Kisa cha bikira wa mobutu

Kisa cha bikira wa mobutu

Tukio hili lilitokea mwishoni mwa miaka ya sabini katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo ambayo kwa wakati huo ilijulikana kwa jina la utani " nick name " la Zaire.

Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo ilitangaza kwamba Serikali ya Rais Mobutu Sesseseko inatoa scholarship ya kwenda kusoma nchini Ufaransa kuanzia ngazi ya primary hadi Chuo Kikuu na baada ya masomo wahitimu wote wangepata nafasi nzuri za kazi katika sekta mbali mbali nchini huko.

Sifa za mwombaji alitakiwa awe msichana mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na mbili na kuendelea na alitakiwa kuwa bikira...

Wazazi wengi nchini humo walichangamkia fursa hiyo na kuwapeleka binti zao ili wapate hizo nafasi.

Walijitokeza mabinti wengi sana ..Idadi kamili haijulikani ..Wapo wanaosema walikuwa zaidi ya mia NNE na wapo wanao sema walikuwa wanakaribia kufika elfu moja. .

Siku ya uzinduzi wa project hiyo mabinti wote walio jitokeza walipakiwa kwenye meli kubwa NNE na kupelekwa Brazzavile kwa ajili ya kufanya shopping.

Wakati meli hiyo inarudi ilipata ajali na mabinti wote walikuwa ndani ya meli hiyo walipoteza maisha yao .

Conspiracy theory zinasemaje kuhusu tukio hilo :

Wacongo wanaamini kuwa mabinti hao walitolewa kafara na Mobutu ikiwa ni maelekezo ya waganga wake ..
Wacongo wanaamini kuwa mabinti hao walichinjwa kwanza halafu miili yao ndio ikaenda kuwekwa kwenye meli ambayo baadae ilizamishwa huku lengo likiwa kile kinachoitwa dressing the scene.

Mobuto alikuwa na utaratibu wa kufanya matambiko mazito mazito ya Mara kwa Mara kwa ajili ya kuulinda ufalme wake pamoja na kujiongezea nguvu za kiroho.

Serikali ya Congo iliwaomba radhi wazazi wa mabinti hao kwa ajali iliyotokea na wazazi wote walilipwa fidia...
Duh duniani kuna mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa kuabudu ulozi watu wa congo, hii itakuwa kweli maana nasikia(ga) bikra inapendwa kwa mambo hayo
 
Back
Top Bottom