Kisarawe: Walimu walazwa uchi na kuchapwa viboko

Kisarawe: Walimu walazwa uchi na kuchapwa viboko

Kisalawe wao wamwjikita katika uchawi Hawataki elimu
 
Kukutana na magumu kama haya ni kawaida,ni moja ya changamoto katika maeneo ya vijijini,mwalimu hutakiwi kuogopa,jamii ya hapo ipewe elimu kuhusu ubaya wa vitendo hivyo.
Kuogopa lazima mkuu.. Kumbuka unapambana na adui ambaye humuoni lakini madhara yake pamoja na aibu vinaonekana.. Mwalimu hawezi kua sawa kisaikoloji hapo. Maafisa elimu wafanye maamuzi magumu ama watafute walimu wazawa wa hicho kijiji warudi kufundisha kwao wataenda sawa.
 
Walimu kueni makini sio kila mwanafunzi ni wakumsemea maneno ya ajabu au kumpiga viboko,matokeo yake ndio hayo mnalazwa na kuchanjwa viwembe.
 
Kumudu kufanya kazi kwenye mazingira magumu kama haya inatosha kutoa motisha,kwani si kila mtu ataweza,wengi watakimbia tu.
 
Wazaramo lini wataachana na haya mambo ya kipuuzi, ndiyo maana hawaendelei..

wazaramo kuhanga kwao ni utamaduni ni sawa na kucheza ngoma.

Aiseee uchawi kumbe Upo nawapa pole sana hao walimu njia Pekee ya kuepukana na uchawi ni maombi.

maombi ni bure, hayana gharama tatizo ni ugumu wa mioyo ya watu.
 
SIAMINI KABISA ETI ISHU YA UCHAWAWI UMEFUNGA MLANGO NAKULOKI WAKAINGIA HAPANA. EITHER NI WAHUNI TUU WANA MASTER KEY NA CHLOROFORM. AMA NI STRESS NA DEPRESSION ZA WALIMU ANGALAU WAMEPATA LIKIZO. LAKINI KUSEMA KUROGWA HAMNAGA IYO MAKITU NI WAHUNI TU WALIWAWINI HAO WALIMU KISAIKOLOJIA
 
Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.

Walimu hao wanakumbana na matukio ya ajabu ikiwamo kujikuta uchi, kupigwa fimbo na mtu asiyeonekana na kulazwa nje ya nyumba zao.

Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kutokana na matukio hayo kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyingine, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.

“Tarehe 26 mwezi wa pili, siku ya Alhamisi sitaisahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa,” alisema Shaaban.

Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipotibiwa kienyeji.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Mbelwa alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa.

Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.

Mzazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.

Mratibu wa Elimu wa Kata ya Marui, Damaru Charles alisema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawasilisha ngazi za juu.

Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa, Aurelia Rwenza alisema tatizo hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika sehemu hiyo.

“Kwa kweli walimu wameathirika, hivi sasa tunatakiwa kuwajenga kisaikolojia,” alisema.


Chanzo: mpekuzihuru
Poleni sana walimu, ombeni uhamisho mtoke huko muachie wazaramo shule yao
 
Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa shule ya msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.

Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyinginge, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.

"Tarehe 26/02/16, siku ya Alhamisi sitasahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa," alisema mwalimu Shaaban.

Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipopata tiba za kiasili ndipo hali yake ilitengamaa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mikidadi Mbelwa naye alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa. Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba yake, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.

Aidha mzazi mmoja mwenye watoto wanaosoma katika shule hiyo, Bi Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.

Mratibu wa Elimu kata ya Marui, Damaru Charles alisema alikuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawakilisha ngazi za juu.
Ofisa Elimu ya msingi wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani, Aurelia Rwenza alisema tukio hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya Elimu.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
 
Back
Top Bottom