Kisima cha gesi Mtwara hatarini kumezwa na bahari

Kisima cha gesi Mtwara hatarini kumezwa na bahari

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Kutokana na kina cha bahari ya Hindi katika eneo la Mnazi Bay Msimbati mkoani Mtwara kuendelea kumomonyoka siku hadi siku kuelekea nchi kavu, huenda nchi ikajikuta gizani kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Hayo yamesemwa jana Jumatatu Desemba 4, 2018 na Naibu mkurugenzi wa Kampuni ya Maurel & Prom Tanzania inayohusika na kuchimba gesi, Elias Kilembe kwa Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alipotembelea visima hivyo vya gesi.

Kilembe alisema siku hadi siku bahari inasogea nchi kavu kuelekea kilipo moja ya kisima cha gesi na mitambo hali inayowapa wasiwasi.

“Hata mwaka jana ulitokea mmomonyoko lakini haukuwa tishio kama wa mwaka 2015, lakini ukija hapa baharini unakuta mchanga umeondoka wote na kupotea, kweli ni tishio kwa kambi hii,” alisema Kilembe.

Waziri wa nishati, Dk Kalemani amesema hali halisi inaonekana na hakuna haja ya utafiti, bali kinachotakiwa kufanyika ni kujengwa kwa ukuta haraka ambao utatenganisha kisima kilipo na bahari ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

“Kuanzia sasa anzeni kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika mahala mtakosa hata pa kuweka ukuta maji yakishafika huku, ni vizuri kuanza sasa ili msije kukumbwa na dhoruba kubwa, haya ni maagizo ya haraka haraka wala si jambo la kufanya utafiti,” amesema Dk Kalemani.
 
Kwani kikizama nani anakula hasara?
Waliojimilikisha gesi kinyemela wajiandae kisaikolojia
Sisi tunaendelea kujenga jiji la Mungu
 
Kibomoke tu maana gas yenyewe hatujui mapato yake yanaenda wapi mpaka mkuu alisema gesi imechukuliwa na wakubwa...cha kuogopa ni madhara ya mazingira tu
 
Sitaki hata kuisikia hii gesi maana tuliaminishwa mauzauza kibao matokeo yake haitusaidii watanzania wala kuwasaidia wananchi wanaouzungunguka mradi
 
Ni nani aliyemwambia kwamba maji huwa yanazuiwa. Maji yaonyeshe mkondo yapite jombaa.
 
Hiyo gesi inatusaidia nini sisi kama watanzania??acha vimezwe tukose wote!!
Kwani kikizama nani anakula hasara?
Waliojimilikisha gesi kinyemela wajiandae kisaikolojia
Sisi tunaendelea kujenga jiji la Mungu
Kianze kutafunwa kwanza ndio kimezwe ili hata kikiharishwa baadae kisifae.
Kibomoke tu maana gas yenyewe hatujui mapato yake yanaenda wapi mpaka mkuu alisema gesi imechukuliwa na wakubwa...cha kuogopa ni madhara ya mazingira tu
Sitaki hata kuisikia hii gesi maana tuliaminishwa mauzauza kibao matokeo yake haitusaidii watanzania wala kuwasaidia wananchi wanaouzungunguka mradi
Kimezwe tu hakuna faida kwetu Sisi tena kibomoke ili kiwe na miksa na maji ya bahari
Ni nani aliyemwambia kwamba maji huwa yanazuiwa. Maji yaonyeshe mkondo yapite jombaa.
Mpaka hapa sasa nimeamini watanzania mmechoka kwa hizi coment zenu kama mliambizana vile
 
hahaha...maji ya bahari yanazuiwa na ukuta...hahahaha
 
Hayo yamesemwa jana Jumatatu Desemba 4, 2018


Are you seriuos na tarehe hiyo kwamba Jumatatu ilikuwa tarehe 4!? Tutakuamini vipi kuwa umeandika habari sahihi kama kitu kidogo tu tarehe umedanganya, vipi kuhusu masuala yaliyomo ya kitaalamu si utakuwa umetuhadaa sana?
 
Back
Top Bottom