Kisa cha Jamaa yangu kuachwa na Mpenzi wake kisa umasikini

Kisa cha Jamaa yangu kuachwa na Mpenzi wake kisa umasikini

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,711
Habari zenu wanajanzi.

Nimekuwa kwenye mahusiano na dada mmoja Muda mrefu sasa. Ninampenda sana kwakweli. Nimekuwa nikijipinda sana ili kumfurahisha kwani nimekuwa nikimnunulia viatu, mikoba, nguo hata vito mbalimbali ili apendeze.

Pia, kutokana na yeye kumaliza Chuo kikuu na kukosa ajira, nilimsaidia kufungua biashara kwa kuchukua mkopo katika taasisi fulani ya mikopo huku nikiweka rehani Nyumba ya wazazi wetu.

Ni mwanamke ambaye nimejitahidi sana kuonesha upendo wangu kwake, nampikia, namfulia nguo na muda mwingine hua namuogesha pale tunapooga pamoja.

Matatizo yalianza pale nilipoenda kumtambulisha kwa ndugu zangu kwa sababu Wazazi wangu walishafariki. Nilifanya hivyo ili asije kudhani nampotezea muda wake.

Kimsingi mimi ndiye naetegemewa na familia yangu kwa sababu ndio Mkubwa kwa wote. Ninawasomesha wadogo zangu wawili wa Kike pamoja na mvulana mmoja kwa kuunga unga hivyo hivyo. Kwa kweli hali sio nzuri kiuchumi kivilee.
Baada ya kumtambulisha mpenzi wangu kwa ndugu zangu, kiukweli walimpenda na kumheshimu sana.

Lakini tulivyorudi, alibadilika kabisa. Nikawa kero kwake. Hapokei simu zangu wala kujibu text zangu. Kama angepokea basi angeniambia niongee nachotaka kumwambia kwani yuko bize.
Sijui tatizo ni nini ila kwakuwa nimekubali kuwa mfungwa wa penzi lake ndio maana nimeamua kuwa nakomaa nae hivyo hvyo.

Siku moja baada ya kutowasiliana wala kuonana nae siku tatu mfululizo niliamua kwenda mahala nilikomfungilia biashara.

Huwezi amini, alinifukuza na kuniambia hayuko comfortable kuwa na mimi na anataka uhuru wa kufanya mambo yake. Mimi ni mtu Mkimya na hua sipendi ugomvi, hivyo, nilirudi nyumbani kwangu.

Ila kwa uchunguzi wangu wa awali naona kabisa ameshapata mtu mwingine tajiri na ameshaona mimi simfai kwa sababu ya mzigo wa familia yangu nayoihudumia. Pia, nafahamu anafanya hivyo kwa sababu anajijua ni mzuri na ni msomi.

Naumia sana Brother, kwani yule mwanamke nampenda sana na nimewekeza vitu vingi sana kwake. Nilipanga Mwaka huu mwezi wa Kumi nifunge nae Ndoa. Lakini muda wote wa mahusiano hakutaka niende kupiga hodi kwao.

Nimepoteza matumaini na mahusiano, moyo wangu umevunjika vipande vipande.
Napitia wakati Mgumu sana Bro wangu maana nashindwa kabisa kumtoa moyoni huyu Mwanamke. Kila napomuona Online WatsApp au Status zake moyo unaniuma mno ukizingatia hajibu texts zangu.

Aliacha nyumbani kwangu baadhi ya Nguo zake, hali inayozidi kunipa machungu. Sijui nini cha kufanya. Najua kwake It's over ila kwangu nafsi inagoma kumsahau. Nisaidie kwa mawazo nifanye nini Mimi....
 
ulikosea hapo kuwa karibu nae hawa viumbe kadiri unavyomuweka karibu yeye ndio anazidi kukuweka mbali nawe.
Mwambie kama aliweza kuacha kunyonya maziwa ya mama yake huyo ni nani asiweze muacha amuache aende ...huko aendako dunia itamfunza
 
Hivi kwanini wanawake wa enzi hizi wana ROHO MBAYA sana??
Kwanini lakini??

Stori hii imeniuma na ya Zero IQ ndo imeninyong,onyeza kabisa daah

Halafu hawaachi kulialia oooj wanaume kumbe wao ndo washenzi wa kutupwa, Mungu anawaona
 
1. Ukimfungulia mwanamke biashara imiliki wewe, akikuzingua kama hivo anashtukia kesho anakuta kofuli kubwa na bango TUMEFUNGA BIASHARA HAPA!

2. Hata gari ukimnunulia limiliki wewe siku akizingua ni unatuma mtu akufiatie gari lako akapaki nyumbani

3. Usipende mwanamke asiye mkeo, wewe danganya danganya mpaka anyooke

4. Unawazaje kumuoa mtu usiyejua kwao? Usioe au kufikiri kuoa sehemu usiyoifahamu

5. Mwanamke asiyependa ndugu zako kaa naye mbali hakufai kama mke.

Mwambie jamaa yako akumbuke haya. Yeye ni kaka wadogo zake wanamtegemea asirudi kuweka nyumba ya urithi rehani.
 
Wanaume kama wewe tumebaki wachache sana, Mungu akuimarishe ktk msimamo wako Chifu.
1. Ukimfungulia mwanamke biashara imiliki wewe, akikuzingua kama hivo anashtukia kesho anakuta kofuli kubwa na bango TUMEFUNGA BIASHARA HAPA!

2. Hata gari ukimnunulia limiliki wewe siku akizingua ni unatuma mtu akufiatie gari lako akapaki nyumbani

3. Usipende mwanamke asiye mkeo, wewe danganya danganya mpaka anyooke

4. Unawazaje kumuoa mtu usiyejua kwao? Usioe au kufikiri kuoa sehemu usiyoifahamu

5. Mwanamke asiyependa ndugu zako kaa naye mbali hakufai kama mke.

Mwambie jamaa yako akumbuke haya. Yeye ni kaka wadogo zake wanamtegemea asirudi kuweka nyumba ya urithi rehani.
 
Alafu nimepishana na gari la Bank hapa wanakuja kupiga mnada hiyo nyumba ya wazazi wako uliyoweka rehani [emoji23][emoji23]

Ushauri wangu ukilala lala na sumu ya panya maana yajayo kwako ni ya kusikitisha!
 
Back
Top Bottom