LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,349
- 36,303
[h=5][/h][h=5] Jamaa mmoja kipofu kaenda mgahawani, alipofika akaletewa orodha ya misosi ila akamwambia meneja: mimi ni kipofu, siwezi kuona. Nenda jikoni niletee kijiko ambacho kimetumiwa lakini hakijaoshwa. Nitakinusa halafu ntakwambia nataka chakula gani. Meneja akashangaa ila akaenda akamletea, kipofu akakinusa akamwambia meneja: nataka hiki kinachonukia, viazi na nyama. Hivyo hivyo. Meneja akashangaa kwamba kweli mteja aliyetumia kile kijiko alikula viazi na nyama. Basi jamaa akaletewa msosi akala akaondoka zake. Siku ya pili akaja mchezo ukawa ule ule, ananusa kijiko, anapatia analetewa msosi, anakula anasepa. Siku ya tatu meneja wa hoteli akamwambia mkewe ambaye alikuwa ndo mpishi: yule kipofu akija leo ngoja nimjaribu. Mchana ukafika kipofu akaenda kuagiza msosi. Meneja akaenda jikoni akamwabia mkewe (alikuwa anaitwa Mwajuma) hebu weka hiki kijiko kwenye kwapa lako, ni kisafi, kiwe tu na harufu yako nataka kutesti akili ya huyu mtu. Wife akakubali, akakiweka kwapani, kipofu akapelekewa. Kipofu akakinusa halafu akasema: Sikujua kama Mwajuma anafanya kazi hapa!
Imeandikwa na Masanja Mkandamizaji kwenye ukurasa wake wa Facebook.
[/h]
Imeandikwa na Masanja Mkandamizaji kwenye ukurasa wake wa Facebook.
[/h]