Kisa kamili cha mapenzi ushauri unahitajika

krava

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
225
287
Mwanaume alimzalisha akiwa form two akaishi nae kiunyumba miezi 6 bila Mimi kujua (alinificha) Mimi nikabeba mzigo nikauzalisha nikaishi nao miaka mitano nimeambiwa na wengine kwamba aliishi na mwanaume miezi sita kabla ya Mimi kuishi nae miaka mitano nikamfukuza sasa ameomba msamaha anataka kurudi nimkubali au nimwache maana ana watoto wawili kwangu na kwa mtangulizi wangu nimuache au nioe nijibuni haraka nataka kufanya maamuzi
 
Tukujibu haraka...!!!!??

mbona wewe umeshindwa kujijibu haraka?

Halafu kuna baadhi ya wanaume mnashangaza kwa hiyo kama aliishi nae miezi sita na wewe umeishi nae miaka mitano nani kamzeesha huyo dada wa miezi sita au miaka mitano? aliyemzalisha mtoto mmoja au wewe uliyemzelisha wawili?

Huyo dada kakosea kukuficha kuwa tayari ana mtoto, ndio kosa lake. Ila hilo na kuishi na mtu sio suala ya kukufanya umfukuze. Na kama kaomba msamaha msamehe.

Na baadhi ya wanawake aisee ni bora kuwa wakweli tunapoanzisha mahusiano mapya. Na tujifunze sio kila mwanaume ni wa kumbebea ujauzito
 
Brother kama kosa ni hilo la kukuficha kuwq aliishi na mwanaume mwingine miezi 5. Msamehee mchukue muishi mkuu.

Ishu kama anamakando kando tofauti na hilo kosa jaribu kufikiria.
Ila kama yupo vizuri ishu ni hiyo miezi 5 jaribu kukaa naye muyajenge.

BTW, Kisheria huyo ni mkeo hupaswi kumfukuza fukuza kama mbwa. Akienda kwenye mamlaka za kudai haki miaka 5 ni mingi saana mzee.
 
Kisheria huyo ni mke wako mkuu. Achana na mawazo mgando ya kutaka kumuacha. Jenga naye familia unataka kuanza upya ikifika miaka mitatu au mitano naye unagundua alikuwa anaishi na mwanaume kwa miaka 3 kipindi anasoma utamuacha tena? Hiyo ndo ndoa yako halali, ongea naye mwambie unampenda sana na aache mambo ya kukuficha ficha linapokuja suala zima la maisha. Sentensi ya mwisho sijaipenda "nijibuni haraka nataka kufanya maamuzi". Hii inakuonyesha wewe ulivyo...badilika mkuu.
 
Like...

mkuu tuwaonee huruma dadaz jamani , umemfunua miaka yote hiyo, yani unamjua ndani njee then unataka ushauri na tiale ana watoto hao , jamani, haya maharage ya wapi tunayokula mpaka wakina dada wanaonekana kama dude la kufutia miguu mlangoni, nyie ndo mnalishwaga libwata na wale wanawake wanaojua kuwashika vicha wanaume , , hata akikugeuza msukule Mungu ataelewa tuuu

√√ Jaaribu kua Hard reset Brain yako ukumbuke zile Beautiful momemt ndo utapata ushauri wa haraka nyie ndo huwa baadaye unapeleka ngoko zako unadai unataka mtoto wakoo
 
Mwanaume alimzalisha akiwa form two akaishi nae kiunyumba miezi 6 bila Mimi kujua (alinificha) Mimi nikabeba mzigo nikauzalisha nikaishi nao miaka mitano nimeambiwa na wengine kwamba aliishi na mwanaume miezi sita kabla ya Mimi kuishi nae miaka mitano nikamfukuza sasa ameomba msamaha anataka kurudi nimkubali au nimwache maana ana watoto wawili kwangu na kwa mtangulizi wangu nimuache au nioe nijibuni haraka nataka kufanya maamuzi
Nadhani issue ni upendo. Mmekua pamoja kwa miaka mitano. Je, imekua ni miaka ya furaha na amani? Upendo, kujituma, kujitoa sadaka? Je, mmefunga ndoa? Dhehebu gani? Ushauri wangu mchukue mke wako. Vijana wengi sana wa kike wanalaghaiwa na wanaume. Wanabaki wameumizwa sana. Hivyo wengi sana walikosea kabla hawajawapata hao walio nao. Ila lazima ujiridhishe katika nafsi yako. Watoto waweza kuwa sababu ya kumrudisha but that should not be the essence. The essence of every marriage is love. Hivyo hakikisha na wewe unapona hilo jeraha ili ukimrudisha umpe pia upendo wote kama mwanzo. Swali la kujiuliza ni kwamba, usingegundua, ungemfukuza? Kumbe kuna mambo mengi tuu hatuyajui. Najua inaumiza na maumivu haya huongezwa na kiburi cha uanaume. Kwamba mimi ni dume, inakuwaje anifanyie hivi? Kumbe pamoja na udume wetu, tuu wadhaifu sana. Watu makini tuu ndio wanaweza kutambua udhaifu wao. Kama ni Mkristi, samehe saba mara sabini, yaani infinitely. Kama wewe nk Mkristo na umefunga ndoa, bado utafungwa na kifungo cha ndoa. Kama hujafunga ndoa, huoni pia kwamba humpendi? Basi, jaribu kutafakari kwa ndani na ujihakikishie kua kweli umemsamehe. Huyo mtoto ambaye sii wako nadhani huhusiki sana. Ila asikutie uchungu sana. Tuko hapa duniani na kila mtu hupitia njia yake. Sii kila mtu ataoa bikira na sii kila mwanamwali anauwezo wa kuwa mke mzuri. Pia sii kila aliyekosea kabla ya kuolewa kwamba hawezi kuwa mke mzuri. Wanasaikolojia wanasema kuwa, wale wanaojikuta wameingia ktka mahusiano ya kimapenzi mapema are very loving pple. They are full of love and they wish to have a commitment as early as possible. Bahati mbaya huangukia mikono isiyo salama na matokeo yake ndio hayo. Hivyo njia yako ndio hiyo uliyoianza. Usilazimishe na wewe kuwa kama fulani aliyeoa mwanamwali. Huyu wako hujui atakuokoa wapi. Mchukue na umpende zaidi. Nikupe tahadhari. Hakikisha umeweza kusamehe na kukubaliana na hali halisi. Thats it is. Historia haitajiandika kivingine. Usijidharau. Hakuweza kukuambia na wachache sana huweza kusema wenyewe bila kuulizwa. Na huenda na wewe hukuuliza pia. Hivyo sii kwamba ulidanganywa, bali ujasiri ulikosekana. Hivyo sasa umejua, pokea. Tahadhari ni kwmba, epuka kulipiza kisasi. Wanaume wengi walipogundua hali za wake zao zinazofananafanana na yako, au waliwatesa wake zao au walipata kisingizio cha wao kuanza kutoka nje ya ndoa na matokeo yake wamekufa kwa ukimwi. Hivyo, umrudishapo, samehe na achilia yote. Hata kama utamwacha huyu wa sasa, una uhakika gani na huyo utakayemtafuta? Afadhali ni ipi: Aliyetoa mimba sita halafu anakuambia hana mtoto au aliyekubali majukumu ya malezi? Je, afadhali ni ipi?: Anayetumia vidhibiti mimba lakini ametembea na wanaume kumi au aliyeumizwa na labda na mwanaume mmoja? Hamna formula hapo. Ni busara na upole utakuokoa. Ila Mungu yupo kama unamwamini. Msikilize pia
 
Yaani wewe ni zaidi ya shetani,yaani uishi naye miaka 5 na kumzalisha juu watoto wawili alafu unataka kumuacha Kwa kikosa cha kipuuzi kabsa!haukumbuki mema ya miaka 5 aliyokufanyia?kukupikia,kukufulia na kuwatunza wanao!?futa kabisa wazo LA kumuacha kama unajielewa na kujitambua!
 
Muoe tu dada wa watu muendelee kulea watoto. Ukimuacha utacomplicate tu mambo.
 
acha ujinga lea watoto hao utatusababishia panya road mtoto wa mkeo ni mtoto wako pia damu moja na wana wako
ndugu wanaokutana kwa mama wanapendana zaidi ya wanaokutana kwa baba
miaka 5 kisheria huyo ni mkeo, halafu unataka kumuacha ataanzia wapi na watoto hao watatu?? unafikiria kupitia wapi braza??
kama unaona unachofanya ni sahihi basi upo sahihi
 
Watu wengi siku hizi wanaoa tu ili wapate uhakika wa mzigo kila watakapo ....Lakini hawajui thamani ya wenza wao kabisa...
 
Back
Top Bottom