Kisarawe: Walimu walazwa uchi na kuchapwa viboko

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,527
865
Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.

Walimu hao wanakumbana na matukio ya ajabu ikiwamo kujikuta uchi, kupigwa fimbo na mtu asiyeonekana na kulazwa nje ya nyumba zao.

Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kutokana na matukio hayo kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyingine, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.

“Tarehe 26 mwezi wa pili, siku ya Alhamisi sitaisahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa,” alisema Shaaban.

Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipotibiwa kienyeji.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Mbelwa alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa.

Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.

Mzazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.

Mratibu wa Elimu wa Kata ya Marui, Damaru Charles alisema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawasilisha ngazi za juu.

Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa, Aurelia Rwenza alisema tatizo hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika sehemu hiyo.

“Kwa kweli walimu wameathirika, hivi sasa tunatakiwa kuwajenga kisaikolojia,” alisema.

Chanzo: mpekuzihuru
 
Walimu! Mnapopangiwa kwenye vituo vya kazi hasa vijjni kueni makini sana maana kuna baadhi ya vijiji walimu ndio wenye vipato zaidi ya wengine, kwahiyo ::-

-msijione bora kuliko wenyeji.
-msiwachape saana watoto wa watu.
-waheshimuni saana wazee wa vijiji.
Vilevile muheshimiane, mshirikiane, na mpendane nyinyi wenyewe katika kazi, maana kuna baadhi ya walimu pia sio watu wazuri.

Ni ushauli tu.
 
Pole yao, hofu yangu ni walimu wakisusa kufundisha huko, hasara ni kwao walimu ama watoto wa wana-kijiji hicho?!

Jamii ibadilike jamani, teknolojia hiyo waitumie kwa manufaa, wajitokeze waitangaze, na siyo kunyanyasa watoto wa wenzao.

Aibu yao pia walaaniwe wachawi hao / wote.

Ahsante!
 
Hawa wanaonyesha hawataki kabisa elimu bora waletewe wachina wawafundishe elimu ya tiba asili na tiba mbadala ili mwisho wa siku ijulikane kabisa kuwa kisarawe ndio sehemu tengefu na maarufu nchini tanzania Kwa kutumia nguvu za Giza ili kutibu mambo mbalimbali . Wachina hawawezi ku shindwa kuwa fundisha uchawi ukizingatia wamesha onyesha uwezo wao kidogo Kwa mtindo huo watajiongezea vipato maana wana kisarawe hawa elimu ya taaluma zingine kwao ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa kweli kabisa hovyo kabisa

Mshana Jr Uko wapi njoo uone kisarawe ahahahaahhhh
 
Mshaurini jafo akaongee na wazee wa kisarawe wayamalize hataikiwa mm huwezi kunipa kazi ya kufundisha maeneo kama hayo ikibidi wawapeleke wazawa wahuko huenda wakawezana
 
Maeneo yenye watu wa tabia kama hizo kupata elimu na hatimaye maendeleo itakuwa ndoto. Hii ni moja ya vikwazo vya elimu katika nchi yetu. Wanaotoka sehemu hizo, watakuwa nyuma kielimu siku zote.
 
Hapa ndo utaona ni kwa namna gani viongozi wa jawa walimu hasa DEO alivyo na kuweza kuhandle hiyo problem properly.
Iliwahi tokea mahala fulan michezo kama hii ya kucheza na walimu miaka ya 90 hvi niliipenda ile approach;
Mosi, DEO alifuata walimu wake wote shule ikabakia na wanafunzi bila mwalimu wakahamishiwa shule nyingine
Pili, waliwekewa embaggo hakuna mwanafunzi kuhama wala kuhamia shule ile yenye tabia hatarishi
Tatu, walipewa muda tu wa kuwatafuta watuhumiwa.
Hiyo ilisaidia sana masna wazee wenye busara na makini wa kijiji walijiunga wakaenda kwa DEO kumwomba radhi na kuahidi tabia kama hiyo haitorudia na kwamba wameshakanyana vya kutosha. Kilichofuata ni kuanza kupelekewa walimu wachache kwanza kwa gharama zao ile tabia ilikoma kijiji kile waliwaheshimu walimu maana walikuwa wameonja joto ya jiwe.
Sasa unakuta afisa elimu amelegea legea tu nani atawaheshimu staffs wako?
Yaani hawa mnawatengenezea machenism nzur ya kuwaonesha wakati wao wanaona walimu wa nni wenzao wanasema watawapata lini.
Tabia za kijinga kbsa hzi.
 
Kukutana na magumu kama haya ni kawaida,ni moja ya changamoto katika maeneo ya vijijini,mwalimu hutakiwi kuogopa,jamii ya hapo ipewe elimu kuhusu ubaya wa vitendo hivyo.
 
Kukutana na magumu kama haya ni kawaida,ni moja ya changamoto katika maeneo ya vijijini,mwalimu hutakiwi kuogopa,jamii ya hapo ipewe elimu kuhusu ubaya wa vitendo hivyo.[/QUOTE

Uko sahihi, na woga wako ndio udhaifu wako kwa wachawi, gakuna haja ya kuogopa kabisa.
 
Walimu! Mnapopangiwa kwenye vituo vya kazi hasa vijjni kueni makini sana maana kuna baadhi ya vijiji walimu ndio wenye vipato zaidi ya wengine, kwahiyo ::-

-msijione bora kuliko wenyeji.
-msiwachape saana watoto wa watu.
-waheshimuni saana wazee wa vijiji.
Vilevile muheshimiane, mshirikiane, na mpendane nyinyi wenyewe katika kazi, maana kuna baadhi ya walimu pia sio watu wazuri.

Ni ushauli tu.
kwakweli hayo ni moja ya mambo ya msingi ya kuzingatia.
 
Walimu! Mnapopangiwa kwenye vituo vya kazi hasa vijjni kueni makini sana maana kuna baadhi ya vijiji walimu ndio wenye vipato zaidi ya wengine, kwahiyo ::-

-msijione bora kuliko wenyeji.
-msiwachape saana watoto wa watu.
-waheshimuni saana wazee wa vijiji.
Vilevile muheshimiane, mshirikiane, na mpendane nyinyi wenyewe katika kazi, maana kuna baadhi ya walimu pia sio watu wazuri.

Ni ushauli tu.
Naomba nikukosoe kwa baadhi ya maoni yako;Kuhusu kujiona bora,naona km haupo sahihi,wapo ambao Mtumishi wa Serikali hata ukijishusha vipi bado watasema unajiona,Kuhusu kutowachapa sana watoto hiyo ni ngumu kwasababu Ili maendeleo ya Kinidhamu na Kitaaluma yawepo lazima kiboko kitumike,kuacha kutumia kiboko eti kisa unaogopa wazazi wa watoto huo ni Uzumbukuku,Kuhusu kuwaheshimu wazee sawa ndio tamaduni zetu watanzania,lkn je kipimo cha heshima ni kipi??,Ya mwisho hiyo ninakuunga mkono.lkn Jambo la Msingi sana Mshikeni sana Mungu kwani yeye ndiye mwenye uweza.
 
Hapa ndo utaona ni kwa namna gani viongozi wa jawa walimu hasa DEO alivyo na kuweza kuhandle hiyo problem properly.
Iliwahi tokea mahala fulan michezo kama hii ya kucheza na walimu miaka ya 90 hvi niliipenda ile approach;
Mosi, DEO alifuata walimu wake wote shule ikabakia na wanafunzi bila mwalimu wakahamishiwa shule nyingine
Pili, waliwekewa embaggo hakuna mwanafunzi kuhama wala kuhamia shule ile yenye tabia hatarishi
Tatu, walipewa muda tu wa kuwatafuta watuhumiwa.
Hiyo ilisaidia sana masna wazee wenye busara na makini wa kijiji walijiunga wakaenda kwa DEO kumwomba radhi na kuahidi tabia kama hiyo haitorudia na kwamba wameshakanyana vya kutosha. Kilichofuata ni kuanza kupelekewa walimu wachache kwanza kwa gharama zao ile tabia ilikoma kijiji kile waliwaheshimu walimu maana walikuwa wameonja joto ya jiwe.
Sasa unakuta afisa elimu amelegea legea tu nani atawaheshimu staffs wako?
Yaani hawa mnawatengenezea machenism nzur ya kuwaonesha wakati wao wanaona walimu wa nni wenzao wanasema watawapata lini.
Tabia za kijinga kbsa hzi.
Mkuu, huyo Deo ni nani???
 
Back
Top Bottom