Kismayo Somalia, Asante KDF!

Kafrican

JF-Expert Member
Jan 26, 2015
7,212
6,972
Kuna mwengi ambayo miji miengine ya Kusini na kati ya Somalia yanaweza yakajifunza kutokana na maendele ya mji mkuu wa Kismayu ambao ndo mji wa Mkubwa Somalia baada ya Mogadishu. Wakati miji miengine ya Somalia ikiwemo Mogadishu inakumbwa na mashambulizi makubwa mara kwa mara, Kwa miaka saba sasa tangu KDF wafike Kismayu, hakujawahi tokea shambulizi lolote kuu (hadi mwanzoni mwa mwaka huu)... Hii imeanya Kismayu kua the safest City in Central and Southern Somalia.

Alafu cha kufurahisha zaidi, Mji huu ambao uko ndani ya Jubaland federal state, kwa sasa KDF na AMISOM walijiondoa ndani ya mji baada ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi na viombo vya Usalama vya Jubaland, Yani ni wanajeshi na polisi wa Jubaland wenyewe ndo wanalinda mji. mpaka wako na kikosi spesheli cha wanajeshi ambao ni former Alshabaab members ambao sasa ndo wanatumika kushambulia alshabaab! Kwa kifupi, Naona Serekali yaJubaland iko tayari kuchukua usukani na kuanza kujilinda....Wanacho hitaji sasa ni bajeti ya kuongeza wanajeshi na kuweza kuwalipa mishahara.







Hii hapa Video ambapo Mwanahabari wa Kisomalia anasema Kismayu is the safest city in Central and Southern Somalia
 
Back
Top Bottom