Kisa cha Mzuka Bungeni

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
458
171
Kisa cha kweli mzuka!

1
Kisa cha kweli mzuka, ulipotajwa bungeni

Ilikuwa heka heka, ninawajuza juweni

Walihamaki mzuka, u wapi hapa bungeni?

Ni mtihani mzuka, unapotajwa bungeni!

2
Aliposema mzuka, nawajulisha bungeni

Siyo uzushi mzuka, alipotaja bungeni

Hakuna aliyecheka, waheshimiwa bungeni

Kisa cha kweli mzuka, ulipotajwa bungeni

3
Mzuka ama mizuka?, wakamuhoji bungeni

Tahadharia mzuka, usijetaja bungeni

Aliposema mzuka, walihamaki vichwani!

Kisa cha kweli mzuka, ulipotajwa bungeni

4
Nikikumbuka nacheka, mzuka huko bungeni

Waliingiwa mashaka, hawakutaka utani

Ilikuwa patashika, na heka heka bungeni!

Kisa cha kweli mzuka, ulipotajwa bungeni

5
Hakika neno mzuka, halitajiki bungeni

Linawatia mashaka, vichwani mwao juweni

Usiutaje mzuka, unapofika bungeni

Kisa cha kweli mzuka, ulipotajwa bungeni

6
Wa nani huo mzuka, na humu wataka nini?

Maswali ya uhakika, waliuliza bungeni

Waliyapata mashaka, wakasinyaa usoni

Kisa cha kweli mzuka, ulipotajwa bungeni

7
Kaditama nimefika, kituo changu mwishoni

Nimeeleza mzuka, ulipotajwa bungeni

Ni wengi walishituka, kwa woga pia huzuni

Ni mtihani mzuka, unapotajwa bungeni!

Choveki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom