holy spirit
JF-Expert Member
- Nov 30, 2020
- 700
- 1,040
Dini nyingi (kama sio zote) duniani zinatueleza kwamba tutapewa zawadi ya maisha mengine baada ya kifo huko mbinguni sehemu ambayo tunaweza kusema kulingana na Imani za kidini ni yenye uzuri uliokamilika kwa asilimia mia pasipo na mapungufu yoyote. Na pia tunapewa ahadi ya miili mipya na kukutanishwa na wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki. Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo yananitatiza kuhusu hii dhana ya mbinguni ningependa kuyaleta kwenu.
1. Tuna ndugu zetu na watu wetu wa karibu ambao tunawapenda na tunawatakia mema (wazazi,watoto, marafiki, kaka na dada zetu), nawezaje kuwa na furaha mbinguni kama mimi nilitimiza vigezo vya kuepuka kuchomwa moto huku mtu/watu wangu ninaowapenda na kuwatakia mema hawakutimiza vigezo hivyo kama ilivyoelezwa na vitabu vitakatifu? au nitawasahau tu nikiwa huko?
2. Vipi mtu akiniua halafu akapata nafasi ya kutubu? nendaje kuishi nae mbinguni? au nitafanywa nisahau tu alichonifanyia? au wale wanaobaka na kuua watoto wakitubu wataenda tu mbinguni kukutana na hao watoto na wazazi wao? wataishi vipi maana mbinguni hamna chuki wala uadui?
3. Kuhusu swala la umri
Nikipewa mwili mpya nitakuwa kwenye ule umri niliokufa nao?
Tukiwa mbinguni tunaganda kwenye umri fulani (hauongezeki wala kupungua) ?
Vipi kuhusu watoto waliokufa bado wachanga wataachwa hivyo hivyo?
Vipi kuhusu watoto ambao hawajazaliwa, wanawake hawatakiwi kutoa mimba kwasababu Ile mimba ni mtoto anaeishi. Mama akitoa mimba sidhani kama mtoto ataadhibiwa kwa maamuzi ya mama yake, kama ni hivi mbinguni si patajaa mabaki ya watoto ambao utengenezwaji wao kwenye mwili wa mama yao ulikuwa haujakamalika ("fetuses" kiswahili chake nadhani tunaita "vijusi") au watakuzwa kikamilifu?
Vipi wazee ambao watatamani warudi kwenye umri wa ujana? Watapewa hii nafasi? Maana mzee sidhani kama atahimili mabikra wote 72 inahitaji nguvu ya ujana kidogo
4. Kuna swala pia la kula mbinguni.
Kwa wakristo inaonekana halitahitajika kulingana na Ufunuo 7:16 kwamba njaa wala kiu havitakuwepo. Lakini Marko 14:25 inasema "Kweli nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa upya katika ufalme wa Mungu" pia Luka 24: 42-43 inasema "Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, naye akakichukua na kukila mbele yao", hapa kwenye samaki ni baada ya kufufuka. Kwa hiyo apa inaonekana yesu aliahidi kunywa divai mbinguni lakini pia alikula samaki akiwa kwenye mwili wake wa ufufuo. Kwa hiyo kulingana na wakristo tunaweza kusema japo sio lazima kula mbinguni ila inawezekana sababu ahadi ya kunywa ipo na ushahidi wa kuweza kula tukiwa kwenye mwili wa ufufuo upo.
Quran Iko wazi kuhusu matunda na nyama kwenye hili andiko
Any fruit that they may choose, And the flesh of fowls that they desire"[56:20-21]
Tatizo langu ni kwamba kama watu wataweza kula hasa nyama au samaki vitatoka wapi? jibu rahisi ni kwamba vitatoka kwenye mazingira yanayokuzunguka tu huko mbinguni. Kwa maana hiyo hawa wanyama walikufa duniani ili waende mbinguni wauliwe tena na kuliwa na wanadamu? Wanyama hawana haki ya kufaidi maisha ya mbinguni? maana hawawezi kufaidi wakiwa na wasiwasi wa kuliwa.
NAOMBA MCHANGO WENU
Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app