Kiss of poverty: Busu moja tu akawa maskini

mcshonde

Member
Jul 15, 2022
66
152
CF697DE5-3A3F-4641-8D73-07D96512EE6F.png


Murang'a Kenya: Hadithi ya mzee Tom Ikonya (60) kufyonzwa zaidi ya Tzs milioni 12 na mwanamke waliyekutana naye baa imeibua hisia tofauti kwa watu.

Mzee huyu aliyetafuta mali kwa miaka mingi, Novemba 2022 aliamua kuuza baadhi ya mali zake na kwenda mjini Maragua. Alipofika tu akapitia baa kupoza koo kidogo ndipo akaja mhudumu ambaye alimpa busu motomoto lililomchanganya kiasi cha kusema "Ndio" kwa chochote alichoambiwa na mrembo huyo...ikiwemo "Twende kwangu".

Ikonya aliishi kwenye nyumba ya mwanamke huyo kwa siku sita akioga, kula na kulala.

Kwa siku hizo, mwanamke huyo alikuwa anampa Ikonya mapendekezo mbalimbali ya kimaendeleo kama kufungua bucha n.k kisha kumuomba kadi ya benki ili atoe pesa ya kuanzisha miradi hiyo. Siku ya sita mzee huyu alijikuta amebakiwa na TZs 150 pekee.

Kwa siku chache zilizopita, hali ya kimaisha imekuwa ngumu kwa mzee huyu ambaye anajuta kuruhusu kupigwa “busu la umaskini”.

Tangu mwisho wa mwaka 2022 aliposimulia mkasa huu, wadau wengi kwenye mitandao ya kijamii wamemuonea huruma mzee huyu kufuatia yaliyomsibu.
 
Hii ndo inaitwa kufungwa goli la ushindi dakika za majeruhi hata kabla ya penalty
 
Back
Top Bottom