Kishindo cha BAVICHA mkoani Rukwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kishindo cha BAVICHA mkoani Rukwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Scolari, Jul 26, 2012.

 1. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu Habari zilizonifikia ni kwamba viongozi wakuu wa BAVICHA John Heche Mwenyekiti na Katibu Mkuu Deogratias Munishi jana waliutetemesha mji wa Mpanda kwa kuishukia vikali CCM na Sekikali yake kwa kuidhoofisha Tanzania kimaendeleo.

  Wakati John Heche akiwataka polisi kumtia mbaroni Martini Shegela kwa uchochezi wa kuwataka vijana wa ccm kupambana na wale wa Chadema na pia kuongeza kuwa hata kama ni kupambana basi watoto wa ccm ni watoto wa laktojeji na wale wa Chadema ni ngangari kweli kweli katibu mkuu wa Bavicha Deo Munishi amesema mikutano ya Chadema hailindi na jeshi la polisi ama kikundi chochote kile bali wananchi wenyewe hivyo CCM wanapojipanga kuvamia mikutano hiyo daima wataangukia pua.

  Wakati John Heche akisema kuwa umasikini wa Tanzania unasababishwa na uchovu na udhaifu wa serikali ya CCM chini ya Kikwete, Pinda na Makinda, Munishi aliwaambia wananchi wa mpanda kuwa katika kushughulikia tatizo la umasikini Tanzania hakuna njia ya mkato zaidi ya kuunganisha uchumi wa vijijini na wa mjini na hii ni kwa kupitia mapinduzi ya KILIMO ambacho ni msingi wa mapinduzi ya viwanda nchini na si kwa ngonjera na mapambio ya kilimo kwanza ya serikali ya CCM.

  Munishi alisema kuwa CCM ni janga la taifa, ni laana kwa taifa na ni mkosi kwa taifa na ana uhakika thabiti kuwa kuendelea kuwepo kwake Tanzania ni kuendelea kuhatarisha utulivu uliopo ambao wao CCM wanauita amani. Wakati John Heche akiendelea kuonyesha udhaivu wa serikali ya CCM kwa kusema kuwa ni aibu kwa rais Kikwete kuendelea kuiabisha Tanzania kwa kuwa matonya na kumtaka aone aibu kwa kupishana angani akiwa na misaada ya vyandarua akitokea ughaibuni huku akipishana na wazungu angani wakitokea Tanzania wakiwa na dhahabu Deo Munishi aliwageuzia kibao CCM kwa kuwaita chama cha Magaidi kwani kimekua kikiratibu vitendo vya kigaidi akitolea mfano vile vya Sigida chini ya Mwigulu Nchemba aliyekodi vijana kutoka Dar es salaam kufanya vurugu kwenye mikutano ya Chadema na vile vya Iringa alivyofanyiwa Mchungaji Msigwa kwenye mikutano ya Chadema.

  Munishi aliendelea kuwataka wananchi wa Rukwa na mpanda kuwa makini katika mchakato wa katiba mpya kwa kuwaomba wananchi wakatae uwepo wa vyeo vya wakuu wa wilaya na mikoa kwa kuwa ni sehemu ya mzigo kwa walipa kodi kwani hawana kazi wanazozifanya.

  Leo vijana hawa wataendelea kutikisa katika jimbo la Mpanda Vijijini na kesho watamshukia Waziri Mkuu kwenye jimbo la Mpanda Mashariki na Ijumaa watautetemesha Mji wa Sumbawanga.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu, wewe ni mwandishi profeshino.
  Nimefurahia sn uandishi wako ambao ni detailed na elaborative kabisa, ukiacha kuwa hujatuwekea PICHA.
  Ccm hakika sasa wakubali tu kuwa cdm ni chama chenye umakini, na waache kukitungia propaganda za kinapenape.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kanyaga twende M4C, sie sera wao propaganda na SMS SPOOFING!, haturudi nyuma!
   
 4. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ninafanya jitihada kupata picha za makamanda hawa na nitazitia hapa pindi nitakapozipata mkubwa
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ukizipata utupiamo tuzione. They talk more than words
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Naona hawa watoto wa CCM hawajawahi kupata kichapo. Haya maswala ya kufanya fujo yatawaponza, hatuwapendi. Waache CDM wafanye siasa zao za amani.
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huu uzi umeandikwa, ukaandikika.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ssa Chadema imekuwa ngangari ?
   
 9. Encyclopaedia

  Encyclopaedia Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viva Chadema
   
 10. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimemsikia Anne Kilango akimlalamikia Pinda kuwa M4C wanapita 'kwenye majimbo yao', cha ajabu hata Pinda naye akaunga mkono na kuanza kutoa vitisho kana kwamba CHADEMA wanavunja sheria kwa kuwaamsha wananchi.

  Nani aliwapa hayo majimbo kuwa "mali yao"? Nimegundua ccm imechanganyikiwa sasa. M4C hadi kieleweke.
   
 11. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwao ccm ni upepo tu utapita...............
  mkakati pekee waliobakiwa nao ni SMS Spoofing. Ndio risasi yao ya mwisho, ikishindwa hiyo wanahamia mabwepande. Eee! Mungu, wafungue macho waone kuwa mwisho wa utawala wao, umefika waondoke kwa amani bila kung'oa miche ya bustani yetu "TANZANIA"
   
 12. b

  bashemere Senior Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RITZ NA WENZAKE WANUMIA KWA UCHUNGU LAKINI UKWELI UNAUMA NCHI INAONGOZWA NA CHADEMA 2015:israel:
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Safi sana kamanda kwa taarifa,
  kama kuna mapix tupia mkuu.
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kazi nzuri...Ungetupiamo vipicha na idadi waliovua magamba ingekuwa muswano mbaya!:A S-baby:
   
 15. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mods kama inawezeka mwamishie Scolari Rep Power za Mwiba:nerd:
   
 16. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  safi sana makamanda.
   
 17. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viva chadema. Vijana endeleeni kueneza elimu ya uraia.
   
 18. ngalelefijo

  ngalelefijo JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 1,800
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  kESHO nitatoka mapema kazini nikawasikilize na kuwapa tano m4c.Duh anapishana na ndege yeye kabeba vyandarua wao madini yetu.Ana roho ya paka kweli haoni aibu wajameni?Nitajitahidi niwape ile cd ya MAPOVU YA MWIGULU NA NAPE WAKATI WANAHUTUBIA kindergatten na akina mama waliokuwa wakichuuza ndizi chini ya miti pale msakila.Jamani wana rukwa au wana pembezoni shime tuje kwa wingi
   
 19. a

  agapetc Member

  #19
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  saaaaaaafi
  natamani uchaguzi ungekuwa kesho tu,ikulu ingetikisika
   
 20. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mwahga Sumu 2015 maji kwa glass
   
Loading...