Kisutu yakataa kumfutia Tundu Lissu mashitaka.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ya kufutiwa mashitaka ya uchochezi yanayomkabili na wenzake watatu.

Hakimu Mkazi Mkuu, Emillius Mchauru alitoa uamuzi huo jana baada ya kukubali pingamizi lililowasilishwa na upande wa Jamhuri waliodai mashitaka hayo yasifutwe kwa kuwa hati ya mashitaka haina makosa.

Mbali ya Lissu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mwandishi wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob. Hata hivyo, uamuzi huo ulitolewa jana bila Lissu kufika mahakamani hapo kwa kuwa anaumwa.

Akiieleza mahakama, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai Lissu ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa, lakini wadhamini wake akiwemo Ibrahim Ahmed wamefika mahakamani na kueleza kuwa Lissu anaumwa malaria. Aidha, ilielezwa kuwa mshtakiwa Idrissa anaumwa na yupo Zanzibar kwa ajili ya matibabu.

Katika maombi yao, washitakiwa kupitia kwa Wakili Kibatala waliiomba mahakama ifute mashitaka hayo kwa kuwa hati ya mashitaka imekosewa kwa kutokueleza makosa hayo wametenda wapi na pia mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza masuala yanayohusu Zanzibar.

Akisoma uamuzi, Hakimu Simba alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote mbili katika kesi hiyo imejiridhisha kuwa hati ya mashitaka haina makosa.

Aidha, alisema mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa makosa yaliyofanyika yanahusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni, mahakama ilifuta mashitaka mawili ya uchochezi kati ya matano yanayowakabili washitakiwa hao, baada ya upande wa jamhuri kuyaondoa katika hati kwa kuwa hayana kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Katika mashitaka yao inadaiwa Januari 12 hadi 14, 2016, Dar es Salaam washitakiwa wachapisha taarifa ya uchochezi yenye kichwa cha habari ‘ Machafuko yaja Zanzibar’.

Pia inadaiwa Januari 14, 2016 Dar es Salaam walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar. Inaendelea kudaiwa siku hiyo hiyo, Lissu na wenzake bila ya kuwa na mamlaka yoyote yale waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar ili wasikubali kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.
CHANZO: Habarileo
 
Siasa za Tanzania ndani ya mfumo wa vyama vingi ukizichunguza kwa makini utagundua huwa zina namna( pattern) inayofanana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na baada ya Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka mitano.

Kinachotokea kwa sasa kuhusu polisi na vyama vya upinzani hasa chama kikuu cha upinzani hayana tofauti na kilichotokea miaka ya nyuma. Tofauti yake ni ajenda ambayo inakuwa ni kichocheo cha viongozi chama kikuu cha upinzani kukwaruzana na polisi.

Katika chaguzi za nyuma, ajenda kuu iliyokuwa inachochea mikwaruzano na migongano kati ya polisi na wapinzani baada ya Uchaguzi Mkuu ilikuwa ni kuibiwa kura. Mwaka huu ajenda ni kuminywa kwa demokrasia.

Dhumuni kuu la hii mikwaruzano na migongano baada ya Uchaguzi Mkuu ni wanasiasa kuonyeshana ubavu ili hatimaye heshima iwepo kati yao. Wanachokifanya ni kile waingereza husema,’’ testing the waters’’.

Kwa sasa bungeni wameishaonyeshana ubavu na wameheshimiana. Wameishafamu kina cha maji kati yao. Tumemuona juzi Mbunge Msigwa akiwa pamoja na Dkt. Tulia. Bunge la Kikao kijacho litakuwa tofauti ukilinganisha na kile kimemalizika.

Ndani ya miezi 12 baada ya Uchaguzi Mkuu, hizi kelele zote za kusema dikteta uchwara au demokrasia zitaisha kwa sababu wanasiasa watakuwa wameheshimiana baada ya kufahamu kina cha maji kati yao. Tusije kushangaa kumuona Lissu akiwa pamoja na Rais Magufuli.

Historia inatuambia hakuna kiongozi mkuu wa kisiasa aliyehukumiwa kifungo gerezani kwa kosa la kuandamana bila ruhusa au kutamka maneno yanayohatarisha amani baada ya kipindi cha mpito cha Uchaguzi Mkuu. Baada ya Uchaguzi Mkuu 2010.

Sitashangaa kuona hizi kesi za kina Tundu Lissu zikibaki kwenye mafaili ya mahakama bila kutolewa hukumu.
 
Back
Top Bottom