Mother Confessor
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 18,684
- 45,613
Hata mm kisamvu hakinichoshi nakipenda saaana,.ni kitam jamanii ukipata na samaki wa kukaanga au firigisi,.doohππMboga niipendayo miaka yote. Kisamvu ugali, kisamvu wali halafu pembeni kuwe na samaki wa kukaanga.
Hahaha Vladimir una wazimu wewe,.utakula kisamvu tuu mimi kunikula ni ndoto mfyuuπππAsante kwa elimu..... Wewe na kisamvu chako..vyote ni Mboga...
Nmewapeenda niwakule
Mbona unakua mchoyo jamaaan, maana kwa haya maelezo ya kisanvu, unaonekana ni mwanamke msafi, unamapaja paja, nyonyo zilizojaa ,sura taaaamu...Hahaha Vladimir una wazimu wewe,.utakula kisamvu tuu mimi kunikula ni ndoto mfyuu[emoji23][emoji23][emoji23]
Nyau wewe wa kijivu,.una nini lakini leo...umefumaniwa eee πππMbona unakua mchoyo jamaaan, maana kwa haya maelezo ya kisanvu, unaonekana ni mwanamke msafi, unamapaja paja, nyonyo zilizojaa ,sura taaaamu...
Naanzaje kutopenda nikukule????khaaaaa embu acha uchoyooo, dunia enyewe ndo IPO mwishon, huo uchoyo wann ????[emoji7] [emoji7]
Unaweza kukichemsha leo ukakipika kesho kwa utuvu..kisamvu kikilala nacho kinautam wake eti,..hahahSafi
Mie huwa nakichemsha
Kikianza kuwiva nakatia kitunguu maji
Naacha vinachemkia
Naweka karoti (box shape)
Naacha kidogo
Naweka nazi ya kwanza
Kisha nazi ya pili
Nachemsha mpaka kikauke...
Nimekimiss Leo nikipike lol
Naww unapenda kisamvuπππ"Baby chuma Kisamvu!"
"Baby chuma Kisamvu!"
"Baby chuma Kisamvu!"
"Haya... Haya.... Waonyesheeee!
"Baby chuma Kisamvu!"
"Baby chuma Kisamvu!"
Q Chilla!
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kukichemsha leo ukakipika kesho kwa utuvu..kisamvu kikilala nacho kinautam wake eti,..hahah
hahahhaaha...kisamvu kiko poa sana...alafu pia kuna kitu kinaitwa mlenda na samaki au nyama ya kukaanga na ugali hapo ndo huwa naona nimekula na nimeshiba...daaahHata mm kisamvu hakinichoshi nakipenda saaana,.ni kitam jamanii ukipata na samaki wa kukaanga au firigisi,.doohππ
Yeeeuuwwwiiii naomba nikakichume aisee uvumilivu umenishindaπ ππKilale halafu kesho ukipike na nundu + wali!!![emoji39][emoji39]
Jamanii jamaniii mate yananchuruzika,na wengine hapa tunavyopenda kula vitu vitamm basii nishawaza hadi kesho itakuwaje hahahhahahhaaha...kisamvu kiko poa sana...alafu pia upate na mlenda na samaki au nyama ya kukaanga...daaah
hahahaahaYeeeuuwwwiiii naomba nikakichume aisee uvumilivu umenishindaπ ππ
ππππ!!Jamanii jamaniii mate yananchuruzika,na wengine hapa tunavyopenda kula vitu vitamm basii nishawaza hadi kesho itakuwaje hahah
πππππππ!!
Mnya mnya mnya [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]but niwie radhi mno... Heading ilinichanganya kidogo nikadhani ni kisamvu kile cha kopo... Kisamvu cha pilau [emoji87][emoji85]Mamboo wapenzi wa mahanjam,mambo matam matam ya jikoni,mambo ya chakula kizuuuri chenye ladha isiyo chosha.....Asalam Alaykhum,.
Leo nataka tujifunze mboga hii jinsi ya kuitengeneza na kuipika,.kisamvu ni moja ya mboga za majani na ni maarufu sana kwa nchi zetu za Africa na hata baadhi ya nchi za ulaya hutumia pia kama mboga ya majani,.YES kisamvu kina utam wake waliowahi kula mboga hii wanaelewa hasa kikiwa kimepikika kwelikweli kikapikika,.aisee ni kitam sanaaa[emoji39][emoji39]
Basi tupike mboga yetu hii ya kisamvu; kwanza utachuma kisamvu chako kitekekiteke (mimi nimekipanda kwangu)utakichambua kwa kutenganisha jani la kisamvu na kikonyo,utaweka kwenye kinu chako kisafi, kisha utamenya kitunguu saumu na utakiweka kwenye kinu pamoja na kisamvu (wengine huweka na tangawizi)japo si lazima sana,.ukitwangia kitunguu saumu kinafanya kisamvu chako kinukie vizuri.
Twanga kisamvu na kitunguu saumu mpaka kilainike sana,tumia kinu kikubwa na kipana kwa sababu kisamvu kikianza kulainika huruka-ruka na kumwagika....kikisha lainika kitoe kwenye kinu kiweke kwenye sufuria pana,weka maji kwenye kinu kisuuze vizuri hayo maji yaweke kwenye sufuria lenye kisamvu chako tayari kwa kuweka jikoni kichemke,.wakati huu unaweza kuchanganya na kunde mbichi vikachemka pamoja,..
Kisamvu chako kikishaiva pamoja na kunde (kama utatumia,sio lazima sana kuweka kunde japo huvutia zaidi)epua hakikisha kimeiva na hakina majimaji mengi(kiwe kimekauka kidogo)weka sufuria nyingine kavu jikoni,ikipata moto weka mafuta ya kupikia kiasi na wakati huu unakuwa umekuna nazi yako iliyokomaa vizuri na kuichuja matui mawili jepesi na zito (tui bubu)au utatumia tui la karanga..
Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji kikaange mpaka kiwe cha rangi ya brown,weka kisamvu chako kikaange pamoja na kitunguu mpaka viingiliane,halafu weka tui lako jepesi acha vichemke kwa dk 5-6 ukiwa umefunika,baada ya hapo punguza moto kidogo halafu weka karoti iliyokatwa katwa vipande vya wastani pamoja na chumvi na pilipili mbuzi kama utapenda,geuza kwa pamoja halafu weka tui zito na uache kichemke taratibu kwa dk 4-5...
Epua kisamvu chako na kitakuwa tayari kwa kuliwa,mboga hii unaweza kula kwa ugali,wali,ndizi,makande na hata chapati ukipenda,.
Mpaka wakati mwingine babaaii[emoji6][emoji6]na weekend njema!!!