GE2025 KISHOA: Najilaumu nilichelewa wapi kujiunga CCM

GE2025 KISHOA: Najilaumu nilichelewa wapi kujiunga CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jesca Kishoa, amesema anajilaumu kuchelewa kujiunga na CCM baada ya kutumia muda mrefu akiwa Chama cha CHADEMA.

Soma pia: Aliyekuwa diwani wa CCM kata ya Themi, lobora ahamia CHAUMMA Agosti 16


Chanzo: Daily News

Akihutubia leo Septemba 10 kwenye mkutano wa kampeni wilayani Iramba, Kishoa amesema CCM ni chama kikubwa chenye mfumo imara wa kusaka viongozi na wagombea, hivyo uteuzi wake si kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya utaratibu mzuri wa chama hicho. “Nimegundua nimechelewa wapi, CCM ni chama makini, kinajali watu wake na kinaweka viongozi bora kwa misingi ya haki na uadilifu.

Hapa ndipo nyumbani pa siasa zenye tija,” amesema Kishoa. Amehitimisha hotuba yake kwa kuwasihi wananchi wa Iramba Mashariki na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 kumpa kura Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wote wa chama hicho.
 
Back
Top Bottom