Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Kisa cha kufukuzwa kazi mtumishi wa serikali (anaedaiwa kuchana juzuu) kimenikumbusha kisa cha daktari fulani wa macho Muhimbili mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80.
Huyo Daktari alipata scholarship kwenda Ujerumani Magharibi (kusomea taaluma ya macho shahada ya kwanza). Alifanya vizuri sana na Wajerumani wakamuongezea nafasi ya kusomea shahada ya pili, lakini kwa kuwa ruhusa (study leave) ilikuwa imeisha alilazimika kurudi nyumbani kuomba ruhusa upya kabla ya kuendelea na masomo.
Enzi hizo ilikuwa ni lazima mtu afanye kazi japo miaka miwili kabla hajarudi tena masomoni; na kwa kigezo hicho, daktari huyo hakupewa ruhusa, ila alishauriwa kusubiri miaka miwili. Ilipopita hiyo miaka akanyimwa tena ruhusa, na tena na tena.
Daktari akapata "kichaa" hadi kulazwa wodi ya vichaa. Kule Ujerumani wakaamua kumfuatilia kujua ni kwanini hakurudi kuendelea na masters yake (official correspondence ya Muhimbili kwenda Ujerumani ilikuwa: Jamaa ana kichaa kwa hivyo tunamteua mtu mwingine aje badala yake). Wajerumani wakamtuma supervisor wake kuja kuthibitisha. Na kweli wakamkuta mwanafunzi wao psychiatric ward na akiwa huko zaidi ya miaka miwili.
Supervisor alipomu-assess aliwaomba akae naye hotelini kwa siku 2. Daktari "kichaa" akapelewa Motel Agip na ndani ya saa 36 alishabadilika.
Wajerumani wakamchukua na alikuja kuwa specialist wa macho wa kutegemewa. Assume huyo Daktari asingefuatiliwa na hao Wajerumani angeishiaje? Tuna ma-specialist wangapi kwenye fani tofauti tuliowapoteza kwa kuwa tu hatuoni umuhimu wa kuponyesha badala ya kuadhibu?
God have mercy on this country.