Kisa cha kofia Bungeni

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
458
171
Kisa cha kofia bungeni

1
Kisa cha sasa kofia, kimetokea bungeni

Na hoja aliitoa, akilalama bungeni

Kwa kina kaelezea, kadharauliwa juweni

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

2
Kakasirika jamaa, kajieleza bungeni

Heshima kamvunjia, hajaelewa kwanini?

Ni vipi amemvua, baraghashia kichwani

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

3
Ilikuwa ni kofia, kaeleza kwa makini

Aina baraghashia, kanyambulisha kwa ndani

Mdada kamzengua, kainyakua kichwani

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

5
Ni kweli yametokea, nasema huko bungeni

Si China wala Korea, tena pia si Omani

Hapa kwetu Tanzania, ninawajuza juweni

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

6
Ya tisa kakumbushia, amri hiyo ya dini

Vya watu kutamania, ni kujitia dhambini

Muumba kakatazia, kufuatisha shetani

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

7
Kwa vazi kukamilia, kofia iwe kichwani

Mdada kainyakua, akaingia mitini

Alibaki kaduwaa, mfadhaiko kichwani

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

8
Mkewe ana sheria, kuinyakua kichwani,

Kufuru ka kufuria, kawaeleza bungeni

Si haki wala sheria, mdada atakiani?

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

9
Ni mwisho ninaishia, kalamu naweka chini

Kwa kina ‘meelezea, kofia huko bungeni

Mdada alonyakua, si mke wake wa dani

Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!

Wakatabahu,

Choveki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom