Kisa cha kweli cha Marietha!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha kweli cha Marietha!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Oct 29, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Leo Marietha anatimiza miaka 50 kamili na ana watoto 4 wakubwa wanaojitegemea na ametengana na mume wake kwa mwaka wa 10 sasa. Marietha ni mwanamke msomi na mjasiriamali na pia ni mwanaharakati! Miaka 30 iliyopita kuna tukio lililomtokea Marietha ambalo ndilo hasa nataka kushiriki nanyi kwenye siku yake hii ya kuzaliwa. Awali ya yote "Happy Birthday" Marietha!!

  Mwaka 1981 wakati huo Marietha akiwa ni binti wa miaka 19 alikuwa amemaliza masomo ya sekondari Kidato cha Sita na anangojea kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria. Wakati huo Marietha alikuwa ana Boy Friend wake waliokuwa wanapendana sana tena sana ambaye naye alikuwa amemaliza kidato cha Sita kama yeye Marietha.

  Lakini katikakati ya Mahusiano yao hayo akatokea Bwana mmoja ambaye anamzidi Marietha kwa miaka 6 na kumrubuni Marietha aachane na mpenzi wake kwa ahadi na zawadi mbalimbali. Katikati ya Mahusiano hayo mapya Marietha akashika ujauzito. Lakini bila ya kumjulisha mpenzi wake wa awali kwamba ni mjamzito.

  Kabla ya kwenda JKT mpenzi wake wa zamani akagundua kwamba Marietha ni mjamzito, na alipombana amueleze ni ujauzito wa nani Marietha maji yakazidi unga akamtaja jamaa aliyemrubuni ambaye wakati huo alikuwa anasomea Diploma yake ya uhasibu pale IFM. Yule mpenzi wake wa awali akakubali kwamba walee ile mimba mpaka mtoto atakapozaliwa halafu waendelee na uhusiano wao kwa lengo la kujenga familia yao pamoja na mtoto wa yule jamaa.

  Hayo yote yakitokea Marietha hakuwahi kumwambia yule aliyempa mimba kama ana uhusiano na mtu mwingine. Siku moja kabla ya kwenda JKT yule mpenzi wake alimtembelea Marietha nyumbani kwao kwa nia ya kumuaga, wakati huo Marietha alikuwa anaishi kwa wazazi wake kwenye Maghorofa ya NHC (zama hizo Msajili wa Majumba) maeno ya Faya.

  Baada ya maongezi na kuagana kwingi Marietha alimsindikiza Mpenzi wake huyo hadi kituo cha Basi Faya, na walipoagana jamaa akawa anavuka upande wa Pili wa barabara ili akapande UDA za kwenda Ubungo. Alipokuwa anavuka barabara gari moja likitokea maeneo ya Posta kwa kasi lilimgonga na kufariki papo hapo!!

  Kishindo kile cha kugongwa kilimstua Marietha na alipogeuka alimuona Mwanaume aliyempenda amelala chini kwenye dimbwi la damu akiwa hana uhai tena. Ingawa Marietha aliolewa na yule aliyempa Mimba na kufanikiwa kuongeza watoto wengine watatu lakini mpaka leo anasema kila inapofika siku aliyogongwa mpenzi wake yule hufanya kumbukumbu ya kibinafsi. Bahati MBAYA sana kwake siku hiyo ni siku yake pia ya kuzaliwa!! Happy Birthday Marietha!!
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  nitarudi.

  Afu leo bday ya mpendwa wangu mmoja

  happy birthday dude!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  duh.....too much coincidence
  hiyo ajali
  na huyo jamaa kumrubuni
  na Marietha kutomsahau huyo mtu
  inawwezekana kuna siri ndani yake
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  okey!!!
   
 5. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Funzo lake ni nini hasa?
   
 6. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  sasa wewe umejuaje yote hayo kama sio fiction
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  aiseee!marietha????????
  happybirthday lakini
   
 8. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa kwanza anaelewa baba ake mzazi ametangulia mbele ya haki?
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Pole yake kwa tukio lilimtokea la kumpoteza mpendwa wake, Happy Birthday kwake kutimiza umri huo!
  By the way hapo kwenye bold pananichanganya, aliwezaje kudanganywa akiwa katikati ya mahusiano na mtu ambaye anasema alimpenda sana? Ni tamaa au kitu gani?
   
 10. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani wewe jambo usilolijua ndiyo linakuwa Fiction? Marietha unamjua na unajua uhusiano wake na mimi? Marietha ni rafiki yangu kwa miaka 30 sasa na wote tuna njia ndefu tuliyopita pamoja kama "dada na kaka". Tujifunze kutumia zaidi akili zetu kwenye kuchanganua mambo!!
   
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  Hivi mi ni mwalimu wa kiswahili au kichina?
   
 12. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimeleta hiki kisa kwa sababu Marietha aliniahadithia kujuta kwake kukubali krubuniwa wakati ule kwa mafuta ya "Yolanda" na sabuni toka Kenya na kumtenda Mtu waliyekuwa wanapendana. Siku zote kila ifikapo Birthday yake hukumbuka tukio hilo kwani pamoja na kwamba alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine aliyekuwa mpenzi wake wa dhati alikuwa tayari kusahau yote na kuanza upya.

  Ilitokea nasibu tu (Cioncidence) tu kwamba ajali yenyewe ilitokea siku ya kuzaliwa kwake, lakini kumbe ndiyo imeacha kumbukumbu mbaya kwenye maisha ya Marietha. Maisha yake ya baadaye na yule aliyempa mimba hayakuwa mazuri sana kwani mbele ya safari Jamaa alipoukwaa "Uheshimiwa" alimtelekeza na kuona binti mdogo wa kizaramo ambaye naye wamezaa naye watoto wawili.

  Madhila aliyoyapata toka kwa mumewe baadaye ndiyo yanamfanya aamini labda yule waliyependana naye angekuwa ni mume bora zaidi ya huyu Mheshimiwa. Jamaa sasa yuko Bungeni kupitia CCM na ana cheo kikubwa tu kwenye taasisi hiyo kubwa ya kutunga sheria!
   
 13. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  my birthday wishes to her.
  ashukuru Mungu hakuvuka barabara na yule mpenzi wake.

  huyo Mbunge alimrubuni mke wake imagine atatufanya nini sisi Watanzania ambao hatujui. nchi za watu hiyo ni bonge la reason ya kumnyima mtu kura.
   
 14. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Story ni ndefu na muda hautoshi, ngoja niwahi kwanza tren ya Mwakyembe nitarudi kuisoma baadaye. Ila HAPPY BIRTHDAY MAMA.
   
 15. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Na mimi huwa namwangalia "Mheshimiwa" yule naishia kucheka. Kwa kweli maadili ya viongozi wetu wengi wa siasa ni ya kuyatilia shaka!!
   
 16. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Da so sad,
  Happy birthday Marietha na pole kwa kumbukumbu hii.

  Hiyo ndiyo historia yako dada!
   
 17. Advicer

  Advicer JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  audiance ndo wanatafuta maana cku zote
   
 18. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ananikumbusha enzi za "mama na mwana" ambako mwisho wa hadithi Debora Mwenda anasema maana ya hadithi. Bahati mbaya kwake hii siyo hadithi ya kutunga!!
   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kwani huyo kiongozi ana tatizo gani Kigarama ...herietha alilazimishwa? ni tamaa zake tu zilimponza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kosa la moja kwa moja haliwezi kuonekana kirahisi. Lakini huyu mheshimiwa pamoja na kumrubuni mtoto wa shule na baadaye kumuoa mwisho wa siku alipoukwaa uheshimiwa akamtelekeza. Marietha amepanda ngazi hadi sasa ana PHD yake kwa kujituma kwa hali ya juu pamoja na ukweli kwamba wakati fulani mumewe alimsaidia kumfundisha baadhi ya masomo!!
   
Loading...