....Ninakusihi usiendelee kubandika simulizi lako hilo kwani linanikumbusha machungu ambayo nimeyapitia na limeshazua mtafafuru kati yangu na baadhi ya marafiki ambao walikuwa wanajua undani wa kilichotokea kati yangu na mke wangu. Kilichotokea "Jumamosi" hakifai kusimuliwa wala kujulikana kwani ni ndiyo nimefanya makosa na nimeyalipia mara mia moja na pamoja na hayo tuliamua kuendelea kuwa pamoja.
Kukisoma kisa chako hadi kilipofikia kimeshatonesha madonda mengi na kurudisha kumbukumbu ya matukio ambayo tulishaamua kuyaacha yapite. Chonde, tafadhali mwanakijiji pamoja na kutumia mbinu zote za kiuandishi kuwaficha wasomaji wako watu wanaofahamu kisa chetu watagundua mapema kabisa kuwa ni nani anazungumziwa.
Naomba usimalizie hicho kisa na niko tayari kuzungumza nawe kwa herufi kubwa ili tuweze kuyamaliza kiutuzima. Tayari nimeshaabika siko tayari kuabika tena hasa kama magazeti ya udaku yatakipata kisa chako. ....