Kisa Ubunge, Salim Kikeke adanganya mahali alipozaliwa

Kisa Ubunge, Salim Kikeke adanganya mahali alipozaliwa

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Salim Kikeke ambaye ni mtia ya Ubunge jimbo la Moshi Vijijini imembidi kudangaya mahali alipozaliwa ili kushinda mioyo ya wajumbe. Huko nyuma wakati anahojiwa alisema kazaliwa mkoani Mbeya, hivi juzi akiwa mkoani Kilimanjaro wakati akijinadi akasema kuwa kazaliwa KCMC mkoani Kilimanjaro.
Mimi natoka Tanzania. Nilizaliwa Mbeya, nikakulia Mbeya, nikakulia Arusha, Moshi na Tanga hatimaye kwenda Dar es Salaam.

Nimezaliwa KCMC (Moshi), nimekulia hapa Moshi, nyumba yangu Soweto (Moshi), makazi yangu sasa hivi ni Mabogini (Moshi)

Nafikiri Ustaadhi Salim Kikeke, alizaliwa kiroho Mbeya halafu akazaliwa kimwili KCMC - Moshi. Najaribu kumuelewa tu…

Anyways, kesho ndugu yangu Salim Kikeke anaweza kusema kazaliwa huko Marangu Kiraracha kule kwa Lyatonga Mrema.

NB; Ustaadhi Salim Kikeke kasema ataongeza soko la nguruwe Moshi Vijijini kwa kutafuta soko na viwanda vya uchakataji. 🙆🏾

Hii ahadi nakubaliana nayo kabisa tena nikiona inatoka kwa mtu ambaye ni ‘ustaadhi’ swala tano, Aaah! Kitimoto siyo haramu…

Kitu pekee kinaweza kutupa shida, ni historia ya marehemu. Tutaandika nini? Amezaliwa Mbeya au Moshi-Kilimanjaro?


Mambo ni mengi sana.

 
Wanatuonaga vilaza sana
20250726_104812.jpg
 
Kikeke aachie watu wa moshi watete jimbo lao. Ye nafasi yake ipo serikalini asubiri uteuzi
 
Back
Top Bottom