Kisa cha Mapenzi...

Kisa cha Mapenzi...

Kitwego

Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
14
Reaction score
13
Naamini Jumapili iko salama kwa kila member na Kama hali haipo hivyo,ni changamoto za maisha tu,amini mambo yatakuwa sawa.
Kisa changu ni kama ifuatavyo hapa chini:

Mwaka 2015 nilihamia mkoa mmoja huko nyanda za juu kusini nikiwa kijana ambaye sikuwa na mahusiano ya kudumu. Katika pitapita zangu kwenye majukumu ya kazi nikakutana na binti ambaye alikuwa anasoma chuo kwa ngazi ya cheti, nikawa naye kwenye mahusiano ya kawaida kabisa mara akaanza kuwa anakuja kulala nilipokuwa naishi (nilipanga chumba kimoja). Siku zikasogea akaanza kuwa haendi chuo mara nyingine anashinda mle ndani nikiwa kazini,nikirudi jioni namkuta na maisha yanaendelea.

Baada ya miezi mitatu kwenye hili penzi binti akapata ujauzito, alivyoniambia kwanza nilishtuka na kwa kuwa najua bado anasoma nikajaribu kuongea naye ili tutoe hiyo mimba kwa kulinda future yake ya shule na familia pia (baadaye nilijua ni mtoto wa mchungaji)
Baada ya kukataa kutoa 2016 tulipata mtoto wa kike,tukafanye mpango wa familia zote kutufahamu na ikibidi mahari itolewe kule kwa binti.Kuanzia hapo mpaka leo tunaendelea kuishi pamoja ingawa hatujafunga ndoa.

Mwaka huohuo 2016 nikahama mkoa kikazi kwenda kanda ya ziwa, nilihama yeye akabaki mkoa tulipokutana,ikawa nikipata nafasi narudi kuwacheki kama familia naye pia akipata nafasi anakuja kunitembelea.Mkoa wa nyanda za juu kusini tulibahatika kujenga pia kwa hiyo lengo likawa abaki pale kuangalia na kutunza familia.

2018 nikahamia Dar kikazi, baada ya kama miezi mitatu akaja kunitembelea na kurudi huko mkoani. Baada ya kurudi kule akaanza ooh Mara anahisi mpweke sana kwa hiyo naye anataka aje,nikamuomba asubiri niweke mazingira sawa.

Kwa kipindi chote hicho cha 2017-2019 mwishoni, alikuwa ananituhumu sana kuwa mm ni Malaya,na haya yalitokana na tabia yake ya kuwa anakagua simu yangu nikiwa nimelala. Vikao vijana vingi ukweni maana kila tukigombana anashitaki kwao,mambo mengine mazito ya ndani anayaweka kikaoni mpaka ikawa tabu sana,tulishafika kipindi mpaka tukataka kuachana ila pande zote walitukalisha yakaisha.

2019 nikaona namba imemtumia hela kweli nilikuwa naitilia mashaka ile namba,siku hiyo hiyo usiku nikiwa nimelewa mwanamke huyu alileta mdomo sana ikabidi nimpige ingawa haikuwa tabia yangu.

Alfajiri siku iliyofuata huyo kapanda basi kwenda kwao, nikampigia mamaa yake kumweleza hiyo ishu,akaaka kwao kama siku tatu halafu akarudi Dar ila cha kushangaza akaenda kukaa kwa shoga na kwao aliwaambia karudi kwangu.

Kweli baada ya kumpeleleza akasema ameamua kufanya kwa kuwa moyo wake bado hauko sawa kutokana na nilichomtendea, nikasema sawa nikawa naenda kumtembelea kwa huyo shosti yake mpaka aliporudi home tukaendelea na maisha.

Kufupishwa story...

Hivi karibuni baada ya kumuuliza yule mwanaume ni nani,maana niliendelea kumuona kwenye mazingira mbalimbali na mpaka kwao wakasema ni ndugu yake,kumbe hawa ndugu walishadate tangu 2012 hata kabla ya huyu mwanamke kufamiana na mimi, kwa maelezo ya huyu mwanamke, kumbe yule bwana niliyetilia mashaka namba yake wanafaniana kiundani mpaka watoto wake wanamfahamu huyu mwanamke na mpaka sometimes alikuwa anatumwa yeye kuwapelekea mahitaji ya shule hao watoto.

So katika kunipa maelezo ya kilichotokea ni kwamba tukigombana alikuwa anaenda kwa jamaa wanadinyana kisirisiri anadai wameacha walivyokuja kujua kuwa ni ndugu(2019)

Sasa hivi tuna mtoto wa pili ambaye alizaliwa mwaka jana katikati na utata umekuja baada ya mwanamke kutojua mimba alipata lini ingawa katika mwezi ambao ni makisio ya mimba kuingia, alifanya mapenzi na huyo jamaa maana mimi tulikuwa tumegombana.

Kwa hiyo jana nilivyopata hii simulizi kutoka kwenye kinywa cha mwanamke, kiukweli mpaka sasa nawaza cha kufanya ili nijue ukweli na uhalali wa huyu mtoto wa pili maana nipo njia panda.

Samahani kwa stori ndefu hivi
 
Kutaka kujua uhalali wa mtoto ni kwenda kupima DNA. Ila nini mzee, kitanda hakizai haramu, lea mtoto wako bwana achana na mambo ya kutaka kufukunyua sana kama hamtaki kuachana.
 
Nchi Ngumu Sana
Hapo Pagumu Sana
Ujanjaujanja Kwenye Mahusiano Ndiyo Tatizo Kubwa Kuliko Ndoa
 
Tuishi nao Kwa Akili Mkuu
JamiiForums2014638457.jpg
 
Pole sana Bwana Kitwego, muache ajifungue salama. Watoto wa namna hiyo kikwetu tunawaita Fidias (Fidia), you didn't play your part; accept the end product of your negligence. Nataka tukae pamoja wewe hutaki, kwa nini hutaki kukaa na mkeo?

Ushauri wangu
1. Usiwe una mpuuza mkeo.
 
Atakusumbua sana huyo mwanamke kwasababu akili zake hazina akili
 
Pole sana Bwana Kitwego, muache ajifungue salama. Watoto wa namna hiyo kikwetu tunawaita Fidias (Fidia), you didn't play your part; accept the end product of your negligence. Nataka tukae pamoja wewe hutaki, kwa nini hutaki kukaa na mkeo?

Ushauri wangu
1. Usiwe una mpuuza mkeo.
Asante mkuu kwa ushauri,kimsingi si kumpuzaa kiasi hicho ila tu zile changamoto za kawaida ambazo naamini kwenye mahusiano mengi sana,sema tu ndo alichokieleza yeye ndo kimenivuruga kwa kiasi kikubwa
 
Kutaka kujua uhalali wa mtoto ni kwenda kupima DNA. Ila nini mzee, kitanda hakizai haramu, lea mtoto wako bwana achana na mambo ya kutaka kufukunyua sana kama hamtaki kuachana.
Asante sana kwa ushauri wako,kwa hiyo unataka niachane na haya mambo,ingawa bado mind inanisumbua sana
 
We jua tu unaishi na mke wa mtu.huyo sio wako na hakutoshi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom