ukuta wa Berlin na kuungana na West Gemany kuunda Germany moja, huku Korea ikiendelea na msimamo wao wa kuwa nchi mbili za Kaskazini na Kusini.

Mabadiliko haya yakasambaa hadi Afrika; ambapo mfumo wa dola kushika hatamu za kisiasa na kiuchumi ulifikia ukomo wake kwa mfumo wa vyama vingi na mfumo wa soko huria kutinga Afrika, Makamisaa na Makada wetu wa Kisiasa wakasisitiza kuwa Tz haiwezi kuwa kisiwa lazima itekeleze mabadiliko haya yasiyo kwepeka ya dunia.

Katika mabadiliko ya mwezi Februari 2015 ya sera ya elimu ya taifa, niligundua kuwa mabadiliko haya yalikuja kwa pupa sana na nilijiuliza kama kweli utafiti wa kina wa kisayansi ulitangulia kufanywa kwanza au yalikuja kwa staili yetu ya siku zote ya zimamoto? Sana sana nimeguswa na jambo moja la msingi sana kwa upande wangu la kutamani mabadiliko ya matumizi ya lugha ya kufundishia toka Kiingereza kwenda Kiswahili.

Nashindwa kuelewa kama matamanio ya mabadiliko haya yalipata fursa ya kujadiliwa kwanza na wadau wa elimu au yalifikiwa kwa staili ile ile ya kusaini kwa siri mikataba ya uwekezaji ambayo mara nyingi imewajibisha serikali nyingi za Afrika.

Katika uchunguzi wangu nilioufanya niligundua kuwa nchi kadhaa za Afrika zina lugha ya taifa kama ilivyo Tz lakini lugha ya kufundishia imeendelea kubaki ile ile waliyorithi toka kwa wakoloni e.g. Malawi lugha yao ya taifa inaitwa Chichewa lakini lugha ya kufundishia ni Kiingereza na Chichewa inabaki kuwa ni somo tu kama masomo mengine ya kawaida.

Nchini Uganda pia wana mfumo huo huo kama wa Malawi lakini lugha yao ya taifa ni Luganda.

Rwanda nayo lugha ya taifa ni Kinyarwanda lakini walikuwa wakitumia Francophone system katika kufundishia, Jenerali Kagame sasa baada ya kushika madaraka ameamua kubadili mfumo toka Francophone kwenda Commonwealth [Anglophone] na kuweka msisitizo pia kwenye Kiswahili kufuatia kugundua unyeti wa Tz katika ustawi wa Rwanda.

Lakini pia Kagame alikwazwa na ukoloni wa Ufaransa katika Kimbari ya mwaka 1994 ambayo ilifuatiwa kwa karibu na Ufaransa kupitia benki yake Banque De France kukubaliana na IMF kushusha kwa zaidi ya nusu, thamani ya sarafu yake ya French Franc dhidi ya dola ya Marekani na kuathiri raia takriban milioni 140 wanaoishi kwenye makoloni ya Ufaransa ya Afrika Magharibi na Kati walioshushiwa thamani ya sarafu yao ya CFA ambayo siku zote iliegemea kwenye nguvu ya French Franc.

Jenerali Kagame akaamua kubadili hata jiografia ya nchi yake toka kuwa Afrika ya Kati hadi kuwa Afrika ya Mashariki. Mabadiliko haya ya thamani ya sarafu ya Ufaransa yaliyoathiri CFA ya Francophone Africa na kuvuruga chumi za Francophone Africa ni makubwa baada ya yale ya 1945 yaliyokuja kama mkakati wa kujipanga na madhara ya kiuchumi ya vita kuu ya pili ya dunia.

DR Congo pia wana lugha zao za kimajimbo lakini lugha ya kufundishia imebaki kuwa Kilingala ambacho nafikiri kinaoana na Kifaransa maana DR Congo ni koloni la Ubelgiji.

Somalia lugha yao ya taifa ni Kisomali, lakini lugha ya kujifunzia ni Kiarabu na Kiingereza.

Nachelea kuamini kuwa hawa waliokuja na mabadiliko ya sera hii ya elimu hawakufanya utafiti wa kina wa kimazingira kwa kujifunza toka nchi zenye lugha za taifa na zinazotumia lugha ya kikoloni katika kufundishia.

Lakini zaidi ni pale ambapo nalazimika kuamini kuwa hawa waliokuja na sera hii walijitoa hata akili kidogo tu ya kuangalia hata pale Afrika Kusini ili wajifunze na madhila ya mabadiliko ya kisera ya elimu yaliyoliingiza nchi hiyo kuandika historia yake kwa wino wa damu za watu, historia isiyofutika ya vizazi na vizazi ambapo watu wapatao 69 wakiwemo wanawake 8 na watoto 10 walipigwa risasi na vikosi vya makaburu kufuatia wazalendo kuamua kuandamana kupinga sera ya elimu iliyoletwa na makaburu ambayo weusi walihisi inawabagua na ingewabagua katika ajira, sera hiyo pamoja na mambo mengine ilitaka weusi wafundishwe kwa lugha ya Ki-afrikaana na siyo Kiingereza.
OIP.32o5Qremqfh6nFcD5wIK_QHaEL

Kilichowatatiza weusi ni kuwa wangewezaje kuajirika ndani na nje ya Afrika Kusini kwa kuongea lugha ambayo haiongelewi huko ya Ki-afrikaana? Kwa maneno mengine ni kuwa Wazalendo wangeajirika ndani ya Soweto tu ambako ndiko ngome ya lugha hiyo na kwamba wasingeweza kuajirika hata kwenye majimbo mengine ya Afrika Kusini ambako Ki-afrikaana hakiongelewi achilia ng'ambo ya nchi.

Je, kuna mtaala wa ki-daktari, ki-sheria, ki-hasibu, Ki-utawala, Ki-sayansi nk ambao uliandaliwa na serikali ya makaburu katika lugha ya Ki-afrikaana ili kwamba weusi hawa watapofuzu mafunzo basi waweze kuajirika kwa kuwa wataweza kuendesha taaluma zao katika lugha hiyo ya kikabila na kwamba hata soko la nje la ajira wahakikishiwe kuwa linatumia lugha ya Ki-afrikaana pia? Baada ya majibu maridhawa kukosekana toka kwa makaburu ndipo moto ukawaka, ANC ikaitisha maandamano katika jimbo-ngome yake ya Soweto tarehe 31 Machi 1960, PAC ikaiwahi ANC na kupoka ajenda ya maandamano na kuyaita siku kumi kabla ya tarehe ya ANC yaani 21 Machi 1960 na kuyaita Soweto Uprising.
R.a8c88a35de7d4d4230f6b10bc3f663d2


Sasa hawa wataalamu wetu wa hapa nyumbani Tanzania waliofikia uamuzi wa kubadili sera ya elimu yetu kwa kuamua kuwa Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia, waliweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Afrika Kusini? Au ufahamu wao ulishindwa kufanya kazi nyuzi 360 ukagota tu kwenye nyuzi 90 [hapa nchini tu]? Je, hawajui kuwa siku zote mabadiliko katika kuendesha mambo ya nchi huwa lazima yawe na sehemu ya kuyaakisi na kuyarejelea?

Naombeni kura zote.


Taswira zote kwa hisani ya:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom