Kisa cha Frola wa Kisutu

Kisa cha Frola wa Kisutu

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,969
Ndugu wa JF nina wasalimia kwapamoja.
Kwa muda mrefu nimepotea JF nilikuwa maporini nikikata miti ya kutengeneza mkaa.

Sasa ngoja nirudi kwenye mada. Ilikuwa mwaka 1992, kipindi kile nilitoroka nyumbani kuja kutafuta maisha hapa dar. Maisha hayakuwa mabaya sana. Niliajiriwa kuwa muuza duka la mzee Khatibu Musa maeneo ya kisutu. Mungu amulaze mahali pema peponi mzee wa watu {amina}

Kusema kweli oh nilikuwa kijana ninayevutia, mabinti walikuwa wakinita "Kindorobo" sikuelwa kwa nini. Stori za hapa na pale, ucheshi na hadith za vijijini zilipa umarufu pale kisutu.

Nakumbuka kabisa ilikuwa ni siku ya Jumatano Binti mwenye shingo ya twinga, mwendo wa kinyonga alikuja dukani kununua sabuni ya KOMESHA vipande viwili.

Kweli damu ilisimama kwa mda wa sekunde 30 hivi sikuweza kuongea. eheh bana mtoto akachukua sabuni na kuondoka zake.

Sasa picha ya huyo binti iliganda kwenye akili zangu kila wakati ilikuwa ikizunguka kwenye ubogo wa mbele, kati na nyuma. Kusema kweli huyo binti aliziteka hisia zangu zote.

Basi unajua sisi wanaume ni kama simba, lazima uwinde na kama hujui mbinu za kuwinda mazingira yatakufundisha. Ni azisha project ya kuwinda binti wa watu.

Mungu si athumani, nilikuwa naelekea dukani nikakutana naye njiani. Aaah si unajua vijana wa vijijini hatunaga uoga!! nikarusha mtego wangu wa kwanza aaah mtoto akanasa kama matani vile.

Wakati huo mimi nilikuwa na kigeto cha uongo na kweli nikamuambia aje getoni tupige stori mtoto akasema poa atakuja saa nne usiku. Siku hiyo nilikuwa nikumuwaza Flora tu mtoto wa KiArusha nywele mpaka kiunoni.

Bana nilifunga duka saa mbili kuenda kujiandaa. Kila wakati nilikuwa nikiangalia saa. Saa nne kamili hakutoke na nusu hakutokea. Lakini saa tano kamili nilisikia mlango ukigongwa, kuufungua mlango kumbe ni Flora mwenyewe.

Tukakaa kwenye godoro langu la kiaina tukapiga stori za hapa na pale. Mtoto akaregea dah nikasema hapa si ndio wakati wenyewe. Mara mtoto macho akayatoa, huku akirusha miguu huku na kule. Aise sikuelewa ni mbwebwe au nini. Baadaye alitokwa mapovu meupe mdomoni.
Dah mtoto kimya haongei tena.

Aise nikagundua Flora ana matatizo ya kifafa sasa nifanye nini.
Nilikuwa niko na shilingi elfu mbili usiku huo nilikimbia na kesho nikasafiri kurudi nyumbani kijijini na kuamua kurudi shule na nilisoma kwa nguvu sana.
 
Kumbe kupenda kusoma hadi ukutane na mwenye kifafa? Usifanye wenye navyo wakaanza kupotea maana mitoto ya siku hizi haipendi shule kazi kuchora zombiz
 
Kumbe kupenda kusoma hadi ukutane na mwenye kifafa? Usifanye wenye navyo wakaanza kupotea maana mitoto ya siku hizi haipendi shule kazi kuchora zombiz
Hilo nitukia langu tu sijui wengine visa vyao. Ni tukio langu tu sijui wengine.
[MENTION]Kongosho[/MENTION]
 
sasa hivi uko darasa la ngapi? Hii stori nzuri kuwahadithia watoto wenzako saa nne wakati mukiwa mapumziko.
 
sasa hivi uko darasa la ngapi? Hii stori nzuri kuwahadithia watoto wenzako saa nne wakati mukiwa mapumziko.
Mwaka 1993 nilianza form one. Sijui sasa nitakuwa darasa la ngapi hebu kisia!!?
 
dont say ukakimbia na kila kitu chako ukaacha geto..
kwani kifaa ni kifo? ungesubiri arui katika hali ya kawaida uzungumze nae
kifaa ni wrong signals zinazotokea katika mwili wa binadamu
elewewa mwili wako ni kama mashine na ina umeme wake,
inapotokea shoti ya umeme ndio hivo hivo mwili wetu unakuwa.....
we una riho mbaya kijana kumkimbia dada wa watu,,anyway ahsante kwa hadithi nzuri ya kutunga
 
Back
Top Bottom