Kisa cha kweli, mbingu ipo na moto wa jehanamu upo

Walokole wanapenda sana hizi stori. Mara alienda kuzimu akaona watu wanateseka nk. Hakuna moto, ila Mungu wa mbinguni yupo.

Ndio walewale walioenda airport na kusubiri wapae bila ndege
Sijui walienda airport kufanya nini

Kuna watu wanavaa tu nguo Safi ila mmh
 
Mkuu


Mkuu shetani ni kiumbe cha kutisha soma
Ezekieli 28:17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. Ezekieli 28:18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. Ezekieli 28:19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.
Hapana....Mungu alimuumba Lucifer akiwa kiumbe mzuri sana pengine kuliko wote....toka alipoasi hakunyang'anywa uzuri ule....hata malaika walioasi wamebadilika tabia tu...ila ni wazuri kimuonekano.

Ilo neno kuwa amekuwa kitu cha kutisha wewe umejuaje kuwa anazungumzia muonekano wake? What if amemaanisha badiliko la kitabia? Hiyo Ezekiel 28 uliyonukuu huko juu inasema Lucifer aliumbwa kwa jinsi ya ajabu na kupendeza...sauti nzuri, firimbi, alifunikwa kwa madini ya kupendeza.

Jua hili kuwa Mungu hakumnyang'anya chochote huyo kiumbe...nguvu zake bado angali anazo..ijapokuwa anazitumia vibaya...kuwashawishi watu watende dhambi.

Hata sisi wanadamu, baada ya anguko la dhambi tulibadilika tabia na kuondokewa na vazi la utukufu uliowafunika Adam na mkewe..ila muonekano wetu wa kimwili ukabaki kuwa ule ule...ukiambatana na laana alizotamka Mungu kama kifo n.k

Shetani (Kerubi afunikaye) na malaika zake ni wazuri kimuonekano...hao viumbe wa kutisha ambao unadai ndugu yako aliwaona hawajawahi kuwepo...na si sehemu ya uumbaji wa Mungu. Mungu hakuumba kiumbe wa namna hiyo. kumbuka Shetani hana uwezo wa kujiumba upya...uumbaji ni uwezo wa Mungu pekee.
 
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
acha uswahili kijana hata mimi naweza kukuletea vifungu vya kitabu cha biblia nikashusha mbaka forum ikajam
Ila haitaondoa ukweli kwamba hizo ni ngano za wayahudi na wayunani wa kale !
 
Ujumbe unaotaka kuleta au kusisitiza kwenye huu uzi wako ni ubatizo wa maji mengi basi hamna la zaidi.

Kama kuingia mbinguni ni kufanya copy & paste ya kila alichofanya Yesu. Mathalani kubatizwa kwa staili ya Yesu alivyobatizwa Basi pia inabidi wote tukabatizwe mto yordani alikobatiziwa yesu tena kwa maji yaliotuama. Na wala sio tiririka kama huku mfanyavyo au kwenye mitungi na visima vya kutengeneza.
Naomba umuulize mtoa mada..kwa majeng au machache kuna tija gan..atueleze hapo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ya asubuhi wakuu!! Hiki ni kisa cha kweli kwa ambaye sio muumini wa Mbinguni na kuzimu hivyi vyitu ni halisi.

Miaka kadhaa iliyopita ndugu yangu, aliumwa sana wakati yupo hospitalini tunaamuuguza, alikuwa ameokoka (mlokole), hivyo kwenye ile wodi wachungaji mbalimbali walikuwa wanapishana kuja kumuombea maana aliumwa kipindi kirefu sana, Siku moja jioni alizidiwa na hatimae kufariki dunia( kwa mjibu wa dakitari ) baada ya taratibu za hapa na pale mwili kuandaliwa! Kupelekwa mchowari alipiga chafya na kurejea na kutoka pale akawa mzima mpaka leo, alichokisema ni hiki hapa baada ya kuzinduka

1: Kuna maisha baada ya haya, anasema alitoka nje ya mwili wake na akaona jinsi dakitari alivyokuwa anampima pima na jinsi ndugu walivyoanza kulia, baada ya hapo alijikuta yupo dunia nyingine kabisa tofauti na hii!!

2: Anaendelea kusema unakuwa na akili zako zote na kumbukumbu zako zote, maana yeye alipofika eneo hilo alikuwa anakumbuka kila kitu kilichopo duniani, na alijua amekufa!

3: Matendo yako ndo yataamua uende njia ipi , ya mbinguni au kuzimu, anasema baada ya kufika eneo aliona kwa mbali majitu mawili ya kutisha yanakimbia kuja kumlaki!, lakini ghafula wakashuka watu wawili wamevaa nguo nyeupe wale majitu waliopoona wale watu wawili walirudi nyuma, wale malaika wakamwambia arudi abatizwe kwa maji mengi, maana hawezi kuingia mbinguni, na ndo maana wale majitu yalikuwa yanamfuata!! Baada ya kuambiwa rudi duniani ukabatizwe ndipo akarejea duniani!

Note:
1: Hamna mtu atakayeenda mbinguni bila kumwamini Yesu!!
2: Ukitaka kwenda mbinguni fuata yote aliyoyafanya Yesu ikiwemo ubatizo aliobatizwa sio vinginevyo.

Huu ushuhuda ni kweli wakuu, Sio wa kudharau.
waliokufa miaka ya 1700 hapa tanganyika kabla wahubili dini hawajaja wataenda wapi na habari za yesu walikua hawajazisikia
 
Shida imeanzia hapa. Yaani UONGO umeanzia hapo.
Hawa jamaa tangu waambiwe fanya lolote ilimrad wati waokoke..hata ukidanganya fresh tu ilimrad watu waokoke..bas wao wanafanya sifa...ndomana unaona utapel makanisan...kuna siku naangalia tv mchungaj malisa wa ubungo et anamtoa mtu pepo...pepo limejitambulsha mim ni lucifer..af likawa linaongea kiingereza...sasa hko kiingereza chenyew ni broken...yaan no grammar no correct tenses etc.vurugu..nikasema ...hiv kwel lucifer kama lucifer aongee broken hiv???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
waliokufa miaka ya 1700 hapa tanganyika kabla wahubili dini hawajaja wataenda wapi na habari za yesu walikua hawajazisikia
Warumi 2:11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. Warumi 2:12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. Warumi 2:13 Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. Warumi 2:14 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Warumi 2:15 Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
 
Hizi ndiyo zinaitwa simulizi za alfu lela u lela.
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
 
acha uswahili kijana hata mimi naweza kukuletea vifungu vya kitabu cha biblia nikashusha mbaka forum ikajam
Ila haitaondoa ukweli kwamba hizo ni ngano za wayahudi na wayunani wa kale !
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
 
Ndio walewale walioenda airport na kusubiri wapae bila ndege
Sijui walienda airport kufanya nini

Kuna watu wanavaa tu nguo Safi ila mmh
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom