Kisa cha Mfalme wa Nyika Simba Kibogoyo

Kisa cha Mfalme wa Nyika Simba Kibogoyo

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
14,557
Reaction score
31,968
KISA CHA MFALME SIMBA KIBOGOYO

Miaka fulani huko Porini kulikuwa na Utaratibu wa Wanyama kubadilishana madaraka. Kila baada ya majira fulan wanyama walikusanyika na kuchagua Mfalme. Huu ulikuwa ni utaratibu waliojiwekea wanyama hao kwa nia ya kubadilishana madaraka.

Wanyama hawa kabla ya kuwa na utawala wao walikuwa wakitawaliwa na binadamu kwa miaka mingi sana. Waliamua kufanya harakati za kumwondoa Binadamu na hatimaye walifanikiwa kumuondoa binadamu. Hivyo wakaamua Tembo ndo awe mfalme wao huko porini. Walimwona Tembo ni mpole na pia alikuwa ni mkubwa sana ukilinganisha na wao.

Pia jambo la faraja Tembo alikuwa na uwezo wa kuwakemea wanyama wote wanaokula nyasi,nyama na hata vijidudu/wadudu. Tembo alitawala kwa miaka kadhaa ni kweli yeye hakuwa akila wanyama wenzie ingawa kuna kipindi ilitokea bahati mbaya aliwalalia wanyama wengine wakiwa kwenye mapumziko yao bila yeye kujua wakafa.

Na kuna wakati aliwalalia kusudi kuwaadhibu pale walipokuwa wanaenda kinyume naye. Lakini alikuja tu kusema ilikuwa bahati mbaya hakuwaona. Ilitokea mara chache sana lakini Wanyama wengine bado waliendelea kumheshimu na kumpenda kwa sababu siku zilivyozidi kwenda alizid kuonesha busara na hekima. Muda wake ukaisha yakaja majira mengine.

Tembo akapendekeza apewe Nguruwe utawala. Ikaonekana Nguruwe pia hakuwa tatizo ikizingatiwa Nguruwe alikuwa ameoa Nyani hivyo ikaonekana watasaidiana vizur tu kwnye Utawala.

Walitawala na ikatokea kuwa Nguruwe yeye hakuwa akila nyama za wanyawa wenzie lakini pia hakuwa mkali kwa wanyama waliokuwa wakiwaonea wanyama wadogo na kuwala.Na ikabainika naye baadaye alikuwa akila Wanyawa wadogo wadogo pamoja na kujinadi kuwa yeye hula majani.

Mkewe Nyani akawa akila sana wanyama kwa siri na ikawa ni tatizo kule Porini. Majira yakaenda baadaye ikaonekana kuwe na Jamii mbalimbali za Wanyama walete wagombea wao wagombee Ufalme. Jamii ya Wanyama wala nyama wakashinda kwa kuwa walikuwa na nguvu na waliogopwa sana. Basi Chui akawa Mfalme. Alianza kwa ukali dhidi ya wanyama wenzie ambao wanakula nyama akiwaasa waache kula wanyama wenzao.

Siku zilivyozidi kwenda Chui uchu wa kula nyama ukamjaa akaanza kula wanyama wenzie waziwazi kabisa. Kukawa na malamiko mengi porini. Muda wake ukaisha.baadaye ukafika wakati wa uchaguzi Fisi akajitokeza kugombea ufalme. Wanyama wengi wakampenda Chui kwa kuwa yeye wakati mwingi alikuwa akicheka. Hasa ukifika usiku akisikia kuna sherehe Fisi alipenda kucheka kwa sauti sana.

Wanyama pia walivyomuona akitembea kinyonge na kucheka na umbo lake hawakuona kama atakuwa Kikwazo kwao.zikapigwa Kampeni Fisi akachaguliwa kuwa Mfalme. Siku zote Fisi alikuwa akizunguka pori zima akisema anatafuta malisho mema kwa ajili ya wanyama wote n.k kumbe alikuwa akitafuta mizoga na akawa akishirikiana na wanyama kama mbwa mwitu,chui n.k wakiua na kula wanyama wengine wanaokula nyasi.

Tofaut yake ilikuwa hata wanyama wengine wakienda kumwona aliwakarimu vizuri kwa kuwapatia maziwa na Mizoga ambapo alisema si vyema kutupa nyama za wanyama waliokufa hivyo ni Bora wale kuliko kupoteza chakula kile. Wanyama wengine walimpenda na aliwatumia mbwa mwitu vizuri sana kumkamatia wanyama huko porini na hatimaye walimletea .Porini kukawa na kelele na malalamiko mengi.

Fisi alikuwa akicheka tu na kujiondokea akitembea kwa madaha. Alidai wanyama wengine walikuwa na wivu kwa kuwa yeye anafanana na SImba kidogo kule mbele, ana mabaka kidogo kama chui na pia huku nyuma chini ni mnyama kama aina ya wanyama wasiokula nyama.

Alicheka na kuelekea kwenye jumba lake la Ufalme. Fisi alifanya Uharibifu mkubwa sana mle porini akiwaacha wanyama wengine wafanye watakavyo. Porini kulikuwa na kilio. Kila mnyama aliyeweza kumla mwenzie aliruhusiwa tu bila shida. Fisi alikuwa mwoga na mwenye uchu mkubwa. Kwa sababu hakuwa na nguvu aliwatumia wenye nguvu kumsaidia kukamata wanyama na kuwala. Na hata alipopelekewa mashtaka ya uvunjifu wa sheria hakuweza kuwahukumu wenzie.

Maana walikuwa wanakula wote. Nyumbu walilalamika sana kuliwa na Mamba. Mamba alisema yeye huwa hawafati Nyumbu nchi kavu, ni wao wenyewe wanakuja mtoni wanamkanyaga hivyo wakidondoka wanakufa na maji hivyo anaona ili wasioze na kuharibu maji basi ni bora awale. Mamba aliyasema haya huku akitabasamu na kujichokonoa kwenye meno na kijiti. Fisi alimtizama tu Mamba na kutabasamu.Basi majira yakakatika ukaja wakati mwingine wa kuchagua Viongozi.

Alijitokeza Nyati na SImba pia. Walifanya Kampeni kubwa wote wakijinadi na hatimaye Simba alishinda hasa baada ya kuwa aliahidi wanyama wengine kuwa yeye atakuwa mkali kuwakamata na kuwaondoa pori lile wanyama wote waliofanya uharibifu na kula wenzao kipindi cha utawala wa Mfalme Fisi.

Wanyama walimkubali sana.hasa baada ya kumwona SImba huyu ni Mpole usoni mwao lakini kila alipozungumzia ubadhilifu uliofanywa na wanyama wa Ufalme uliopita aliruka kwa hasira, alinguruma na kupiga piga miguu yake ya mbele akikwaruza chini kwa hasira. Wanyama wale walimpenda sana Simba wakiamini kweli walihitaji kupata Mfalme mkali si kama Fisi aliyekuwa anawala wanyama na kuacha wanyama wengine wawale pia.

Nyati alishindwa kwenye Uchaguzi hasa baada ya kutishiwa pia na makundi makubwa ya Mbwa Mwitu, Mbweha,duma n.k Nyati akashindwa uchaguzi ule Simba akawa ndiye Mfalme.

Simba huyu alianza kwanza na kuwakamata kamata nguruwe pori, akawakamata na vicheche…wanyama wengi wakamsifu. Alipita porini kote akinguruma na kusababisha pori zima liwe limetulia. Wanyama wengine walikatazwa kabisa kutoa Sauti zao. Simba huyu alitaka angurume kila kona ya pori lile akipita kila sehemu wanyama walijua amepita. Porini kukaanza kurudi hali ya utulivu,woga na hofu.

Haikuchukua muda mrefu wanyama walikuja kugundua kuwa Simba Yule pamoja na zile mbwembwe zake,kutoa kucha kali wakati wote, kunguruma n.k kumbe alikuwa Kibogoyo. Ndo maana hakuweza kuwakamata au kuwakemea Fisi, hakuweza kuwakemea Chui, Duma ,kiboko na Vifaru. Yeye alikuwa anawakamata vicheche, paka shume na wanyama wadogo wadogo akawararua kwa makucha yake miili yao ikavuja damu na wengine wakafa kwa kihoro au kuishiwaa damu.

Kamwe hakuonekana akiwang’ata zaidi ya kuwakwarua na kuwagonga gonga. Simba alipoona kuwa wanyama wameanza kugundua kuwa yeye ni kibogoyo aliwaalika mbwa mwitu wawe wakitumika kuwanyamazisha wanyama wengine mle porini. Pori zima likafundishwa nyumbo na mapambio ya kumsifu Mfalme Simba shujaa. Huyu Mfalme Simba , Simba Kibogoyo.
 
KISA CHA MFALME SIMBA KIBOGOYO
Miaka fulani huko Porini kulikuwa na Utaratibu wa Wanyama kubadilishana madaraka. Kila baada ya majira fulan wanyama walikusanyika na kuchagua Mfalme. Huu ulikuwa ni utaratibu waliojiwekea wanyama hao kwa nia ya kubadilishana madaraka.

Wanyama hawa kabla ya kuwa na utawala wao walikuwa wakitawaliwa na binadamu kwa miaka mingi sana. Waliamua kufanya harakati za kumwondoa Binadamu na hatimaye walifanikiwa kumuondoa binadamu. Hivyo wakaamua Tembo ndo awe mfalme wao huko porini. Walimwona Tembo ni mpole na pia alikuwa ni mkubwa sana ukilinganisha na wao. Pia jambo la faraja Tembo alikuwa na uwezo wa kuwakemea wanyama wote wanaokula nyasi,nyama na hata vijidudu/wadudu. Tembo alitawala kwa miaka kadhaa ni kweli yeye hakuwa akila wanyama wenzie ingawa kuna kipindi ilitokea bahati mbaya aliwalalia wanyama wengine wakiwa kwenye mapumziko yao bila yeye kujua wakafa. Na kuna wakati aliwalalia kusudi kuwaadhibu pale walipokuwa wanaenda kinyume naye. Lakini alikuja tu kusema ilikuwa bahati mbaya hakuwaona. Ilitokea mara chache sana lakini Wanyama wengine bado waliendelea kumheshimu na kumpenda kwa sababu siku zilivyozidi kwenda alizid kuonesha busara na hekima. Muda wake ukaisha yakaja majira mengine. Tembo akapendekeza apewe Nguruwe utawala. Ikaonekana Nguruwe pia hakuwa tatizo ikizingatiwa Nguruwe alikuwa ameoa Nyani hivyo ikaonekana watasaidiana vizur tu kwnye Utawala.

Walitawala na ikatokea kuwa Nguruwe yeye hakuwa akila nyama za wanyawa wenzie lakini pia hakuwa mkali kwa wanyama waliokuwa wakiwaonea wanyama wadogo na kuwala.Na ikabainika naye baadaye alikuwa akila Wanyawa wadogo wadogo pamoja na kujinadi kuwa yeye hula majani. Mkewe. Nyani akawa akila sana wanyama kwa siri na ikawa ni tatizo kule Porini. Majira yakaenda baadaye ikaonekana kuwe na Jamii mbalimbali za Wanyama walete wagombea wao wagombee Ufalme. Jamii ya Wanyama wala nyama wakashinda kwa kuwa walikuwa na nguvu na waliogopwa sana. Basi Chui akawa Mfalme. Alianza kwa ukali dhidi ya wanyama wenzie ambao wanakula nyama akiwaasa waache kula wanyama wenzao. Siku zilivyozidi kwenda Chui uchu wa kula nyama ukamjaa akaanza kula wanyama wenzie waziwazi kabisa. Kukawa na malamiko mengi porini. Muda wake ukaisha.baadaye ukafika wakati wa uchaguzi Fisi akajitokeza kugombea ufalme. Wanyama wengi wakampenda Chui kwa kuwa yeye wakati mwingi alikuwa akicheka. Hasa ukifika usiku akisikia kuna sherehe Fisi alipenda kucheka kwa sauti sana. Wanyama pia walivyomuona akitembea kinyonge na kucheka na umbo lake hawakuona kama atakuwa Kikwazo kwao.zikapigwa Kampeni Fisi akachaguliwa kuwa Mfalme. Siku zote Fisi alikuwa akizunguka pori zima akisema anatafuta malisho mema kwa ajili ya wanyama wote n.k kumbe alikuwa akitafuta mizoga na akawa akishirikiana na wanyama kama mbwa mwitu,chui n.k wakiua na kula wanyama wengine wanaokula nyasi. Tofaut yake ilikuwa hata wanyama wengine wakienda kumwona aliwakarimu vizuri kwa kuwapatia maziwa na Mizoga ambapo alisema si vyema kutupa nyama za wanyama waliokufa hivyo ni Bora wale kuliko kupoteza chakula kile. Wanyama wengine walimpenda na aliwatumia mbwa mwitu vizuri sana kumkamatia wanyama huko porini na hatimaye walimletea .Porini kukawa na kelele na malalamiko mengi.Fisi alikuwa akicheka tu na kujiondokea akitembea kwa madaha. Alidai wanyama wengine walikuwa na wivu kwa kuwa yeye anafanana na SImba kidogo kule mbele, ana mabaka kidogo kama chui na pia huku nyuma chini ni mnyama kama aina ya wanyama wasiokula nyama.

Alicheka na kuelekea kwenye jumba lake la Ufalme. Fisi alifanya Uharibifu mkubwa sana mle porini akiwaacha wanyama wengine wafanye watakavyo. Porini kulikuwa na kilio. Kila mnyama aliyeweza kumla mwenzie aliruhusiwa tu bila shida. Fisi alikuwa mwoga na mwenye uchu mkubwa. Kwa sababu hakuwa na nguvu aliwatumia wenye nguvu kumsaidia kukamata wanyama na kuwala. Na hata alipopelekewa mashtaka ya uvunjifu wa sheria hakuweza kuwahukumu wenzie. Maana walikuwa wanakula wote. Nyumbu walilalamika sana kuliwa na Mamba. Mamba alisema yeye huwa hawafati Nyumbu nchi kavu, ni wao wenyewe wanakuja mtoni wanamkanyaga hivyo wakidondoka wanakufa na maji hivyo anaona ili wasioze na kuharibu maji basi ni bora awale. Mamba aliyasema haya huku akitabasamu na kujichokonoa kwenye meno na kijiti. Fisi alimtizama tu Mamba na kutabasamu.Basi majira yakakatika ukaja wakati mwingine wa kuchagua Viongozi. Alijitokeza Nyati na SImba pia. Walifanya Kampeni kubwa wote wakijinadi na hatimaye Simba alishinda hasa baada ya kuwa aliahidi wanyama wengine kuwa yeye atakuwa mkali kuwakamata na kuwaondoa pori lile wanyama wote waliofanya uharibifu na kula wenzao kipindi cha utawala wa Mfalme Fisi. Wanyama walimkubali sana.hasa baada ya kumwona SImba huyu ni Mpole usoni mwao lakini kila alipozungumzia ubadhilifu uliofanywa na wanyama wa Ufalme uliopita aliruka kwa hasira, alinguruma na kupiga piga miguu yake ya mbele akikwaruza chini kwa hasira. Wanyama wale walimpenda sana Simba wakiamini kweli walihitaji kupata Mfalme mkali si kama Fisi aliyekuwa anawala wanyama na kuacha wanyama wengine wawale pia.

Nyati alishindwa kwenye Uchaguzi hasa baada ya kutishiwa pia na makundi makubwa ya Mbwa Mwitu, Mbweha,duma n.k Nyati akashindwa uchaguzi ule SImba akawa ndiye Mfalme.
Simba huyu alianza kwanza na kuwakamata kamata nguruwe pori, akawakamata na vicheche…wanyama wengi wakamsifu. Alipita porini kote akinguruma na kusababisha pori zima liwe limetulia. Wanyama wengine walikatazwa kabisa kutoa Sauti zao. Simba huyu alitaka angurume kila kona ya pori lile akipita kila sehemu wanyama walijua amepita. Porini kukaanza kurudi hali ya utulivu,woga na hofu. Haikuchukua muda mrefu wanyama walikuja kugundua kuwa Simba Yule pamoja na zile mbwembwe zake,kutoa kucha kali wakati wote, kunguruma n.k kumbe alikuwa Kibogoyo. Ndo maana hakuweza kuwakamata au kuwakemea Fisi, hakuweza kuwakemea Chui, Duma ,kiboko na Vifaru. Yeye alikuwa anawakamata vicheche, paka shume na wanyama wadogo wadogo akawararua kwa makucha yake miili yao ikavuja damu na wengine wakafa kwa kihoro au kuishiwaa damu. Kamwe hakuonekana akiwang’ata zaidi ya kuwakwarua na kuwagonga gonga. Simba alipoona kuwa wanyama wameanza kugundua kuwa yeye ni kibogoyo aliwaalika mbwa mwitu wawe wakitumika kuwanyamazisha wanyama wengine mle porini. Pori zima likafundishwa nyumbo na mapambio ya kumsifu Mfalme Simba shujaa. Huyu Mfalme Simba , Simba Kibogoyo.

Unazunguka weeeeee!!
Si useme tu unachotaka kusema au unaogopa faini ya M7?
 
hadithi nzuri.
 
Ni ndefu sana ila nimeisoma yote,imekaa vizuri,ujume umefika japo sidhani kama wahusika wanaweza kujishughulisha kusona hiki kisa chote hasa ukizingatia kuwa wao wamezoea sentensi mbili mbili za instagram
 
ha ha ha.. sasa Jamii Forums inapata watu tuliokuwa tunawataka. Hii hadith ukiisoma na kuielewa ni nzuri sana. hongera sana bro. Hadith kama hizi ni ngumu kuzipata miaka hii hasa kwa kizazi hiki cha doc com. sasa wewe mzee babu chizi maarifa unaturudisha nyuma miaka ile tunaulizwa hadith hii inatufundisha nini. nakupongeza maana hapa hakuna wa kusema umemsema yeye maana hujataja jina la mtu hata mmoja. hii ndo kazi ya fasihi kutupa burudani. simba huyo ana makeke lakini ni kibogoyo... hawezi kuuma wanyama wakubwa. anauma wadogowadogo na kuwashindwa wakubwa. ingawa ana mkwara sana na makeke mengi. ni kama simba wa maonesho au joka la kibisa. tuletee ngano hizi kila Ijumaa kaka ili weekend yetu ikwishe vizuri.
 
KISA CHA MFALME SIMBA KIBOGOYO
Miaka fulani huko Porini kulikuwa na Utaratibu wa Wanyama kubadilishana madaraka. Kila baada ya majira fulan wanyama walikusanyika na kuchagua Mfalme. Huu ulikuwa ni utaratibu waliojiwekea wanyama hao kwa nia ya kubadilishana madaraka.

Wanyama hawa kabla ya kuwa na utawala wao walikuwa wakitawaliwa na binadamu kwa miaka mingi sana. Waliamua kufanya harakati za kumwondoa Binadamu na hatimaye walifanikiwa kumuondoa binadamu. Hivyo wakaamua Tembo ndo awe mfalme wao huko porini. Walimwona Tembo ni mpole na pia alikuwa ni mkubwa sana ukilinganisha na wao. Pia jambo la faraja Tembo alikuwa na uwezo wa kuwakemea wanyama wote wanaokula nyasi,nyama na hata vijidudu/wadudu. Tembo alitawala kwa miaka kadhaa ni kweli yeye hakuwa akila wanyama wenzie ingawa kuna kipindi ilitokea bahati mbaya aliwalalia wanyama wengine wakiwa kwenye mapumziko yao bila yeye kujua wakafa. Na kuna wakati aliwalalia kusudi kuwaadhibu pale walipokuwa wanaenda kinyume naye. Lakini alikuja tu kusema ilikuwa bahati mbaya hakuwaona. Ilitokea mara chache sana lakini Wanyama wengine bado waliendelea kumheshimu na kumpenda kwa sababu siku zilivyozidi kwenda alizid kuonesha busara na hekima. Muda wake ukaisha yakaja majira mengine. Tembo akapendekeza apewe Nguruwe utawala. Ikaonekana Nguruwe pia hakuwa tatizo ikizingatiwa Nguruwe alikuwa ameoa Nyani hivyo ikaonekana watasaidiana vizur tu kwnye Utawala.

Walitawala na ikatokea kuwa Nguruwe yeye hakuwa akila nyama za wanyawa wenzie lakini pia hakuwa mkali kwa wanyama waliokuwa wakiwaonea wanyama wadogo na kuwala.Na ikabainika naye baadaye alikuwa akila Wanyawa wadogo wadogo pamoja na kujinadi kuwa yeye hula majani. Mkewe. Nyani akawa akila sana wanyama kwa siri na ikawa ni tatizo kule Porini. Majira yakaenda baadaye ikaonekana kuwe na Jamii mbalimbali za Wanyama walete wagombea wao wagombee Ufalme. Jamii ya Wanyama wala nyama wakashinda kwa kuwa walikuwa na nguvu na waliogopwa sana. Basi Chui akawa Mfalme. Alianza kwa ukali dhidi ya wanyama wenzie ambao wanakula nyama akiwaasa waache kula wanyama wenzao. Siku zilivyozidi kwenda Chui uchu wa kula nyama ukamjaa akaanza kula wanyama wenzie waziwazi kabisa. Kukawa na malamiko mengi porini. Muda wake ukaisha.baadaye ukafika wakati wa uchaguzi Fisi akajitokeza kugombea ufalme. Wanyama wengi wakampenda Chui kwa kuwa yeye wakati mwingi alikuwa akicheka. Hasa ukifika usiku akisikia kuna sherehe Fisi alipenda kucheka kwa sauti sana. Wanyama pia walivyomuona akitembea kinyonge na kucheka na umbo lake hawakuona kama atakuwa Kikwazo kwao.zikapigwa Kampeni Fisi akachaguliwa kuwa Mfalme. Siku zote Fisi alikuwa akizunguka pori zima akisema anatafuta malisho mema kwa ajili ya wanyama wote n.k kumbe alikuwa akitafuta mizoga na akawa akishirikiana na wanyama kama mbwa mwitu,chui n.k wakiua na kula wanyama wengine wanaokula nyasi. Tofaut yake ilikuwa hata wanyama wengine wakienda kumwona aliwakarimu vizuri kwa kuwapatia maziwa na Mizoga ambapo alisema si vyema kutupa nyama za wanyama waliokufa hivyo ni Bora wale kuliko kupoteza chakula kile. Wanyama wengine walimpenda na aliwatumia mbwa mwitu vizuri sana kumkamatia wanyama huko porini na hatimaye walimletea .Porini kukawa na kelele na malalamiko mengi.Fisi alikuwa akicheka tu na kujiondokea akitembea kwa madaha. Alidai wanyama wengine walikuwa na wivu kwa kuwa yeye anafanana na SImba kidogo kule mbele, ana mabaka kidogo kama chui na pia huku nyuma chini ni mnyama kama aina ya wanyama wasiokula nyama.

Alicheka na kuelekea kwenye jumba lake la Ufalme. Fisi alifanya Uharibifu mkubwa sana mle porini akiwaacha wanyama wengine wafanye watakavyo. Porini kulikuwa na kilio. Kila mnyama aliyeweza kumla mwenzie aliruhusiwa tu bila shida. Fisi alikuwa mwoga na mwenye uchu mkubwa. Kwa sababu hakuwa na nguvu aliwatumia wenye nguvu kumsaidia kukamata wanyama na kuwala. Na hata alipopelekewa mashtaka ya uvunjifu wa sheria hakuweza kuwahukumu wenzie. Maana walikuwa wanakula wote. Nyumbu walilalamika sana kuliwa na Mamba. Mamba alisema yeye huwa hawafati Nyumbu nchi kavu, ni wao wenyewe wanakuja mtoni wanamkanyaga hivyo wakidondoka wanakufa na maji hivyo anaona ili wasioze na kuharibu maji basi ni bora awale. Mamba aliyasema haya huku akitabasamu na kujichokonoa kwenye meno na kijiti. Fisi alimtizama tu Mamba na kutabasamu.Basi majira yakakatika ukaja wakati mwingine wa kuchagua Viongozi. Alijitokeza Nyati na SImba pia. Walifanya Kampeni kubwa wote wakijinadi na hatimaye Simba alishinda hasa baada ya kuwa aliahidi wanyama wengine kuwa yeye atakuwa mkali kuwakamata na kuwaondoa pori lile wanyama wote waliofanya uharibifu na kula wenzao kipindi cha utawala wa Mfalme Fisi. Wanyama walimkubali sana.hasa baada ya kumwona SImba huyu ni Mpole usoni mwao lakini kila alipozungumzia ubadhilifu uliofanywa na wanyama wa Ufalme uliopita aliruka kwa hasira, alinguruma na kupiga piga miguu yake ya mbele akikwaruza chini kwa hasira. Wanyama wale walimpenda sana Simba wakiamini kweli walihitaji kupata Mfalme mkali si kama Fisi aliyekuwa anawala wanyama na kuacha wanyama wengine wawale pia.

Nyati alishindwa kwenye Uchaguzi hasa baada ya kutishiwa pia na makundi makubwa ya Mbwa Mwitu, Mbweha,duma n.k Nyati akashindwa uchaguzi ule SImba akawa ndiye Mfalme.
Simba huyu alianza kwanza na kuwakamata kamata nguruwe pori, akawakamata na vicheche…wanyama wengi wakamsifu. Alipita porini kote akinguruma na kusababisha pori zima liwe limetulia. Wanyama wengine walikatazwa kabisa kutoa Sauti zao. Simba huyu alitaka angurume kila kona ya pori lile akipita kila sehemu wanyama walijua amepita. Porini kukaanza kurudi hali ya utulivu,woga na hofu. Haikuchukua muda mrefu wanyama walikuja kugundua kuwa Simba Yule pamoja na zile mbwembwe zake,kutoa kucha kali wakati wote, kunguruma n.k kumbe alikuwa Kibogoyo. Ndo maana hakuweza kuwakamata au kuwakemea Fisi, hakuweza kuwakemea Chui, Duma ,kiboko na Vifaru. Yeye alikuwa anawakamata vicheche, paka shume na wanyama wadogo wadogo akawararua kwa makucha yake miili yao ikavuja damu na wengine wakafa kwa kihoro au kuishiwaa damu. Kamwe hakuonekana akiwang’ata zaidi ya kuwakwarua na kuwagonga gonga. Simba alipoona kuwa wanyama wameanza kugundua kuwa yeye ni kibogoyo aliwaalika mbwa mwitu wawe wakitumika kuwanyamazisha wanyama wengine mle porini. Pori zima likafundishwa nyumbo na mapambio ya kumsifu Mfalme Simba shujaa. Huyu Mfalme Simba , Simba Kibogoyo.

Mkuu kwa mafumbo tu we kiboko!
 
Kwa hiyo mkulu ndio simba kibogoyo?

Na hao mbwa mwitu wanaotumika ndio wale wazee wa kupiga tu!!?

Sijamtaja mtu hapo, nyumba yangu ndio kwanza inahitaji kupauliwa na fweza zenyewe zakudunduliza, afu nije kulipa M7
 
Back
Top Bottom