Kiswahili kiacheni tu jamani

Kiswahili kiacheni tu jamani

Mi ningependa kujua kama hayo maneno yapo Kamusi gani ya kiswahili?
 
Mim nilikuwa najua puku,kiungo na baobonye nilishayaona hayo maneno kwenye tovuti ya wikipedia lakin hayo mengine hapana kuna neno tarakilishi mpakato, nilisikia kwenye st swahili ikiwa na maana ya laptop
kweli kabisa
 
Aaah! Hicho sio kiswahili ila ni Kiruga

Bora Kiingereza kiingereza ni *chepethi
 
Habari za leo. Napenda kuwapa rai ndugu zangu.
Najua sisi sote humu ndani ya hili *_kundi sogozi_* tunamiliki _*simu tamba*_. Tuweni makini kwani kutumia _*sikanu*_ zetu _*mkondoni*_ kunaweza wapa mwanya wezi wa mtandaoni kutuibia. Wezi hutuma _*maunzi laini*_ yanayoweza kuharibu _*kitumi*_ chako au kuingilia _*makavazi*_ ya _*sikanu*_ yako. Wakishatuma _*maunzi laini*_ hayo nawe pasi na kujua ukibofya _*kiungo*_ kilichobeba _*maunzi laini*_ unakuwa _*umeshapakua*_ na _*kusanidi mtaliga*_ wenye uwezo wa kubadili au _*kughushi nenomsingi*_ lako na hivyo kunyima uwezo wa kuitumia _*sikanu*_ yako kwa kuifanya _*puku*_ kushindwa kutambua amri unazoipatia _*baobonye*_ ya _*kiwambagusa*_ cha _*sikanu*_ yako.

*JE KISWAHILI KITUMIKE KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA KWA NGAZI ZOTE ZA ELIMU?*


*Tafsiri ya maneno hayo*

1. Kundi sogozi = chatting group
2. Sikanu = smartphone
3. Kitumi=device
4. Maunzi laini=software
5. Kiungo=link
6. Kusanidi=install
7. Mtaliga=virus
8. Neno msingi=keyword
9. Puku=mouse
10.Baobonye=keyboard
11. Kiwamba gusa=touch screen
12. Makavazi=archives
13. Simu tamba=mobile phone
14. Mkondoni=online
15. Pakua=download


C&P
@Joseverest,Asante kwa kutuongezea kamusi hii ya maneno je wapi tunaweza pata maneno mengi zaidi kuongeza kamus zetu kwa wakati?
 
@Joseverest,Asante kwa kutuongezea kamusi hii ya maneno je wapi tunaweza pata maneno mengi zaidi kuongeza kamus zetu kwa wakati?
Kwenye vyanzo mbalimbali mfano Majukwaa ya elimu hasa Lugha, vitabu mbalimbali na Hata Kamusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom