Kisulisuli na kuolewa bila dalili

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Amani iwe nanyi,

MIAKA 27 NA KWENDA JUU ni miaka yenye changamoto sana kwa wanawake, kwani katika miaka hii wanawake wengi wasipoolewa hujikuta wakiwa na pupa na mahusiano na matokeo yake kugeuka watumwa wa mapenzi.

Ni katika miaka hii, wanawake wengi hujikuta wakisahau vigezo vya wanaume wanaowataka na kuamua kuolewa na JITU lolote lenye jinsia ya kiume kwa sababu ya hofu ya kutoolewa.

Ni katika miaka hii, wanawake wengi hulazimika kubadili dini ili wawahi ndoa kwa sababu hudhani wakiacha kufanya hivyo wataachwa na bahati ya ndoa.

Ila cha kusikitisha sana, pupa hii ya kuwahi ndoa hata kwa kulazimika kubadili dini na kusahau vigezo vyao vya awali haiwapi wanachotaka, wanaweza kupata ndoa ila wakakosa amani na raha ipatikanayo katika ndoa, matokeo yake hujihisi na mikosi na balaa.

Hisia hizi za kudhani wana mikosi, huwapelekea kukosa amani zaidi hata kuwafanya wafikirie maamuzi ya hovyo ama kupata maradhi ya kisaikolojia kama vile PSYCHOPATH.

Mapenzi yanayolazimishwa kwa sababu yoyote ile, hugeuka kuwa sukari iliyoungua hivyo haiwezi kukupa utamu wa sukari ila itakupa uchungu wa shubiri usioutarajia.

FB_IMG_1571627864842.jpeg


Batani ya sauti imeng'oka nadhani nimesikika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom