Kuna mdada Leo kanitafuta, ndo nikakumbuka Mikasa baina yake na mimi, Imepita kama miaka mitatu hivi, Kuna tukio lilitokea nikajiapiza Hawa wake za watu ntakaa nao mbali kabisa katika maisha yangu
Turudi nyuma kidogo, nimekulia mkoa ambao Kuna ubabe ubabe wa kijinga Sana , nakumbuka Kuna siku niliwahi kubananishwa mchana kweupe watu wakanisachi na kuchukua Simu yangu kibabe huku wapita njia wanapita na kuangalia tu, au unapita mahali watu wanakuomba Hela kibabe tu bila sababu yoyote, nikawa nimeweka akilini ntajitahidi katika maisha yangu nipate basic defensive trainings za kujilinda na matukio hapa na pale, miaka hiyo nipo chuo udsm kulikua na gym flani bubu nyuma ya mabibo hostel kule nilikua naenda Kuna mwamba alikua anatufundisha ngumi(boxing).... Ilikua gym flani local tu Ili kulikua na ubabe wa kijinga Sana hata na huko, nakumbuka kuna jamaa alikua anaitwa Thomas mashali alikua anakuja na vijana wake huko basi tu ubabe mwingi ila tukawa tunapiga dojo kibishi tu, nilikuja kuishia katikati maana Hawa kina mashali walikua wakifika ni fujo tu watataka kutumia equipments zote na nafasi yote ya gym wao, nilikuja kuskia aliuawa kimara huko mambo yake ya ubabe Wala sikushangaa, RIP!!!!
Fast forward, Niko mwanza, nilikua na jamaa mmoja tulifahamiana alikua mbabe kweli wa taekwondo, basi ikapita muda nikawa namuomba anifundishe sema nae akawa analeta pozi, siku akaniambia atanipeleka Kwa jamaa yake anifundishe maana mi na ye tumezoeana Sana tizi haliwezi kua serious, basi Kuna siku tukaenda gym Moja mjini kati tukawakuta wale matrainer jamaa alikua anajuana nao akaniunganisha Kwa mmoja tukaongea nae tukapatana nimlipe laki na nusu Kwa mwezi anifundishe taekwondo, ila nje na hapo akaniambia inabidi nilipe elfu 80 kama membership ya gym ya mwezi mmoja ili tutumie facilities za hapo hapo kwao
Ratiba ikaanza vizuri tu kama siku 3 za mwanzo, baada ya hapo mizinguo ndo ikaanza rasmi Sasa, naenda jamaa hanifundishi atanipa nifundishwe na madogo tu, Hali hio ikakaa kama wiki nikaona hapa hamna kitu, nikawa nikitoka kazini napita hapo nafanya weight lifting kama nusu saa then nafanya cardio nikichoka naondoka zangu, nikampotezea jamaa wa taekwondo maana niliona Kila siku analeta uswahili tu
Siku Moja nimetoka kufanya weight lifting nimeenda ule upande wa cardio nikawa naendesha vile vi baiskeli huku naskiza zangu mziki akaja dada mmoja akawa amekaa kwenye baiskeli ya pembeni yangu!! Black beauty, mwili wa mazoezi ngozi Ina nuru kuanzia chini mpaka juu, tukapeana salamu Kila mtu akaendelea na mazoezi.....
After kama dakika 30, nikaona kama mtu ananisemesha nikatoa earpods akawa anacheka ananiambia we kaka baiskeli sio nzuri Sana Kwa mwanaume shauri Yako, nikawa simuelewi namuuliza kwanini akawa anacheka tu ananiambia kaulize tu utapata jibu, nikampotezea baada ya muda nikaondoka zangu......
Usiku wake nimepumzika nikaanza kugoogle kama Kuna shida mwanaume kutumia machine ya baiskeli gym Kwa muda mrefu, basi zikaja opinions mbalimbali Kuna unavyokua unakaa vile inapunguza nguvu za kiume na bla bla kibao, wakawa wanatoa mifano kua hata Hawa professional cyclists wameshatoa Sana tahadhari kua wakimaliza mashindano ya muda mrefu hua wanapata shida Sana kupata msisimko na nini, anyway nikaachana nayo hayo mambo....
Kesho yake same routine namaliza weight lifting nimekaa juu ya baiskeli akaja tena yule dada, alivyofika akawa anacheka ananiambia we kaka jana hujaskia tu, nikamwambia nimeona mahali lakini mi nafanya dakika 40 tu Wala sioni tatizo .... Basi bana mazoea ndo yakawa yameanzia hapo.... Ikawa Kila siku tunakutana huko ni salamu, story kiasi badae Kila mtu anaondoka zake, mpaka kuna siku akanifata akawa analalamika amekua mvivu kufanya mazoezi na nini anahitaji mtu wa ku mpush kuja gym, akaniomba namba nikampa tukaagana Kila mtu akaondoka zake
Mazoea yakatoka Sasa yakahamia kwenye Simu, akawa mtu wa kunipigia, mara tutachat akaanza kunihoji maisha yangu na nini, nikamwambia mi nina mke, na ye pia akaniambia kaolewa!!! At least Sasa tukawa na mipaka kiasi, ila mazoea Sasa nayo yanazidi tu siku nikimwambia siendi gym nae ataniambia hata nae haendi, huyu Binti kitu ambacho nilikua namshangaa Sana alikua anatembelea magari kama manne tofauti, Kila mkikutana gym ni ngumu Sana kukuta katumia usafiri aliokuja nao Jana!!!
Basi mazoea yakaendela ikafika mahali Kila akija utaletewa zawadi iwe juice, snack, ice cream etc.... Siku Moja nikamuuliza mbona unasumbuka Sana Kila siku mpaka upite mahali uniletee kitu ndo akaniambia ana supermarket Kwa hio hua anachukua huko tu, mazoea yakaendea ivo ivo mpaka siku Kuna dogo mmoja nilikua nimezoeana nae kiasi akaniita akaniuliza "bro una ishu gani na huyu Binti mbona siwaelewi" nikamwambia hamna ishu ni mazoea ya kawaida tu hakuna lolote, dogo badae akaniuliza " mme wake unamjua kwani??" Nikamwambia hapana, jamaa akacheka akaniambia kua makini bro mjini hapa utakuja kupotezwa ......
Nikaondoka lakini na maswali kadhaa kichwani, zikapita siku Kuna siku nachat na yule Binti Sasa nikamuuliza kuhusu mme wake, ndo akaanza kufunguka Sasa akawa ananielezea kuhusu mme wake, ni jamaa flani wa makamo tajiri mmoja wa mjini hivi nilikuja kupata kumjua baadae kidogo, Binti anaonekana Bado mdogo Sana ukimlinganisha na jamaa, Binti ndo ananiambia jamaa walikutana Binti akiwa kwenye mashindano ya miss mwanza, jamaa akaanza kumspoil mtoto wa watu, Kila weekend ni kupanda ndege kwenda mikoa na nchi za jirani kula Bata tu, baada ya kama mwaka jamaa akamposa akamuoa Binti wakazaa na watoto wawili, ila akawa analalamika Hana amani kwenye ndoa yake, mara mume wake ana mambo mengi Sana na blah blah kibao( typical women, hakuna mke wa mtu atatoka nje ya ndoa bila kuleta visababu kua mme wake ana matatizo na nini, sijui kwanini hata??)
Basi akaanza kunihoji na mimi nikamwambia tu am happily married sikutaka maongezi mengi Sana upande wangu, siku zinapita huyu Binti nazidi kuzoeana nae, najua kabisa kua I want more, lakini ni mke wa mtu na nilishaonywa hivo nakua makini naona ni heri tu nimpotezee......
Siku Moja sasa kanipigia ananiambia anataka tuongee, sikuenda gym nikawa nimemuelekeza mahali anifate baadae, ikafika muda akapiga Simu akaniambia njoo tuongee kwenye gari siwezi kukaa huko mtu anaweza kuniona, nainuka naenda kwenye gari yake tunaongea kama dakika 10 hakuna la maana analoniambia, baadae akaanza kulalamika anaweza kutokea mtu akajua gari yake, akawasha akaniambia twende sehemu nyingine, kufika mbele akatoka main road akaingia njia za mtaani, kwenda mbali mpaka Kuna mahali ni nje kidogo na makazi ya watu nyumba zipo Moja Moja, nikaingia uoga Sasa namuuliza huku wapi tena , ye yupo calm ananiambia we tulia tu....
Dah nikaanza kuwaza Sasa ukiskia watu wanavyotolewa figo ndo huku Sasa, kwanini huyu mtu ananileta huku kote, nikamwambia hebu simama, akapaki gari pembeni kumetulia hakuna hata nyumba karibu, hapo ni nishaingia uoga nawazia usalama wangu tu, mara akainuka Toka siti ya dreva ananivamia upande wangu, akakaa juu yangu, just like that hata kuniambia chochote hakuna akaanza kunikiss, akili yangu haijakaa sawa tunajikuta tunakiss tu, mara mtu anataka kuanza kutoa nguo ya juu, nikamshika mkono nikamwambia siko comfortable kabisa, kwanza tupo gizani huku Bado Sina hata amani, tukabishana pale nikamwambia tutatafuta siku nyingine Leo hapana kwanza haya mazingira siyaelewi, basi after a while kishingo upande akanirudisha pale aliponikuta akaondoka zake, nikabaki nashangaa tu
Simu Sasa, sms kila mara!!! Akili yangu ikawa kama haiafiki haya mahusiano, siku nikamtafuta yule dogo wa gym nikamuuliza kuhusu mme wa huyu Binti, jamaa ndo ananipa mkanda mzima mme wake ni mafia vibaya mno, jamaa ana reputation mjini, nikawaza hapa naingia Cha kike, it's not too late, hapa niachane na huyu binti mapema Kabisa
Ile gym nikaacha kwenda kabisa, nikaanza kupunguza mazoea, mpaka siku ananipigia ananiuliza Kuna shida gani ikabidi nimwambie wazi tu, una mme na mimi Nina familia yangu tusiharibu miji yetu Kwa tamaa za kimwili, nikwambia siwezi tu, basi akalalamika Sana Kuna voice note akanitumia Whatsapp analia, mi sikuwaza Sana nikaja kumblock kabisa na Ile gym sikuwahi kwenda tena
Fast forward, Imepita kama miezi 6 hapo hatuna mawasiliano kabisa, napigiwa na namba mpya baada ya muda anajitambulisha ni yeye, hapo tulikua tumekaa mahali tu na marafiki weekend tunachangamsha akili, anauliza uko wapi nataka nikuone, mimi hapo nishakula vitu kidogo kichwani nikajiuliza why not? Nikamuelekeza akaja ila gari akaacha car wash ya jirani akawa kaja na boda!!!
Basi tukakaa pale story mbili tatu akawa analalamika simtafuti na nini, baadae nae shetani akanizidi nguvu, nikawaza mtoto kama huyu naogopa nini hasa, nikamwambia naomba nikahamishe, anauliza unanipeleka wapi, namwambia mimi si ndo mwenyeji wako kwani Kuna shida.... Baadae ananiambia sawa hakuna shida, fasta naenda kufanya booking ya chumba maana hapo hapo Kuna hoteli, nampeleka mpaka chumbani,Whatever happened happened, mpaka Mida ya usiku tunaagana Kila mtu anaondoka, Simu Sasa hazikatiki nikawa namuonya kua Kila mtu ana familia tuache kuwasiliana Kila mara
Inapita muda mahusiano yanaendelea hivo hivo Kwa Siri, Kuna siku kaniita mahali Kuna rafiki yake wa kike alikua anafungua lounge, tumekaa pale baadae ndo ananitambulisha Kwa rafiki yake, anamuambia " huyu hapa flani ndo nilikua nakuambiaga kuhusu yeye" mimi Sasa hapo, nabaki nashangaa tu huyu nae vipi, tumekaa pale ndo yakawa mazoea Sasa, tukaanza kukutana Sasa pale lounge Kwa rafiki yake, yeye hata akichelewa akisema yupo pale mume wake ataongea na yule rafiki yake basi inakua sawa
Imepita muda, siku mume wake nae kaja pale, wakawa wamekaa meza tofauti na sisi, mimi nimekaa na yule rafiki yake mwenye lounge pale, mara jamaa katutumia vinywaji, ni jamaa mtu mzima kidogo, dah namuangalia roho inanisuta naona hapa nakosea kabisa yaani kama mwanaume, ingekua ndo mimi ndo nafanyiwa ivo, anyway mapenzi kikohozi tunaendelea ivo ivo mpaka nakuja kupata safari kikazi, tunaagana poa tu mi naondoka zangu tukawa tunawasiliana mara moja Moja Whatsapp kipindi npo mbali, mpaka ikafika siku tu akakata mawasiliano, wahtsapp wala ñormal calls simpati, sijui kwanini na mi Kila siku nikawa namtafuta sema bila mafanikio, basi nikaja kuzoea nikampotezea mpaka nikaja kurudi, Bado simpati hapo na mi Kuna muda inatokea namuwaza tu sijui kwanini, ikapita muda siku naenda Sasa pale lounge maana yule dada sikua na mawasiliano nae hata, nafika tumekaa pale ndo namuuliza flani yupo mbona simpati kabisa kwenye Simu, yule dada ananiangalia kama Kwa huruma kwanza kisha ananiuliza kwani huna taarifa? Namuuliza nini kwani
Ndo anaanza kunipa mkasa mzima, ananiambia dogo una bahati Sana sijui hata mume wake angejua angekufanya nini yaani, namuuliza kwanini? Aisee ndo ananiambia Kuna siku wamegombana mdada wa watu kafungasha vitu kaondoka, jamaa karudi ameshalewa anauliza mke wake yupo wapi wanasema kaondoka hawajui yupo wapi, anayemjibu ni mdogo wake wa kiume na huyo dada Sasa alikua kamaliza form 4 anaishi hapo Kwa shemeji yake, jamaa akamuambia dogo we na dada Yako mnajuana lazima uniambie yupo wapi, kama utani jamaa kaanza kumshushia dogo kipigo, kipigo kipigo mpaka dogo uhai ukamtoka kiutani utani, jamaa ndo akawa kamuua shemeji yake hivo(allegedly)......
Jamaa kawekwa ndani, bidada akarudi wakazika mdogo wake baada ya hapo wakatalakiana bidada kachukua watoto kahama Jiji Moja Kwa Moja na watoto wake, aisee nikachoka kwanza, maswali mengi nikajiuliza huyu jamaa kama ndo mimi angenikuta ingekuaje!!!! Nikaona nilikua nacheza na kifo
Fast forward, jamaa alikaa ndani kama mwaka kesi sijui ikaendeshwa vipi akarudi uraiani..... Kuanzia hapo nikajiapiza mke wa mtu is a no go zone!!! Siwezi kurudia tena maisha yangu yote