Kisa cha Mimi kugombea demu na Jini

Injili ya Gheto

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
1,997
2,000
Baada ya kupewa masharti ya kutokunywa pombe na kufanya mapenzi kabla ya ndoa anasema alishtuka sana!

Maana mrembo huyo alikuwa mpenzi wa Amarula sana tu.Alikuwa anapenda kunywa amarula akiwa kwenye mapumziko yake,hasa nyakati za jioni pia kusikiliza nyimbo za Kicongo.Na alikuwa anapenda sana nyimbo za Koffi Olomide.Wimbo wake kipenzi ulikuwa Kisanola.

Kuhusu sharti la pili nalo ilikuwa mtihani mkubwa sana kwake.Kwa sababu kwa umri wake ule wa miaka 23 alikuwa tayari keshafahamu mapenzi na anaijua raha ya sex.Alikuwa hawezi kukaa mwezi pasi kupanda Boat kwenda Dar kwa mpenzi wake kukaza bolt na alikuwa na matumaini kuwa wangeyajenga na mpenziwe ili arudi Dar weekend kufanya lolote ili wayajenge.
Alilia sana.Ila akaondoka kurudi home,alipiga moyo konde na kujisema kuwa Mungu atamvusha.Sio siri akisimama kujitazama na chain yake ya gold alizidi kuvutia.Alitamani kuivua ila akikumbuka yule mzee alivomla tigo alishindwa.Ghafla akapitiwa na usingizi bila kula wala kuoga.
Anasimulia kuwa alipolala aliona ametokea kwenye sauna moja nzuri sana.Maji ya moto matamu na harufu ya manukato mazuri ilimpa faraja na furaha ya ajabu.Anasema ghafla wakatokea mabinti wawili na matray mawili.Moja lina sabuni ya maji lingine lina taulo safi laini sana hajawahi kuona popote pale duniani.
Kwa matabasamu mazito na bashasha walimtoa kwenye sauna mfano wa mtoto mchanga kwa kumuita jina lake halisi.'Usiogope binti karibu sana', anasema hakustuka sana kwa sababu alishaanza kuzoea viroja.Mmojawao alikuwa na asili ya kichina na mwingine kiarabu.Anasema alipelekwa kwenye bafu akaogeshwa kwa muda mrefu huku wakimsifia kwa urembo wake.Anasema alipigwa na bumbuwazi ghafla baada ya kuletewa sahani iliojaa chakula baada ya kuogeshwa.Nywele zake nzuri natural za kishombe shombe zilipakwa mafuta na kukaushwa kwa mashine anasema kama za salon ila nzuri sana.
Baada ya kula akapelekwa chumba cha masaji.Akalala kifudifudi na kuanza kufanyiwa masaji ambayo hajawahi kupata.Anasema alijisikia raha mnoo.
Ghafla mabinti wakatoweka na 'bwana mkubwa akatokea'.Hili lilikuwa lile jini mlinzi alilopewa na ustaadh.
Anasema alikuwa kafanana sana na mugizaji fulani wa movie za kihindi mtoto wa Bacchani jina alisahau.
Anasema akaona kama mbwai na iwe mbwai akataka kukimbia.Jamaa akamshika bega lwa upendo akawa kama anaishiwa nguvu na kujiskia hali fulani ya usingizi.Akamwambia asiogope hatomdhuru,atamlinda na kumpenda.

Alichohitaji ni uamnifu na usafi.Kuanzia siku hiyo atamtreat kama mmewe halali mpaka pale atakapo olewa.Jamaa alikuwa handsome sana,Kifua cha mazoezi na surwali ya lineni.Marashi yake yalikuwa mazuri sana.Binti akajikuta anamlalia kifuani na kulia kwa kugugumia.Ghalfa akajikuta kalala kitanda cha sita kwa sita akiwa mtupu.Anasema hakuwa na hiyana.Jamaa alimwandaa kisawa sawa akampa mapenzi matamu mnoo.Baada ya mbilinge nzito liliolopelekea mashuka ya satin kuchomoka akapitiwa na usingizi.


Akaamka saa sita mchana.Alistuka sana akaoga haraka haraka na kwenda kazini.Kuhusu kukuta ute,hilo usiulize makofi polisi.Ila alijikuta kavaa pete nzuri ya uchumba yenye kidani cha rangi ya dhambarau.

Kwa mshangao alipofika kazini meneja hakumuuliza kwanini kachelewa zaidi ya kujichekesha tu.Wenzie wote walimshangaa kwa upekee aliokuwa nao siku ile yani alikuwa na mvuto fulani amazing.Mmoja wapo alimtania kuwa siku ile alifanana na Priyanka Chopra kabisa,yule miss world wa India.Anasema alicheka sana.Alijiskia mwepesi mno na mwenye amani.

Rafiki yake aliyempeleka kwa Ostadh alipotaka kujua kinachojiri anasema hakutaka kuzungumzia kabisa.Anasema muda ulimbia mno.
Akarudi home.Akakuta sofa jipya,jiko jipya kila kitu kipya ndani.Alistuka mno nusu azirai.Ghafla simu yake ya kiganjani ikaita.Akaitazama na Neno 'La azizi' lilitokea akasema hakupokea ila simu ikaendelea kuita kama mara 3.Ghafla sms ikaingia.
Alipoifungua ilisema," La azizi ahsante kwa mahaba ya jana.Nimekupa zawadi ndogo sana,utainjoy yaani". Japo mwisho alinalizia kimasihara kama kigogo wa Tweeter anasema alijiskia raha saana.Sababu ndani kulipendeza mno.
Kuanzia hapo ikawa kama kaposwa rasmi.Akifungua wallet anakuta pesa.Akilala tu ni gemu kali matata sana.Akiamka usafi ushafanywa n.k
Baada ya mabadiliko yale makubwa kwenye maisha yake anasema alinawiri sana na kuikubali hali yale.Alipendeza mno kiasi kwamba usumbufu kwa wanaume ukazidi maradufu.

Itaendelea....
Mkuu leta mambo watu tukate kiu maana kama ni kubembeleza tumembembeleza sana

Shusha vitu watu tukate kiu
 

Mjamaa1

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
5,210
2,000
Wadau jambo la kushangaza sana leo asubuhi yule dada amenipigia simu. Ni miaka zaidi ya 8 sikuwahi wasiliana naye.leo amepiga simu asubuhi hii kunisalimia. Anasema amenikumbuka sana. Namuuliza upo wapi hajataka kujibu.

nimeshangaa sababu tulipotezana kitambo sana kwa mawasiliano.mimi namba ninayotumia sikuwahi badilisha kwa zaidi ya miaka 15 yeye alipotea tu hewani akawa hapatikani.leo ndo amenipigia. Sikumtambua mpaka alipokutambulisha. Nmeshindwa elewa imekuaje.

Tayali
 

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
3,781
2,000
Napenda watu wanaomalizia story pongezi na hongera kwake [mention]Phoinix [/mention] maana watu wanasimulia kisha wanaleta pozi, kuhamishwa kwa uzi kuna athari gani kwa mfano?
 

BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
1,402
2,000
Ameona mambo yasiwe mengi akapokea kijiti, iliwahi kutokea kwenye stori nyingine pia, mwenye uzi wake alianza kuleta madoido jamaa akaamua kuumalizia na mambo yakawa fresh
Kwahiyo acha tu jamaa atuondolee arosto
Iko hivi..kuna kundi la whatsup huko huyu kichaa mwenye maarifa hii habari ameisimulia na kuimaliza..hivyo huyu mdau naona yuko huko pia..hivyo amecheza fair.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom