Kisa cha abunuasi na tamaa ya utajiri

Deo bony

Member
Mar 27, 2011
74
8
Basi hapo mwanzo abunuasi alibahatika kuwa na mbuzi jike hivyo basi akawa na fikra za kuwa tajiri hapo baadae kwani alijua kwamba ipo siku ambapo mbuzi wake angezaa na yeye angekuwa tajiri kwa kuwa na mbuzi wengi.Basi siku moja alienda nambuzi wake malishoni na wakati alipokuwa anatembea mara akaona kiatu kizuri sana tena cha gold njiani lakini kutokana na upungufu wake wa mawazo hakukiokota kile kiatu akaamua kuendelea na safari basi baada ya mwendo kama wa masaa mawili aliona kiatu kingine cha gold yaani mwenza wa kiatu kile cha mwanzo,safari hii aliamua kukiokota kile kiatu akakiweka sehemu ambapo alimfunga mbuzi wake na kuamua kurudi kukifwata kiatu cha mwanzo kwa bahati mbaya alipofika eneo husika hakukikuta kiatu kile ndipo alipoamua kumrejea mbuzi wake pamoja na kiatu cha pili alicho kiacha cha kushangaza hakumkuta mbuzi wala kiatu ndipo alipoanza kuhuzunika na kulia kwani ndoto yake yakuwa tajiri ilikuwa imetoweka .MWISHO
 
stori nyingine ni: Kulikuwa na sherehe kubwa kwa mfalme na akaalika watu kibao matajiri, kwenye eneo hilo kulikuwa na maskini mmoja alikuwa na njaa sana ila ndio hivyo hakualikwa kwenye sherehe. Ndani alikuwa na kiporo chake cha wali akakichukua na kukaa nje akisikilizia harufu ya msosi toka kwa mfalme, akala kiporo chake kwa kusindikizia ile harufu nzuri ya chakula.
Alipomaliza akanywa maji akaenda kwa mfalme kumshukuru kwa kushiba! mfalme alikasirika sana akamkwida aeleze ni vipi amekula chakula chake wakati hakualikwa, kesi ikapelekwa barazani itolewe hukumu kesho yake. maskini akaenda kwa abunuwasi kuomba msaada kwani alijua faini atayopewa hatoweza kulipa, abunuwasi akamwambia tulia kesho tutaenda wote. asubuhi wakaenda, maskini akaambiwa alipe faini, abunuwasi akaenda mbele ya mfalme akamuuliza 'ulimualika maskini?' akajibu hapana, sasa alikulaje chakula chako? akamwambia amekula harufu. abunuwasi kamjibu sawa, basi ngoja nikupe faini yako.
Akatoa sarafu kadhaa mfukoni mwake akaziangusha chini zikazagaa kwa kelele nyingi, zilipotulia akazichukua na kuzirudisha mfukoni, kisha akamwambia mfalme' kama maskini alikula harufu akashiba, basi umelipwa faini kwa mlio wa sarafu uridhike!'
 
Vitu vingine vinavyoandikwa humu si lazima ucheke au unune ila jitahidi uishughulishe akili yako upande wa pili wa shilingi.
Welevu wananielewa.
 
Vitu vingine vinavyoandikwa humu si lazima ucheke au unune ila jitahidi uishughulishe akili yako upande wa pili wa shilingi.
Welevu wananielewa.
All stories are good.
 
huu uzi umerudiwa! tazama chini.

Basi hapo mwanzo abunuasi
alibahatika kuwa na mbuzi jike hivyo basi akawa na fikra za kuwa tajiri
hapo baadae kwani alijua kwamba ipo siku ambapo mbuzi wake angezaa na
yeye angekuwa tajiri kwa kuwa na mbuzi wengi.Basi siku moja alienda
nambuzi wake malishoni na wakati alipokuwa anatembea mara akaona kiatu
kizuri sana tena cha gold njiani lakini kutokana na upungufu wake wa
mawazo hakukiokota kile kiatu akaamua kuendelea na safari basi baada ya
mwendo kama wa masaa mawili aliona kiatu kingine cha gold yaani mwenza
wa kiatu kile cha mwanzo,safari hii aliamua kukiokota kile kiatu
akakiweka sehemu ambapo alimfunga mbuzi wake na kuamua kurudi kukifwata
kiatu cha mwanzo kwa bahati mbaya alipofika eneo husika hakukikuta kiatu
kile ndipo alipoamua kumrejea mbuzi wake pamoja na kiatu cha pili
alicho kiacha cha kushangaza hakumkuta mbuzi wala kiatu ndipo alipoanza
kuhuzunika na kulia kwani ndoto yake yakuwa tajiri ilikuwa imetoweka
.MWISHO
 
Back
Top Bottom