SoC01 Kisa cha Samaki na chambo

Stories of Change - 2021 Competition

Brother du

New Member
Jul 8, 2020
4
2
Habari za uzima ndugu zangu wana JF.

Hii ni story ya ukweli kabisa, na ilinifunza kitu flani kwenye maisha.

Sasa sio mbaya kama tutajifunza wote kupitia story hii.

Katika jaribio la utafiti, nilimshika samaki kambale kwenye mto flani pale Kigoma, samaki huyo niliondoka naye nyumbani akiwa mzima kabisa.

Nilichokifanya nikachukua beseni kubwa, nikaweka maji ya baridi mengi tu. Ilikuwa asubuhi, ilipofika jioni, nikaenda kutafuta chambo(vyambo vingi) nakarudi navyo nyumbani, nilipofika nikavitumbikiza kwenye lile beseni la maji, dakika moja nyingi, yule kambale akavila vyote.

Asubuhi yake nikaenda kumuangalia yule samaki kwenye beseni, nikakuta kama ameanza kuchoka choka,nikajua ni sababu hajazoea kukaa kwenye maji madogo, nikamla.

Sijaishia hapo. Baada kama ya wiki mbili hivi kupita, nikaenda tena mtoni, nikamnasa samaki mwengine aina hile hile ya kambare.

Nikachukua beseni, maji mengi kama kawaida,ila safari hii ya pili nikachukua na kioo ambcho kipo transparent kiadi kwamba ukiwa upande mmoja unaona upande wa pili bila tatizo(clearly)

Sasa basi, yule samani nikamuweka kwenye baseni,full maji, katikati nikawka kile kioo. Yaani baeseni nililigawa mara mbili. Upande huu wa samaki nikaweka vyambo, dakika moja nyingi yule samaki akavila vyote.

Baadae nikaweka vyambo pande zote mbili. Vya upande wa samaki vikaliwa vyote, sasa bwana yule samaki akawa anataka ale na vile vyambo vya upande wa pile,si akawa anakutana na kile kikwazo cha kioo,

Samaki aliteseka sana,maana vyambo vilikuwa vinachezacheza,anavimezea mate tu,aligonga kwenye kioo kwa mda mrefu sana bila mafanikiyo.

Mwisho wa siku yule samaki alikata tamaa,akaacha kabisa kusogelea kweny kile kioo. Nilichokifanya nikaweka chambo kimoja tu upande wa samaki, fasta kikaliwa, nikawa kama nimemkumbusha tena akaanza kutamani kwenda kula vile vyambo vya upande wa pili. Akafeli. Tena akaacha kabisa kwenda kusogelea kwenye kioo.

Kisha nikaondoa kile kizuizi. Lakini kambare hakuenda kushambuliya vile vyambo.

Kambare alifundishwa kwamba kizuizi kilikuwepo kati yake na vyambo. Vile vyambo vilianza kuchezacheza kwenye maji tena karibia na yule samaki bila kushambuliwa.


SOMO: Wengi wetu, baada ya kupata shida na kutofaulu, hukata tamaa na kuacha kujaribu.

Kama Samaki kambare katika historia, tunaamini kwamba kwa sababu tulishindwa zamani, tutashindwa kila wakati.

Kwa maneno mengine, tunaendelea kuona kikwazo vichwani mwetu, ingawa hakuna kizuizi "halisi" kilichopo kati ya mahali tulipo na tunakotaka kwenda.

Tusikate tamaa na kushindwa kujaribu tena.
Ahsanteni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom