Kipindi cha viwanjani cha AZAM 2 leo kilikuwa ni zaidi ya kipindi cha michezo

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
Leo nimebahatika kusikiliza kipindi cha AZAM cha viwanjani, katika siliza yangu nimegundua walichokuwa wakikiongelea ni zaidi ya michezo, lakini wametumia michezo kufikisha ujumbe.
Walipokuwa wanaongelea juu ya mchezo wa simba na ile timu ya misri wamesema kuwa watanzania hatujui kudai haki zetu...lilipokuwa likitokea jambo wachezaji wa misri kwa umoja wao walikuwa wakienda kumzonga refa tu lakini wachezaji wa tanzania walikuwa hawafanyi hivyo, wakasema aliyekuwa anajaribu kufanya hivyo ni Okwi peke yake ambaye ni Mganda, wakasema waganda nao wanajua kudai haki maana hata ukiangalia namna upinzani unavyodai haki ni tofauti na tanzania, wakasema sisi watanzania ni waoga..wakatolea mfano wa wafanyakazi kuwa wanaweza kuwa wanazurumiwa haki zao lakini wakawa kimya wanagugumia mioyoni, akitokea mtu wa kujitoa mhanga kwenda kudai haki wao hujifanya wapo nyuma yake..yule mfanyakazi akishikishwa adabu yake tu kwa kufukuzwa kazi hao waliokuwa nyuma yake hutawaona. Wakasema yawezekana mfumo umetulea hivyo kuwa lazima awepo kiongozi wa kutusaidia maana toka darasani tunaambiwa mamonitor au viranya ndo wa kutudaia haki il ukiwa wa kawaida huwezi..yaani lazima awepo mtu wa kutufanyia jambo.

Wanasema watz tumezoea kukimbia matatizo mfano upo karibu na shule ya serikali ukiona inafanya vibaya unamchukua mtoto wako unampeleka shule binafsi halafu unakaa kimya kumbe suluhisho ilikuwa ni wewe kudai elimu nzuri kwenye ile shule..wakatoa mfano mwingine kuwa umeme ukikatika sisi tunanunua majenereta au sola na maji yakiwa hakuna tunajichimbia visima vyetu...wakati suluhisho ilikuwa ni kudai upatikanaji bora wa hizo huduma..kwa vile hatujui kudai mambo yanakaa hovyo ndo maana hata tukiwa na raisi mkali kiasi gani mambo ya serikali yanaenda hovyo tu.

Wakaja pia wakaongelea kuhusu uwajibikaji..kwa kutumia mechi hiyo hiyo wakasema walitegemea ama viongozi wa soka ama wa serikali kuwajibika ama kwa kutolea maelezo kwanini umeme ulikatika uwanjani au kwa kuwachukulia watu hatua za kinizamu. Wamemlaumu waziri wa michezo kwa kukaa kimya kwa kosa kama hilo hasa kwenye mechi kama hiyo.

Wameongelea ishu ya mapato, wanasema mechi hizi mbili zimeingiza milioni mia na kitu tu wakati mechi moja miaka ya numa ya TP mazembe iliingiza zaidi ya milioni mia nne...japokuwa hawajasema moja kwamoja ila hii inamaanisha hata uwezo wa watu kupata pesa tu za viingilio vya mechi umekuwa mgumu manaake uchumi wa mtu mmoja mmoja umekuwa shida.

Nimeona kipindi hiki wameongelea zaidi ya michezo kwasababu wametoka hata nje ya michezo kwa kuhusianisha na mambo mengine, hii manaake nini ni kwamba "samaki ana mengi ya kuongea ila ndo hivyo yuko ndani ya maji"

Sio hao tu ambao wanatafuta nafasi ya kuongea hawapati ila kuna wengine wana mengi ya kuongea ila hawana nafasi ya kufanya hivyo
 
Imekaa njemaaa...wanafunzi wa vyuo wanaposimama na kudai haki utasikia mijitu mizima eti hao watoto hanajihusisha na siasa hawasomi... Poor Tanzanians
 
Hiyo ni tafsiri yako, siku hizi hata mtu akijamba watu watatafuta njia ya kuunga dots na kusema uchumi na maisha magumu kwa ujumla.
 
na mi nimepata fursa ya kukishuhudia nadhan ezekiel kamwaga ndio kamwaga nondo za hatari kuliko wote
 
Walijadili vizuri sana...wanaeleza kwa ufasaha na kwa mitego hivi....kama wanaongelea michezo lakini wanatoka wanatudi halafu wanatoka tena
 
Huo ndo ukweli!
Sampuli ya Binadamu wa Tanzania, huipati popote Duniani...
Made in Tanzania only....!
Watanzania wengi ni Mazuzu sio uongo.
 
Leo nimebahatika kusikiliza kipindi cha AZAM cha viwanjani, katika siliza yangu nimegundua walichokuwa wakikiongelea ni zaidi ya michezo, lakini wametumia michezo kufikisha ujumbe.
Walipokuwa wanaongelea juu ya mchezo wa simba na ile timu ya misri wamesema kuwa watanzania hatujui kudai haki zetu...lilipokuwa likitokea jambo wachezaji wa misri kwa umoja wao walikuwa wakienda kumzonga refa tu lakini wachezaji wa tanzania walikuwa hawafanyi hivyo, wakasema aliyekuwa anajaribu kufanya hivyo ni Okwi peke yake ambaye ni Mganda, wakasema waganda nao wanajua kudai haki maana hata ukiangalia namna upinzani unavyodai haki ni tofauti na tanzania, wakasema sisi watanzania ni waoga..wakatolea mfano wa wafanyakazi kuwa wanaweza kuwa wanazurumiwa haki zao lakini wakawa kimya wanagugumia mioyoni, akitokea mtu wa kujitoa mhanga kwenda kudai haki wao hujifanya wapo nyuma yake..yule mfanyakazi akishikishwa adabu yake tu kwa kufukuzwa kazi hao waliokuwa nyuma yake hutawaona. Wakasema yawezekana mfumo umetulea hivyo kuwa lazima awepo kiongozi wa kutusaidia maana toka darasani tunaambiwa mamonitor au viranya ndo wa kutudaia haki il ukiwa wa kawaida huwezi..yaani lazima awepo mtu wa kutufanyia jambo.

Wanasema watz tumezoea kukimbia matatizo mfano upo karibu na shule ya serikali ukiona inafanya vibaya unamchukua mtoto wako unampeleka shule binafsi halafu unakaa kimya kumbe suluhisho ilikuwa ni wewe kudai elimu nzuri kwenye ile shule..wakatoa mfano mwingine kuwa umeme ukikatika sisi tunanunua majenereta au sola na maji yakiwa hakuna tunajichimbia visima vyetu...wakati suluhisho ilikuwa ni kudai upatikanaji bora wa hizo huduma..kwa vile hatujui kudai mambo yanakaa hovyo ndo maana hata tukiwa na raisi mkali kiasi gani mambo ya serikali yanaenda hovyo tu.

Wakaja pia wakaongelea kuhusu uwajibikaji..kwa kutumia mechi hiyo hiyo wakasema walitegemea ama viongozi wa soka ama wa serikali kuwajibika ama kwa kutolea maelezo kwanini umeme ulikatika uwanjani au kwa kuwachukulia watu hatua za kinizamu. Wamemlaumu waziri wa michezo kwa kukaa kimya kwa kosa kama hilo hasa kwenye mechi kama hiyo.

Wameongelea ishu ya mapato, wanasema mechi hizi mbili zimeingiza milioni mia na kitu tu wakati mechi moja miaka ya numa ya TP mazembe iliingiza zaidi ya milioni mia nne...japokuwa hawajasema moja kwamoja ila hii inamaanisha hata uwezo wa watu kupata pesa tu za viingilio vya mechi umekuwa mgumu manaake uchumi wa mtu mmoja mmoja umekuwa shida.

Nimeona kipindi hiki wameongelea zaidi ya michezo kwasababu wametoka hata nje ya michezo kwa kuhusianisha na mambo mengine, hii manaake nini ni kwamba "samaki ana mengi ya kuongea ila ndo hivyo yuko ndani ya maji"

Sio hao tu ambao wanatafuta nafasi ya kuongea hawapati ila kuna wengine wana mengi ya kuongea ila hawana nafasi ya kufanya hivyo

Sawa kabisa...wangeongelea pia unafiiki wa waandishi wa habari wa kuandika matatizo ya wengine na kuacha yao...utaona au kusikia wanaandika au kutangza kuwa Wachezaji wa timu fulani hawajalipwa mishahara miezi minne...lakini kumbe vipo vyombo vingi vya habari nchini hawawalipi mishahara wafanyakazi wao wakiwemo waandishi wa habari mishahara hata ya miezi mitano au sita...Waandishi wa habari nao waweke wazi matatizo yao..utawaona au kusikia wanasema serikali inaminya uhuru wa vyombo vya habari...Lakini hawaandiki namna wamiliki wa vyombo vya habari wanavyominya uhuru wa vyombo vyao kwa kuacha au kushindwa kuandika au kuweka wazi 'maovu' ya wamiliki hao
 
Sawa kabisa...wangeonelea pia unafiiki wa waandishi wa habari wa kuandika matatizo ya wengine na kuacha yao...utaona au kusikia wanaandika au kutangza kuwa Wachezaji wa timu fulani hawajalipwa mishahara miezi minne...lakini kumbe vipo vyombo vingi vya habari nchini hawavilipi mishahara wafanyakazi wao wakiwemo waandishi wa habari mishahara hata ya miezi mitano au sita...Waandishi wa habari nao waweke wazi matatizo yao..utawaona au kusikia wanasema serikali inaminya uhuru wa vyombo vya habari...Lakini hawaandiki namna wamiliki wa vyombo vya habari wanavyominya uhuru wa vyombo vyao kwa kuacha au kushindwa uandika au kuweka wazi 'maovu' ya wamiliki hao
haya matatizo ya maslahi ya waandishi ndio yamepunguza weredi wa waandishi...kwasababu hawalipwi kabisa ama wanalipwa kidogo imekuwa rahisi kuwekwa mifukoni mwishowe wamekuwa watu wa kuandika vitu vya ajabu ajabu sana
 
mwenye audio/video please! wengine hatuna access na AZAM. Personally nimependa uchambuzi wao kwa mujibu wa mleta taarifa. As you said, "samaki ana mengi ya kuongea ila ndo hivyo yuko ndani ya maji". Thanks for sharing bro. bless up
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom