Kisa cha Mimi kugombea demu na Jini

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,467
23,745
Hili jambo sikuwa napenda sana kuwahadithia wadau. Lakini leo naona niwape kisa hiki kilichonipata miaka ya 2000s.

Mimi nimekulia Sinza kivulini kwa miaka yangu yote na washkaji kibao ambao wengi walienda Usa na South Afrika. Bongo tulibaki wachache sana ktk group letu. Akina Mandawe na Jitu Utu. Lakini Bozo, King Mayor, Lusugwa na Kaya Man walikuwa na ndoto za kuishi ughaibuni kitambo sana.

Nakumbuka siku hiyo nlienda mtembelea mshkaji maeneo ya Tabata Mawenzi. Tulikuwa ma braza men sana nlienda na Toyota Mark 2
ndo zinatamba.

Nlipofika nikakumbuka kuwa nlikuwa nmeishiwa deodorant then kwa jamaa kuna joto sana. Nikapark gari mitaa flani kabla ya kufika Mawenzi.nikashuka nikavuka upande wa kulia kulikuwa na duka la vipodozi limechangamka sana. Yaani vitu vingi.

Nikaenda dukani. Kumwangalia muuzaji...dada mmoja mzuri kinyama.ila umri alikuwa anaonekana amenizidi kidogo.pembeni yake yupo msaidizi.

Yule dada alinivutia sana.kiumri alikuwa amenizidi kidogo ila alikuwa anaonekana mzuri zaidi then ana body nzuri kama kuna uarabu kwa mbali.mweupe na urefu wa wastani.

Nlipoteza muda pale nikajikuta nimenunua Nivea Deodorant,Body Spray, nikanunua na perfume, mkanda wa kiuno na mafuta ya nywele. Vitu hivyo vingine sikupanga hata kununua. Nilinunua na miwani ya jua.

Nikamwambia kuna perfume flani nahitaji. Nlijua hana sema nlikuwa natafuta namna ya kupata namba yake ya simu. Nikamtajia akanambia akienda Town atanitafutia.nlimweleza mimi si mwenyeji Tabata so tupeane number za simu akienda kuchukua mzigo akipata anijulishe but pia kama atapata mambo mengine mazuri anijulishe.

Nikaondoka. Siku nzima nlijikuta namfikiria yeye tu. Kila nikikaa namwona huyu hapa. Kesho yake nikamsalimia kwa simu baada ya week akanambia kuna mzigo ameleta. Nilimfuata tena. This time nlitumia kama 170,000 kununua mazaga zaga kwake.

Week ya pili nikaanza funguka.yule dada aligoma.akanambia hapana ana mtu.nlimsisitizia sana.nikawa naenda nampa zawadi ,sometimes tunatoka ile jioni. Nikawa sielewi anasema ana mtu but mbona yupo free sana.

Mi nliendelea kupush ili nile mzigo. Mwishoni sana akakubali tuwe wapenzi. Nakumbuka siku ya kwanza nmeenda naye lodge mashine iligoma kabisa kucharge. Tulihangaika sana. Mashine haipati moto. Nikahisi labda mshtuko. Basi tukaishia kupiga love stories tu. Tukaagana nikiwa na fedheha sana. Yeye hakuonesha kusikitika au kushtuka.

Ile nmerudi home kumfikiria tu mashine imejaa charge kinoma. Usiku nmelala siku hiyo nikaota jamaa mmoja kaja ananipiga beat nmemchukulia mke wake. Tuligombana na jamaa kwa maneno sana. Asubuhi nikaamka nmechoka sana.

Ikapita. Usiku nikaota tena ndoto kama ile. Sikujali nlijua ni mawazo tu.

Mara ya pili nikaomba tena game. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Ijumaa nikapita mitaa flani kwa wana wangu walikuwa wamepika kitimoto. Sisi tulikuwa hatuna dini kwa kweli. Tuligonga na ugali nikashiba sana.nikapiga na Malta Guiness nikaelejea tbt kumchukua mrembo.

Miaka hiyo hapa Makaburini kuna Lodge inaitwa Kilimanjaro ilikuwa bado mpya kabisa (kwa sasa nadhani imechoka) basi naelekea Tabata, mashine ipo juu ile mbaya yaani full charged aisee. Nikasema leo ntamchapa nao huyu dada kinyama, yaani ntamchapa sana.

Nilifika nikamchukua kurudi naye Kilimanjaro maana room yangu ilikuwa ghorofa ya pili nliipenda coz ilikuwa na bath tub so sometimes tunacheza kwenye maji.

Nikaingia naye room....

Inaendelea chini kwenye posts nyingine.
 
Nikaingia naye room. Pale chini pana bar pia na kwa kuwa mimi nlikuwa nmepita kwa washkaji tukala ugali na kitimoto asubuhi tu ile nikawa sina sababu ya kula sana. Nakumbuka nliagiza mchemsho wa kuku na chapati naye hivyo nikaagiza na grand malt mbili tukala tukanywa tukawa tumejilaza kitandani tunaangalia movie kwenye laptop.

Ktk mashine ilikuwa imesimama vizuri kabisa. Bila shida na demu ni kama alishangaa kwa mashine kusimama kama kawaida.tofauti na siku ile ya kwanza hakuonesha kushtuka.nikamla.tofauti na nlivyotegemea. Alikuwa hana utamu. Alikuwa wa baridi tu.

Nlichukua muda sana kumaliza.yeye wala hana hisia za kitendo. Nlihangaika sana kumweka sawa.sikufanikiwa. akawa tu amepoa. Tulifanya mara tatu tu tena kwa shingo upande maana last time was like nambaka. She wasnt ready kabisa.mkavu analalamika kuumia. Pamoja na kumwandaa kote hamna kitu.

Baadaye tukawa tunatoka nikamrudisha mpaka kwake. Dukani nikarudi zangu home.

Mida ya saa 2 nlianza sikia baridi kali sana ila natokwa jasho.sikuelewa mpaka saa nne nakumbuka baada ya kuangalia tamthiliya flani (kama sikosei ilikuwa days of our lives au the young and the restless ) nikaenda kulala.

Saa saba usiku nikiwa kama nipo usingizini kama nipo macho. Nikaona nageuzwa kitandani.but ni kama naota au naona live. Nlichapwa viboko sana.sana huku damu ikitoka mgongoni.nlilia sana lakini kila napojaribu kuamka nashindwa.nikijaribu kupiga kelele sauti haitoki.ila nalia sana bila kutoa sauti.

Kesho nliamka mwili unaniuma sana na mgongoni ni kama nina majeraha yanayopona.maumivu nayasikia.sikuweza mwambia mtu ni nini kilitokea.

Nikampigia simu yule dada kumsalimu.hakupokea. nliendelea kupiga simi kila baada ya muda haikupokelewa. Mpaka usiku simu haipokelewi.

Keshokutwa yake nikaenda tabata dukani.nikamkuta yule dada msaidizi kumuuliza boss wake yu wapi akajibu toka amerudi juzi alikuwa anajisikia vibaya amepumzika.sikuoneshwa nyumbani kwa yule dada. So sikuweza enda.

Siku ya tatu napiga simu haipokelewi.nikaacha. siku ya 5 nikapiga simu kwa namba ya mdogo wangu. Akapokea nikamwambia ni mimi akakata simu.

Baada ya week na nusu toka tumefanya mapenzi akanipigia simu kuwa nipange tuonane sehemu ambayo ni ya wazi isiyo bar. Nlihangaika sana nikaja pata sehemu moja hapa Sinza.akasema atakuja mwenyewe.

Nlimtajia muda then nikawahi nikaenda subiri sehemu ili nimwone anakuja na nani. Kweli hiyo mida akapiga simu nikamwelekeza akafika.mimi nmepark gari mbali kidogo namcheck. Alikuja na gari peke yake. Akaingia nami baada ya muda akanifuata.

Ndani tumekaa mdada hakuwa na furaha.amevaa nguo ndefu sana na miwani mikubwa myeusi.tukaongea mambo kadhaa.kisha ndo tukarudi kwenye jambo la msingi.nilimweleza kilichonipata hakushtuka.nlishindwa mwelewa.mimi nlimweleza nikijua ni ushirikina maana kuna mama mmoja kitaa walikuwa wanasema ni mchawi.mtu wa kigoma.but nlishangaa why that night.na home sikumwambia mtu yeyote.

Bi dada akaanza nisimulia maisha yake yalivyo.katika hali ambayo alikuwa anaonesha ameachoka na hana furaha kabisa. Akaamua sasa aniweke wazi ni nini hasa ambacho kinaendelea katika maisha yake. This day hakuwa mwenye nuru.weupe wake ulikuwa umepungua, usoni ni kama mtu aliyechoka pengine hakulala week nzima.

Anasema shida ilianzia Zanzibar...


Ntaendelea na kisa wadau naingia barabarani kurudi home.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom