Kirusi cha Corona ni Kirusi kwa Uchumi pia

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
420
670
A0A507E9-E219-4CEE-BE71-641C343383F6.jpeg


Kirusi cha Corona, sio tu ni kirusi kinachoathiri watu kiafya pekee, bali kiuchumi pia. Na kuna uwezekano mkubwa wa uchumi kubadilika kwa kipindi hiki.

Had sasa kirusi hiki kimeshaathiri burudani, usafiri na utalii kwa kiasi kikubwa kwa kuwa ni shughuli hizo zimepata zuio la wazi. Mambo mengine yanakutana na zuio kama derivation yamambo yanayoendelea.

Inaweza ikaleta shida kubwa kiuchumi kuliko 2008-2009. Huu ndio muda watunga sera, wachumi na wataalamu wengine wanapaswa kuonyesha umahiri wao.

Hili swala kwa kiasi kikubwa limeathiri biashara, mashirika ya ndege yamesitisha safari zake, nchi zimefunga mipaka kuzuia utalii. Kama haitoshi inakadiliwa kuwa tatizo linaweza kuongezeka na kuua takriban watu milioni 60 upotevu utakao fanana na vita ya pili ya dunia

Kama litadhibitiwa hata mwaka huu, kuna uwezekano mkubwa mwaka 2021 ukawa mwaka wenye ugumu.

Hadi sasa tayari ‘demand and supply’ zimeshaathiriwa na masuala ya uwekezaji yamepungua kwa kuwa ni ngumu kupata faida kwa kipindi hiki ambacho yapo mazuio mengi.

Katika yote hayo maana yake hata serikali inaathrika kwa kukosa kodi na tozo mbalimbali kama vyanzo vya mapato.

Wakati nimesoma kuhusu mapendekezo ya Zitto kuhami uchumi wa tanzania, Niliwaza swala lake la kuwafidia wafanya biashara, na niliona ugumu katika hilo kwa kuwa hata serikali sidhani kama itakuwa na fedha kuwalipa wafanya biashara kwa muda usiojulikana, labda waje kufidiwa baada ya tatizo kuisha na watu kuangalia hasara kamili waliyoipata kipindi hiki cha hili gonjwa.

Ieleweke kuwa, sio lazima tuugue au tufe sana ili kuona madhara ya kiuchumi ya hili gonjwa bali hata walioathirika hadi sasa wanaelewa, mathalini waliokuwa wanawauzia chakula watoto wa shule.

Hii ni hali ya hatari, na ni vyema basi wataalamu wakae kukadiria madhara na kupendekeeza suluhu kabla mambo hayajawa mabaya. Katika andiko langu lililopita niliuliza, siku 30 halafu kitu gani? Kwa hizi sikuthelathini za kuhami watu kuambukizwa ziwe siku thelathini za kupima na kutoa mapendekezo ya kuhami afya za watu na uchumi wa nchi

Na kama hatutaona matatizo yanayoweza kutokea kichumi basi iko hatari kubwa ya kuingia madeni makubwa kama nchi mara baada ya hili gonjwa kupita

Katika hii emergency ya kiuchumi, ni haki kuchukua hatua za kiuchumi kuhami baadhi ya benki kuu za nchi nyingine wameanza kuchukua hatua hizo ili kuongeza hali ya ukwasi kwa watu wao, bado sijona tamko la nchi yetu,

Ni vyema kutathmini madhara ya kiuchumi ili kujua namna bora ya kuhami uchumi wetu kwa kipindi hiki cha gonjwa hili


Signed!

Oedipus
 
Back
Top Bottom