Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 57,240
- 90,297
October 26, 1979 huko Korea Kusini kulitokea kisa cha ajabu cha mkuu wa ujasusi wa shirika la Korea Kusini(KCIA) Kim Jae-gyu kumtwanga risasi mbili boss wake rais wa Korea Kusin Park Chung-hee na bodyguard wake mkuu Cha wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku. Inasemekana mzozo wa wawili hao ulikuwa wa muda mrefu sana ukihusisha tofauti za jinsi rais Park alivyokuwa akitawala nchi kwa ushauri wa bodyguard wake Cha ambaye ndiye alikuja kuwa mtu wa karibu zaidi na mshauri Park kadri upinzani wa utawala wake ulivyoongezeka.
Siku yenyewe ya tukio ambayo ilikuwa ni katika hafla ya chakula cha usiku Kim akiwa ameshawapanga watu wake kwamba atamshughulikia Cha, Cha alikuwa akimlaumu Kim kwamba alikuwa ameshindwa kumshughulikia vizuri kiongozi mkuu wa upinzani wa nchi hiyo ambaye chama chake kilikuwa kimetoka kushinda viti vingi zaidi vya ubunge na alikuwa akiwaomba mabeberu wa Marekani kuutelekeza na kuupa mbinyo zaidi utawala wa rais Park ili kuipa fursa demokrasia. Inasemekana kila mara Kim Jae alipokuwa anajaribu kukatisha na kuiondisha mezani hiyo mada Cha alikuwa akiirudisha kwa nguvu na msisitizo zaidi hadi boss wake rais Park naye akaungana na bodyguard wake Cha kumkaripia na kumzodoa mkuu wake wa ujasusi Kim kwa uzembe wa kushughulika na upinzani, ndipo Kim aliporushiana nao maneno akatoka nje akurudi na bunduki na kuanza kuwatandika risasi Rais Park, Cha na walinzi wengine wanne, wote walikufa Kim naye akakamatwa akanyongwa na huo ndio ukawa mwisho wa utawala wa kidikteta wa miaka 18 wa rais Park.
Kim Jae-gyu anachukiliwa kama mtu aliyekuwa na mkanganyiko/dillema kubwa sana na mkuu wa ujasusi wa kipekee na tofauti wa KCIA kuwahi kutokea, kwa upande mmoja alionekana kuipenda demokrasia na kuhusiana na wadau wa demokrasia nchini Korea wakiwemo viongozi wa upinzani na maaskofu wa Katoliki, kwa upande mwingine kuna matukio mabaya ya wapinzani na wakosoaji wa Park kuuwawa na kupotea yeye akiwa mkuu wa KCIA. Inasemwa Kim mwenyewe hakufurahia kuteuliwa kuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Korea(KCIA) lililokuwa katili na la kuogopeka sana enzi za utawala wa dikteta Park lakini aliikubali hiyo nafasi hiyo mwaka 1976 akiamini ilikuwa ni fursa kwake ya kuweza kumshauri rais Park kuruhusu kubadili katiba mbovu ya nchi iliyojulikana kama Yushin na kuruhusu demokrasia kuchukua mkondo wake.